Wanaozuia mtandao mpaka sasa wamepata faida gani?

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
688
Reaction score
1,039
Tangu mwaka jana jukwaa hili lilizuiwa kwa muda wa siku 90 na TCRA.

Tulipitia wakati mgumu sana kwa sababu hili jukwaa lina manufaa mengi sana hasa kwa ustawi wa taifa letu.

Ni kupitia jukwaa hili ambapo wananchi huwasilisha kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Ni kupitia jukwaa hili ambapo serikali huweza kuona kero, changamoto na hata viashiria vya ubadhirifu wa mali za umma na kuchukua hatua ya haraka ili kuboresha maisha ya watu wanaowaongoza.

Hata hivyo hali ni tofauti sana kwani baada ya siku 90 kuisha bado jukwaa hili halikufunguliwa. Kila mara ukijaribu kuingia haiwezekani mpaka utumie njia mbadala kama VPN.

Najiuliza je adhabu iliongezwa? Kama siyo, kwa nini jukwaa hili halipatikani kama kawaida?

Kila jambo linalofanyika au maamuzi yoyote yakifanywa ni lazima kufanyike pia tathmini yake ili kuangalia matokeo yake chanya na/au hasi.

Je hao walioufungia jukwaa hili kwa muda wote huo mpaka sasa wakifanya tathmini wamepata faida gani hasa?

Kwa nini serikali inayodai kuchaguliwa na watu na kupenda watu wake wawe na furaha iendelee kufunga mitandao au majukwaa ambayo wananchi hupaza sauti zao?

Je serikali ipo kwa ajili ya nani? Si kwa ajili ya watu na ustawi wao? Kama ndiyo, kwa nini serikali haitaki kusikia sauti za watu wake?

Nafikiri ni wakati sahihi sasa wa serikali kukaa na kufanya tathmini ya maamuzi ya kuendelea kuzuia mitandao au majukwaa kama hili.

Naamini hakuna faida yoyote yenye manufaa kwa taifa iliyopatikana kutokana mwenendo huu, zaidi naona hata serikali inajipotezea mapato na imani kwa watu wake.
 
Nahisi hao wanaouzuia hili jukwaa washasahau kama walilizuia.

Tungeandama ili kuwakumbusha walifungulie.

Tunateseka sana
 
Nasikia pia kuwa ni serikali ya binti kiziwi.

Hawasikii lolote kutoka kwetu
 
Yaani nawazaga bora hata mkoloni arudi atutawale tena labda tutapata cha kujifunza waafrica! Imagine mtu yuko madarakani anajua ni binadamu na watu wake wa chini pia ni binadamu wana mapungufu yao, kwanini asikosolewe na wale anaowaongoza ili warekebishe? Wanafunga mitandao ili tu wananchi wasiseme, mbona Trump ye ule pale wanamjadili mpaka anavalishwa skuna lakini hafungi mitandao? Watu wenyewe bado ombaomba hakuna kitu walichonacho lakini akiingia madarakani anajifanya Mungu mtu. Ila Mungu fundi nyie ngojeni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…