Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Wanasayansi wa mazingira wa kimataifa wameitaka Mamlaka ya Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA) kuhamisha ujenzi wa hoteli ya kifahari ya nyota tano kutoka Hifadhi ya Msitu wa Ngezi, Pemba, wakionya kwamba mradi huo unahatarisha mimea na wanyama adimu waliopo eneo hilo.
Katika barua ya wazi iliyochapishwa kwenye Science mnamo Septemba 26, 2025, watafiti 14 wakiongozwa na Profesa Tim Caro kutoka Chuo Kikuu cha Bristol walitoa wito mradi wa Mantuli Luxury Estate wenye thamani ya dola milioni 8 (zaidi ya Shilingi bilioni 17.3) uhamishiwe eneo jingine lisilohatarisha mfumo wa ikolojia ulio hatarini.
Watafiti, akiwemo Giacomo Baldesi kutoka Chuo Kikuu cha Pavia, Grazia Borrini-Feyerabend wa ICCA Consortium nchini Uswisi, na Matthew Clark wa Chuo cha Imperial London, wameonya kuwa waendelezaji wa mradi huo hawajakamilisha Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii (Environmental and Social Impact Assessment) kama inavyotakiwa.
Walisema kuwa mradi huo unahatarisha kutoweka kwa spishi kadhaa za mimea za pekee zinazopatikana eneo hilo pekee, kama vile Bulbophyllum, Disperis na Oeceoclades orchids, pamoja na spishi za Sansevieria. Pia waliitaja hatari kwa wanyama kama popo wa Pemba (Pemba flying fox), bundi wa Pemba (Pemba scops owl) na njiwa wa Pemba (Pemba pigeon). Aidha, walionyesha wasiwasi kuhusu hatari inayolikabili Panzi wa Pemba (Pemba featherleg damselfly), anayepatikana tu katika eneo la Ngezi.
Timu hiyo ilimshauri Zipa kuhamishia mradi huo nje ya hifadhi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 14.4, ambayo ina miti yenye umri wa zaidi ya miaka 200.
“Upekee wa hoteli hiyo ya kifahari utazuia wananchi kufikia ufukwe unaotumiwa na wanafunzi na wavuvi wa eneo hilo,” waliongeza.