Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Huwa najaribu kujiuliza, hawa wenzetu wameumbwaje? Sijawahi kupata jibu. Akili zao zinafanya kazi vipi, huwezi kuelewa.
Mkataba wa DP WORLD ni mbovu, na unatunyonga sisi wenyewe. Tunapiga kelele vifungu vibovu virekebishwe, lakini CCM wamekuwa wakitumia kodi zetu kuzunguka nchi nzima wakisema huo mkataba hauna ubaya wowote uko sawa tu.
Presha sasa imekuwa kubwa, mabaya ya mkataba wa DP WORLD yanawekwa bayana hadi vilabuni huko vijijini ndani ndani kabisa.
Naamini muda si mrefu, huenda mama akasalimu amri na kuachana na DP WORLD.
Mtashangaa hawahawa ambao wamezunguka nchi nzima wakiusifia mkataba wa DP WORLD kuwa ni mzuri na hauna kasoro, ndio hao hao watakaozunguka tena nchi nzima wakimsifia mama kwamba anaupiga mwingi, mkataba ulikuwa haufai.
Yangu macho, yajayo yanafurahisha