Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikiongoza dunia kama taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, nchi kama China na Urusi zimekuwa zikiongeza ushawishi wao na kupinga baadhi ya sera za Marekani.
Swali, Je, wanachotafuta ni dunia yenye usawa ambapo hakuna taifa moja linatawala kila kitu, au wana lengo la kuwa nguvu kuu kuliko Marekani?
Ukweli ni kwamba ushindani huu hauhusu nguvu za kijeshi pekee, bali pia unahusu uchumi, teknolojia, biashara, rasilimali na ushawishi wa kisiasa duniani.
Dunia inabadilika kutoka mfumo wa nguvu moja kuelekea ushindani wa mataifa makubwa, ambapo kila taifa linatafuta kulinda maslahi yake na kuongeza nafasi yake kwenye jukwaa la kimataifa.
Kutokana na hali hii huenda kukazuka shida ile ile baadae ikiwa marekani itaanguka kutokavnafasi yake ya sasa.
Mfano China au Urusi ikiwa ndo top bado kutaibuka tena mataifa yanayopinga.
Wewe unasemaje?