Wanasema Hayati Magufuli Alikuwa Anakubalika sana: Kwanini basi aliiba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020?

Tatizo la wabongo wengi story za vijiweni ndio wanatuletea tuzijadili.Hii ni tatizo kubwa Sana.
Na hata vijana wa sasa wengi wanaamini mitandaoni kuliko hata wanachofundishwa Madarasani.
 
unataka tuweke zile video za wizi wa kura ambao hata maaskari waliiba?
Ni kwanini walizima mitandao ya kijamii waliogopa nini
 
Hivi unadhani unaongea na watoto ama? Huenda mnafikiri tumesahau ukweli wa wizi ule. Taarifa za wizi ule na mabox ya kura fake yalikamatwa na kupelekwa polisi, na polisi walikaa kimya. Kibaya zaidi polisi walikuwa sehemu ya ulinzi wa kura zile za wizi ili zifike vituoni! Ushahidi wa haya upo wazi, lakini unaenda kushitaki wapi ambapo hapakuwa sehemu ya utawala wa kihayawani wa Magufuli?

Hakuna uchaguzi uliopata kuwa na uvunjifu wa sheria kama ule. Ule haukuwa uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Mpumbaff weye!Gunioooo!
 
CHADEMA mkishindwa uchaguzi mnakimbilia neno KUIBIWA KURA ila mkishinda wala hakuna neno na huisikii CCM ikilalamika kuwa mmeiba kura.

Hata mahakamani hali ni hiyohiyo; miinshindwa kesi mnasema mahakama haiko huru ila mkishinda kesi mnasema mahakama iko huru.

kuna wakati mnatakiwa kubadilika na kuachana na siasa zilizopitwa na wakati za kutegemea huruma ya wananchi. Wananchi wa sasa hawatoi kura kwa huruma kama ambavyo mlitegemea Tundu Lissu angepata kura za huruma za kushambuliwa na risasi halafu mwisho wa siku kura zote akapigiwa Magufuli kwa sababu wananchi waliona ni nafuu kuipigia kura CCM yenye sera
 
Alipoiba we kama uliyeibiwa ulichukua hatua gani? Au ulitulia tu kana NDEZI?
 
*Vyeti feki.

*Watumbuliwa kazi kwa ufisadi.

*Wazibiwa mianya ya upigaji madili.

*Wauzaji wa madawa ya kulevya.

*Wasafirisha magendo.

*Wakwepa malipo ya kodi

*Wasiompenda JPM bila sababu ya msingi.

Unadhani hao wote, wataacha kutafuta visababu uchwara kuja kumchafua mwamba JPM kuhusu legacy yake [emoji848][emoji28]

Wahuni wasiozidi watu 300, wanaolipwa kila siku posho kwa sababu ya kuchafua legacy na kukubalika kwa Hayati JPM kwa wa-TZ hapa online kusikutishe, wa-TZ si wajinga kuamini huo upumbavu [emoji2]
 
Kila mtu anajua magufuri aliiba kura,labda ulikuwa mmojawapo wa waliomsaidia kuiba kura
 
Aliiba kura hilo lipo wazi , kwani wasimamizi hawajui?
 
Mungu akuongezee umri mrefu mkuu Wangu.
 
unataka tuweke zile video za wizi wa kura ambao hata maaskari waliiba?
Ni kwanini walizima mitandao ya kijamii waliogopa nini
Nimeuliza swali moja!

Ilikuwaje Chadema wadai kukamata begi la kura feki na muda mfupi baadae,hao hao wanachoma kidhibiti moto.

Halafu ndio muendelee kujifariji huko vijiweni.
 
majibu yenu ya kitoto sana
Ulivyoyaona ndo kitoto, we kama mtu mzima umemuona mwizi anakuibia, unachukua hatua gani? Napima ukomavu wako wa kupambana na wezi wa hadharani uliowaona wakikupora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…