Wanasayansi: Sio kweli kwamba minara ya simu inasababisha kansa kwa binadamu

Wanasayansi: Sio kweli kwamba minara ya simu inasababisha kansa kwa binadamu

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Baadhi ya watu wamekuwa wakijenga hoja kuwa kuishi, kutembea au kusoma karibu na minara ya simu kunawaweka watu katika hatari ya kupata kansa au matatizo mengine ya afya.

Lakini mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja juu ya hoja hiyo. Katika nadharia za afya kuna sababu chache ambazo zinakubaliana na dhana ya minara ya simu kusababisha kansa. Chama cha Kansa cha Amerika (ACS) kimeeleza sababu mbalimbali za kwanini minara ya simu sio tishio kwa afya ya binadamu:

Kwanza, Nguvu ya mawimbi ya radio yanayotumiwa na minara ya simu ni ndogo ukilinganisha na mionzi mingine kama ya jua (ultraviolet light), Eksirei (x-rays) na nyuklia (gamma rays) ambayo inaongeza hatari ya kupata kansa. Mionzi ya mawimbi ya radio inayotolewa na minara ya simu haina nguvu ya kutosha kuvunja kemikali zilizoungana za vinasaba (DNA) vilivyopo mwilini.

Suala lingine ni urefu wa mawimbi. Mawimbi ya radio yana urefu ambao unaweza kujikusanya kwa inchi 1 au 2 na sio zaidi ya hapo. Hii ina maana kuwa mionzi ya mawimbi ya radio haiwezi kujikusanya kwa ukamilifu kuhatarisha seli za mwili.

Hata kama mawimbi ya radio kwa sehemu yangekuwa yanaathiri seli za mwili yasingefanikiwa kwasababu kiwango cha mawimbi hayo kinachopatikana ardhini wanakoishi watu ni kidogo sana kuliko kile kinachopendekezwa na watalaamu wa mawasiliano.


Zaidi, soma hapa => Ukweli kuhusu minara ya simu kusababisha kansa kwa binadamu | FikraPevu
 
Back
Top Bottom