Wanaposema uchumi wa kati huwa wanamaanisha nini?

mchuziwapweza

Senior Member
Joined
Aug 19, 2018
Posts
107
Reaction score
149
Leo naomba mnitoe ushamba kidogo, jamani hivi wanaposema uchumi wa kati hua wanamaanisha nini? Kwani kuna level ngapi za uchumi?
 
Tuanzie kipengele cha pili (kwani kuna level ngapi?)

Wachumi(Benkk ya dunia) imezigawanya chumi za nchi katika makundi matatu.

Nchi za kipato cha juu (nitaziita NKJ), Nchi za kipato cha kati(nitaziita NKK) na Nchi za kipato cha chini (nitaziita NKC). Vigezo mbalimbali vinatumika kuashiria chumi hizi; elimu, huduma za afya, vizazi na vifo. Kikubwa zaidi ni wastani wa kipato cha kila raia wa nchi husika kwa mwaka (GNI per capita). Hiki hupatikana kwa jumla ya mapato ya ndani ya nchi kwa mwaka gawanya kwa idadi ya wananchi wake.


NKJ

Nchi hizi huwa zina wastani wa kipato cha kila mwananchi cha dola za kimarekani 12,056 kwa mwaka. Hizi ni sawa na sh 28,000,000 (kwa dola 1=2284/=). Sasa na takribani sh 2,290,000 kwa mwezi. Kiasi hiki kwa huku kwetu ni mshahara wa mtu kama mkurugenzi wa halmashauri. Nchi zenye uchumi huu zipo takribani 80. Nchi nyingi za ulaya zipo kundi hili.


NKK

Nchi hizi zipo katika makundi mawili. Nchi za kipato cha kati juu (NKK-J) na Nchi za kipato cha kati chini (NKK-C)

NKK-J

Nchi hizi zina wastani wa pato la mwananchi la mwaka la $4,036(sawa na sh 9,000,000 ) hadi 12,056(sawa na sh 27,000,000) kwa mwaka. Au wastani wa juu ya sh 750,000 hadi 2,000,000 kwa mwezi. Nchi kama urusi, china , afrika kusini, brazil(BRICS), Jamaica, n.k zipo kundi hili


NKK-C


Hizi ni za uchumi wenye wastani wa kipato cha wananchi kwa mwaka cha dola 1,024 hadi 4,035. Takribani ya 2,000,000 hadi 9,000,000 sh . sawa na wastani wa kila raia kuingiza kiasi cha sh 190,000 hadi 750,000 kwa mwezi. Nchi kama kenya zipo daraja hili.


NKC


Hizi ndio masikinj zaidi. Zina pato la chini ya dola 1,024. Kwa fedha yetu ziko chini ya pato la wastani wa sh 190,000 kwa mwezi. Nchi nyingi za afrika ziko hapa, mali, tz, uganda, zimbabwe.
 
Barikiwa
 
Nimekuelewa
 
Well and clear explanation [emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…