Wanaozunguka nchi nzima kushawishi umma ukubaliane na mkataba mbovu wa DP World ndio hao hao watakaosema mama anaupiga mwingi tukiachana nao

Wanaozunguka nchi nzima kushawishi umma ukubaliane na mkataba mbovu wa DP World ndio hao hao watakaosema mama anaupiga mwingi tukiachana nao

Mmechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Watu ndiyo kwanza wanaendelea na reforms za mashirika yote ya umma.

Unalijuwa hilo?
Karamu hiyo kama Mtume wenu angekuwepo, angeifananisha na nyama ya nguruwe mana iliandaliwa kwa kificho. Mbaya zaidi ikaletwa kwa kuvizia dakika za nyongeza.
 
Kwanini Watanganyika ni marufuku kumiliki ardhi Zanzibar ila wazungu wanaruhusiwa?
Hakuna Tanzania hii yeyote anaeruhusiwa kumiliki ardhi popote. Siyo bara siyo visiwani. Hakuna anaemiliki ardhi zaidi ya serikali, na mamlaka yote ya ardhi anayo Rais pekee.

Hata wewe Tanzania bara humiliki ardhi, usijidanganye, wewe unapewa utumie tu, kwa miaka 33 au 66 au 99. Na mwenye ardhi akiitaka wakati wowote huwezi kupinga wala kuzuwia asiichukuwe.

Kaisome hati yako ya ardhi kama unayo. Kama hauna ipo mtandaoni.

Msitake kujaza watu ujinga mlio nao. Mkadanganyane hukohuko machungani kwenu. Msifikiri wote ni makondoo.
 
Sijawahi kiusikia ndoa ya mwanamme na mwanamme Afrika hii. Huu muungano ulikuwa baina ya watu wawili, nyerere na karume.

Nani mwengine alishauriwa? Unataka kusema posa alipelekewa karume, akaolewa?

Matusi hayo.
Haya sasa
 
Huwa najaribu kujiuliza, hawa wenzetu wameumbwaje? Sijawahi kupata jibu. Akili zao zinafanya kazi vipi, huwezi kuelewa.

Mkataba wa DP WORLD ni mbovu, na unatunyonga sisi wenyewe. Tunapiga kelele vifungu vibovu virekebishwe, lakini CCM wamekuwa wakitumia kodi zetu kuzunguka nchi nzima wakisema huo mkataba hauna ubaya wowote uko sawa tu.

Presha sasa imekuwa kubwa, mabaya ya mkataba wa DP WORLD yanawekwa bayana hadi vilabuni huko vijijini ndani ndani kabisa.

Naamini muda si mrefu, huenda mama akasalimu amri na kuachana na DP WORLD.

Mtashangaa hawahawa ambao wamezunguka nchi nzima wakiusifia mkataba wa DP WORLD kuwa ni mzuri na hauna kasoro, ndio hao hao watakaozunguka tena nchi nzima wakimsifia mama kwamba anaupiga mwingi, mkataba ulikuwa haufai.

Yangu macho, yajayo yanafurahisha
Ukitaka kugundua kuwa wabunge wa ccm haziwatshi , kipindi cha mwenda zake walisifia kweli kuwa huyu ndo rais hijwahi kutokea, amefariki wakarudi kwa mam tena ameirudisha nchi vizur
 
Huwa najaribu kujiuliza, hawa wenzetu wameumbwaje? Sijawahi kupata jibu. Akili zao zinafanya kazi vipi, huwezi kuelewa.

Mkataba wa DP WORLD ni mbovu, na unatunyonga sisi wenyewe. Tunapiga kelele vifungu vibovu virekebishwe, lakini CCM wamekuwa wakitumia kodi zetu kuzunguka nchi nzima wakisema huo mkataba hauna ubaya wowote uko sawa tu.

Presha sasa imekuwa kubwa, mabaya ya mkataba wa DP WORLD yanawekwa bayana hadi vilabuni huko vijijini ndani ndani kabisa.

Naamini muda si mrefu, huenda mama akasalimu amri na kuachana na DP WORLD.

Mtashangaa hawahawa ambao wamezunguka nchi nzima wakiusifia mkataba wa DP WORLD kuwa ni mzuri na hauna kasoro, ndio hao hao watakaozunguka tena nchi nzima wakimsifia mama kwamba anaupiga mwingi, mkataba ulikuwa haufai.

Yangu macho, yajayo yanafurahisha
Ndo hao hao watakasema MAMA MSIKIVU..!!
 
Back
Top Bottom