Wanaouza mihogo wanajiita wajarisiamali

Wanaouza mihogo wanajiita wajarisiamali

Ujasirimali ni mtu mwenye kujituma asie taka kusubiri cha kugaiwa, ni mtu au watu wenye maono ya kujitegemea.

Wapo wajisirimali wanaanzia na kuuza mihogo leo kesho maadanzi kesho kutwa ana mgahawa wake mwenyewe. Kuwa mjaairimali ni njia ya kuanzia safari ya kutoka maisha duni na kuelekea maisha bora.

Jee. Unajua Bakhresa alipo anzia na alipo sasa?
Jee wajua alipo anzia vunja bei na alipo sasa?
Jee. Wajua kama Diamond platinum nae alikuwa mjasirimali wa mitumba unamuona jitihada zake leo alipo?

Hawa nao walikuwa wajasiri mali kabisa usidharau ajira ya mwenzako kwasababu hujui mwisho wako upoje.
Unaongea vitu vizuri lakini, haujaelewa point ya mleta Mada. Neno mjasiriamali linatumika mahali pasipo sahihi
 
Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.
Tanzania, nchi yangu 😅
Acha kupotosha,neno ujasiriamali ni muunganiko wa maneno mawili,ujasiri na amali,amali ni kazi,kuuza mihogo ni ujasiri wa Hali ya juu kwa kuwa wengi ukiwemo wewe hudharau,ujasiriamali siyo kubuni Jambo jipya linalosaidia jamii
 
Tafsiri ya neno ujasiriamali ni kitendo Cha kuumiza akili(brainstorming) na kubuni jambo ambalo halijawahi kuwepo kwa lengo la kuisaidia jamii. Mfano wa ujasiriamali ni kama vile ugunduzi za engine, kompyuta na n.k.

Sasa sikuhizi unakutana na mama muuza mihogo ya kukaangwa au mchicha anajiita mjasiriamali.
Tanzania, nchi yangu 😅
Hapo umechanganya Innovation na Entrepreneurship. Innovation kwa kiswahili ndo uvumbuzi ambacho ndo umeelezea hapa. Ujasiriamali ni kuanzisha biashara yoyote mpya au kuendeleza iliyopo lakini katika namna ambayo italeta faida. Sifa kuu ya mjasiriamali ni kutoogopa sana hatari zinazoweza kutokea kwenye mchakati wa biashara (Risks). Mjasiriamali sio lazima awe mvumbuzi. Na pia mvumbuzi sio lazima awe mjasiriamali.

Lakini kwa dunia ya sasa wavumbuzi wengi wamekuwa wajasiriamali pia kwa maana ya kuweka uvumbuzi wao kwenye biashara na kuanza kupiga noti ndefu. Wale wavumbuzi ambao hawakuwa wajasiriamali wengi wao waliishia kupata kiasi kidogo cha fedha au pengine kufa maskini huku akiwafaidisha wajasiriamali makini watakaouchukua uvumbuzi wake na kufanya biashara.

Kina Mark Zuckerberg, Bill Gates na wengine ni wavumbuzi na hapohapo wajasiriamali. Wapo wavumbuzi kama kina Newton tunawasifu ila kwenye upande wa biashara hawatajwi kabisa.

Ulivyotaja mihogo nimemkumbuka mama aliyekuwa anatuuzia mihogo pale mtoni karibu na kanisa la St Theresa, Arusha. Mungu ambariki sana yule mama kwa kutuwezesha wanafunzi kwenye suala zima la mihogo. Tuliokuwa tunaenda maktaba ya mkoa na tuition Arusha Sport mtakuwa mnamkumbuka yule mama. Nimalize kwa kusema wewe Restless Hustler ni mtu wa KUPUUZWA kwenye jamii ya watu wastaarabu.
 
Acha kupotosha,neno ujasiriamali ni muunganiko wa maneno mawili,ujasiri na amali,amali ni kazi,kuuza mihogo ni ujasiri wa Hali ya juu kwa kuwa wengi ukiwemo wewe hudharau,ujasiriamali siyo kubuni Jambo jipya linalosaidia jamii
Maana hii inakinzana na Tafsiri ya moja kwa moja ya entrepreneurship
 
Hapo umechanganya Innovation na Entrepreneurship. Innovation kwa kiswahili ndo uvumbuzi ambacho ndo umeelezea hapa. Ujasiriamali ni kuanzisha biashara yoyote mpya au kuendeleza iliyopo lakini katika namna ambayo italeta faida. Sifa kuu ya mjasiriamali ni kutoogopa sana hatari zinazoweza kutokea kwenye mchakati wa biashara (Risks). Mjasiriamali sio lazima awe mvumbuzi. Na pia mvumbuzi sio lazima awe mjasiriamal...
Bill gates alinunua zile codes kwa lecturer wa chuo,kwa Dola 50k za marekani
 
Kwa iyo muuza mihogo tunamuweka kwenye kundi gani sasa?
Mfanyabiashara ndogo ndogo. Ili aitwe entrepreneur (mjasiliamali) inabidi ajitofautishe na wauza mihogo wengine kwa kuongeza thamani ya mihogo yake. Utofauti ndio utakaomfanya aitwe mjasiliamali
 
Back
Top Bottom