Wanaowazika kishujaa waliokufa kwenye maandamano wanakosea?

Wanaowazika kishujaa waliokufa kwenye maandamano wanakosea?

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Itakuwa umeona video mbalimbali za sehemu mbalimbali watu wakienda kuzika wapendwa wao huku wanacheza na kuweka nyimbo za kishujaa. Hii ni tofauti sana tuliozoea misiba kuwa na vilio.

Je maumivu yamepitiliza hadi wanaona wawape ushujaa wapendwa wao?

 
Kimsingi huo ni ujumbe wa moja kwa moja unaoelekezwa kwa serikali.

Ifahamike kuwa lengo la serikali lilikuwa ni kuongeza uwoga sambamba na kuupandikiza hofu

Hii hali ya watu kuwazika wapendwa wao kwa heshima sambamba na nyimbo zakishujaa ni pigo jingine kwa serikali.

Tuache kutiana moyo

Hali husika haiwapi amani watawala , na hata sasa wengi wao wapo kwenye majuto ya wazi kabisa hasa viongozi mmoja mmoja kuanzia madiwani hata wabunge maana wengi wanatokana na hizo jamii .

Usisahau kauli mbiu za wahanga ni moja tu KISASI NI LAZIMA.
 
Ushujaa na kuomboleza ni subjective, kila mtu ana mtazamo wake, hisia zake na percaption yake, so vitendo anavyofanya vinareflect hayo, unaruhusiwa kufikiria vyovyote unavoona sawa

Wakati wengine wanaona ni uhalifu wengine mashujaa, hata Mandela kwa makaburu, Nyerere kwa waingereza na kenyatta kwa wakoloni walikua ni wahalifu lakini ni mashujaa kwa maskini wenzao, so michango hapa itabase zaidi wapi mchangiaji anapatia mboga!
 
Hawa marehemu inabidi wapewe case ya uhaini kwa kutoroka kunyongwa
 
Wanakosea sana uhalifu uliofanywa na waandamaji haupaswi kuvikwa ushujaa!
Hivi mfano wewe ungepigwa risasi iliyotoboa paa la nyumba yako ukapelekwa hospital ukaorodheshwa kwenye list ya walioandamana kwa sababu tu ulitolewa risasi iliyokupiga kwenye mfupa wa paja na risasi imekupiga ukiwa nyumbani kwako, hapo wewe ukiitwa gaidi au mhalifu unataka kusemaje?
 
Serikali sasa inapambana na wananchi. Sijui kama watawashinda.

Watu wa juu wangejiuzulu tu kutuliza hali
 
Itakuwa umeona video mbalimbali za sehemu mbalimbali watu wakienda kuzika wapendwa wao huku wanacheza na kuweka nyimbo za kishujaa. Hii ni tofauti sana tuliozoea misiba kuwa na vilio.

Je maumivu yamepitiliza hadi wanaona wawape ushujaa wapendwa wao?

View attachment 3499255
Hii serikali imetibua kabisa utulivu wa Tanganyika.

Hawa wanaimba na kucheza kwa jazba, kukitokea maandamano mengine au hata sintofahamu yoyote kati ya watawala na jamii, hali itakuwa mbaya sana.
 
Kimsingi huo ni ujumbe wa moja kwa moja unaoelekezwa kwa serikali.

Ifahamike kuwa lengo la serikali lilikuwa ni kuongeza uwoga sambamba na kuupandikiza hofu

Hii hali ya watu kuwazika wapendwa wao kwa heshima sambamba na nyimbo zakishujaa ni pigo jingine kwa serikali.

Tuache kutiana moyo

Hali husika haiwapi amani watawala , na hata sasa wengi wao wapo kwenye majuto ya wazi kabisa hasa viongozi mmoja mmoja kuanzia madiwani hata wabunge maana wengi wanatokana na hizo jamii .

Usisahau kauli mbiu za wahanga ni moja tu KISASI NI LAZIMA.
Ndio maana sijaona hata mbunge mmoja akipongeza ushindi wa Rais. Majuto na kuhisi hatia ni mengi sana.

Huyu Mama mwenyew anajifanya chuma, lakin nina uhakika anajutia.

Ngoja tuone kama kufikia pasaka atakuwa sawa.
 
Wanakosea sana uhalifu uliofanywa na waandamaji haupaswi kuvikwa ushujaa!
Unachanganya waliofanya uhalifu na waandamanaji. Si wote walifanya uhalifu

Lakin kuna wale askari waliwafuata nyumbani na kuwafyatulia risasi

Na wapendwa wao wana haki ya kuwazila kwa style yoyote wanayotaka, huwez kuwazuia na kuwapangia
 
Back
Top Bottom