Wanariadha wa 4 kutuwakilisha kwenye mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa Mwezi Julai, Kambi kuwekwa Arusha

Wanariadha wa 4 kutuwakilisha kwenye mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa Mwezi Julai, Kambi kuwekwa Arusha

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
DA8CA999-3BF4-43E6-BECE-B8E03B038C0B.jpeg

BAADA ukimya wa muda mrefu kuhusu lini timu ya Taifa ya Riadha itaingia kambini kuanza maandalizi ya mashindano ya Olimpiki ambazo zitafanyika mwezi Julai huko Paris Ufaransa hatimae Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),imefunguka kuwa kambi hiyo itaanza mapema wiki hii.

Tanzania itawakilishwa na wanaridha wanne pekee ambao wanakimbia mbio ndefu kilometa 42 ,Alphonce Simbu,Gabriel Geay,Magdalena Shauri na Jackilne Sakilu.

Simbu alifuzu kupitia Shangai Marathon za China akitumia muda wa 2:05:39,huku Jackline Sakilu nae akifuzu kupitia mbio hizo kwa muda wa 2:26:50,mbio zilifanyika Novemba 26,2023.

Magdalena yeye alipenya kupitia Berlin Marathon zilizofanyika Septemba 24,2023 nchini Ujerumani akitumia 2:18:41 huku Geay akitokea Valencia Marathon ambazo zilitimua vumbi Disemba 2,2023 Hispania kwa 2:04:33.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),Jackson Ndaweka alisema kambi hiyo ambayo itaanza mapema wiki hii katika Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine tawi la Arusha ambayo lipo Olmotonyi Ngaramtoni itakuwa chini ya makocha wawili.

Makocha hao ni Michael Washa wa jeshi la Magereza na Antony Mwingereza kutoka jeshi la wananchi (JWTZ),ambaye wanariadha wake watatu wamefuzu kushiriki Olimpiki,Simbu,Jackline na Magdalena.

“Tumechelewa kuingia kambini Kwa sababu wanaridha wetu walikuwa na mashindano mbalimbali ya Kimataifa hivyo isingekuwa vyema baadhi kuanza huku wengine hawapo"

"Wachezaji wetu wote wapo kwenye hali nzuri ya kimashindano kwani wana viwango bora na wana uwezo wa kucheza chini ya muda ambayo itawafanya kurudi na medali”,alisema Ndaweka.

Aliongeza licha ya kwamba Olimpiki za mwaka huu zitakuwa na ushindani mkubwa sana kwani wanariadha wengi wenye ubora kwa sasa watashiriki.

Lakini pia kutolewa zawadi za fedha kwa mara ya kwanza kwa washindi ambao watapata medali kwa upande wa Riadha ila wana matumaini makubwa na viijana wao katika kwenda kupambania medali zingine baada ya kupita miaka 44.

“Tunafanya kila kitu ili kambi iwe bora kuanzia kwenye morali na motisha pia kamati ya Olimpiki Tanzania itakuja kutuongezea nguvu”,alisema.

Tangu Tanzania ilipopata medali mbili za shaba katika mashindano hayo kwenye mbio za mita 5000 na 3000.Olimpiki za Moscow Urusi mwaka 1980.

Moja ilitwaliwa na mwanariadha Suleiman Nyambui aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za Mita 5000 na nyingine ikichukuliwa na Filbert Bayi katika mbio za Mita 3000.

Mashindano ya Olimpiki yatafanyika kuanzia tarehe 26 Julai hadi 11 Agosti 2024 huko Paris, Ufaransa.
 
Wamefuzu kwa nguvu na juhudi zao.
Basi ngoja uje usome list ya maafisa watakaowasindikiza kutoka BMT, Wizara ya Utamaduni, Chama cha Riadha, Kamati ya Olimpiki, ... nk. Utakuta msafara una maafisa 26 huku wanariadha wenyewe wanne tu.
 
Basi ngoja uje usome list ya maafisa watakaowasindikiza kutoka BMT, Wizara ya Utamaduni, Chama cha Riadha, Kamati ya Olimpiki, ... nk. Utakuta msafara una maafisa 26 huku wanariadha wenyewe wanne tu.
kama vile uliota
 
Back
Top Bottom