Hiyo habari nilisoma mchana hao wanasayansi hawajafungwa kisa walichotengeneza, tena nilidhani labda wametoa siri. Kumbe wamefungwa sababu wakishiriki makongamano ya kimataifa ya hypersonic missile technology, vile vitu vya kufanya presentation na maprofesa wenzako wa Japan au Korea. Pia wamechapisha maandiko kama ambavyo wanasayansi wa afya na siasa wanachapisha. Mwishowe wamejikuta wanakamatwa tena kimyakimya na kesi zao zinafichwa mbele ya public.
Taasisi yao inalalamika mazingira waliyokamatwa hayaridhishi, kipimo cha kusema wametoa siri hakiwezi tolewa na watu wa usalama ambao yawezekana hawajui hypersonic ni nini, kipi ni siri ya kitaifa na kipi kinajulikana.
Hayo matatizo kwa wanasayansi wa Urusi ni kawaida enzi na enzi, mfano Pavel Dulov alivyotengeneza Vkontakte, Facebook ya Urusi serikali ililazimisha inunue shares kubwa iathiri maamuzi ya platform kama access ya database. Dulov akajiondoa akaanzisha Telegram nako wakamzingua akakimbia nchi.