Hili jambo ni kweli tupu.
Siyo pesa nyingi unazokusanya kidogo kidogo, ni zile fedha za mkupuo kupata mamillioni ama mabillioni ghafla bin vuu, ndozinachanganya akili kinyama!
Pesa zitokanazo na kubahatisha madini ama mafao, wizi nk nk.
Hilo jambo mie liliwahi kunitokea zamani, baada ya kujaza begi la hela, nyekundu tupu bila hata kujua idadi ya hesabu yake.
Nilishindwa kula muda wa siku3 sipati njaa kabisa hadi nilipododoswa na washikaji zangu kwanini hawajaniona kula tangia juzi, je naumwa?
Ndipo nikakumbuka kweli sijala siku3 na bado sisikii njaa, nadhani bila kushituliwa ningedanja kwa njaa bila kujijua wala kuhisi!
Ikabidi nianze kujilazimisha kula biskuti na vimiminika huku natembea, eti naona kukaa na kuanza kula ni kupoteza muda, zilinichanganya!
Nikajaa hofu nikawa simuamini kila mtu, nikihisi kila nayekutana naye tayari kagundua kama nina hela, presha ikawa juu!
Ikawa silitui begi langu kutoka mgongoni, usiku nalala nalo, nadhani nilitaka kuchanganyikiwa!
Ninachojiuliza mpaka leo, ni kitu gani kilichoua njaa kwa siku tatu hadi nilipokumbushwa kula?
Hali hiyo nilidhani ilinitokea mimi tu, kumbe ni tatizo la "umma", ngoja nisikilize wazoefu!