Wanaposema Kula Bata wanamaanisha nini?

Wanaposema Kula Bata wanamaanisha nini?

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,496
Inawezekana sielewi wanaposema kula bata wanakuwa wanamaanisha nini haswa.

Je, ni kukutana na marafiki na kupiga soga? Kunywa pombe? Kula nyama choma? Kuogelea ufukweni au bwawa maalumu? Kutembelea vivutio? Kulala? Kuangalia michezo? Mitoko ya kifamilia?

Je, mimi ninayelala badala ya kutoka kama wengine nahesabika kama nakula bata? Au nikiwa 'outing' nikaishia kunywa soda na kupiga soga na washikaji nahesabika kama nakula bata?

Je, kuna 'standards' na 'criteria' za kusema mtu fulani anakula kula bata au la?

Hebu tusemezane, ukisikia mtu anakula bata unaelewa nini? Au unaposema unakula bata huwa unafanya nini?

Hii dhana inanichanganya kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea. Km n mpenzi wako hapo huli bata ila km n MTU wa kubadilisha totoz ,hapo tunamuhesabia anakula bata na totoz

From profile picture to proper future
Kwanini kwa totoz wengine ionekane bata,kwa mpenzi/mchumba/mke/mume ionekane kawaida..

Why??
 
Una umri gani?kula bata maana yake ni kufanya starehe...starehe yoyote utakayoifurahia uilipie au kutoilipia ili mradi umestarehw iite bata

Japo vijana wa mjini kula bata inamaana ya kutumia fedha kwenye pombe, mziki, ngono, kamari na mengineyo bila kuwa na feeling ya kujutia...we only live once
 
Inawezekana sielewi wanaposema kula bata wanakuwa wanamaanisha nini haswa.

Je, ni kukutana na marafiki na kupiga soga? Kunywa pombe? Kula nyama choma? Kuogelea ufukweni au bwawa maalumu? Kutembelea vivutio? Kulala? Kuangalia michezo? Mitoko ya kifamilia?

Je, mimi ninayelala badala ya kutoka kama wengine nahesabika kama nakula bata? Au nikiwa 'outing' nikaishia kunywa soda na kupiga soga na washikaji nahesabika kama nakula bata?

Je, kuna 'standards' na 'criteria' za kusema mtu fulani anakula kula bata au la?

Hebu tusemezane, ukisikia mtu anakula bata unaelewa nini? Au unaposema unakula bata huwa unafanya nini?

Hii dhana inanichanganya kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanamaanishs " butter" ana siagi kwa kiswahili. Kula raha. # Mkate na siagi # Nchi ya ahadi waliahidiwa watakuwa wanakula mkate siagi maziwa na asali
 
Back
Top Bottom