Wanasema kwa kejeli ati najitia kuijua historia ya Uhuru wa Tanganyika

Heshima yako . Ni upi mchango wa John Okello kwenye mapinduzi ya Zanzibar
 
Nilimskia na kumuona bibi Fatma Karume akusema ,siku kabla ya mapinduzi,Karume alichukuliwa usiku akenda kufichwa Dar Es Salaam.Hivyo hadi mapinduzi yanatokea Karume hakuwa Visiwani.Ukweli wa mapinduzi kuongozwa na Okelo liko wazi maana hata serikali ya kwanza ya mapinduzi ya Zanzibar ilitangazwa na Okelo.
 
Heshima yako . Ni upi mchango wa John Okello kwenye mapinduzi ya Zanzibar
Laki...
Swali lako halijakaa vyema kuniuliza mimi swali hilo.

Dr. Harith Ghassany katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," kamueleza vizuri sana John Okello.

Kitabu kipo mtandaoni kinapatikana bure.
Lakini nikuongezee kitu.

Mchango mkubwa katika mapinduzi siku ziliponyanyuliwa silaha uko kwa Wamakonde kutoka Kipumbwi, Tanga.

Hawa waliua Wazanzibari wengi kiasi cha kusabaisha hofu isiyo na mfano.

Ghassany ndiye mwandishi wa kwanza kawaleta hawa Wamakonde katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Hawakuwako kabla katika kitabu chochote.
Usihangaishwe na Okello.

Soma historia ya yaliyopitika Kipumbwi, Tanga katika matayarisho ya mapinduzi.
 
Shida ya huyu jamaa ametanguliza udini hapo ndiyo anaonekana hana la maana.
Joh...
Udini ingekuwa nafundisha Uislam kutafuta wafuasi.
Hapa mimi nasomesha historia ya uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ilifutwa ikawa haipo.

Mimi nimeandika kitabu cha Abdul Sykes na ni kitabu maarufu sana kipo sasa mwaka wa 25 na kimechapwa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.

Kitabu kimependwa sana.

Historia hii imesababisha Mohamed Said kutunukiwa na JF Mwandishi Bora Jukwaa la Historia mara mbili mfululizo 2021 na 2022.

Sijaaliwa kuwa mtu asiye na maana.
Alhamdulilah.


 
Mama...
Historia ya Nyerere imeandikwa miaka mingi: Duggan, W R and Civille, J,R Tanzania and Nyerere, Orbis Book, Maryknoll New York, 1976.

Ikaja kuandikwa tena na Prof. Issa Shivji, Prof. Saida-Yahya Othman na Dr. Ngwanza Kamata, ''Nyerere Biography,'' Mkuki na Nyota, 2020.

Soma vitabu hivyo uone wameandika kitu gani.
Umepata kuvisikia vitabu hivi vikizungumzwa hapa?

Bila shaka vitabu hivi vimemwandika Nyerere kwa haki anayostahili kuandikwa.

Mbona kuna ukimya?
 
Nikuulize Mzee, Hayati Julius Kambarage Nyerere ilikuwaje hadi akawa Rais baada ya Uhuru? Yaani Waislamu walikuwa wengi na wenye nguvu za Kiuchumi na Ushawishi sasa huyu Nyerere Mtu kutokea Bara akawaje tena RAIS?!
 
Nikuulize Mzee, Hayati Julius Kambarage Nyerere ilikuwaje hadi akawa Rais baada ya Uhuru? Yaani Waislamu walikuwa wengi na wenye nguvu za Kiuchumi na Ushawishi sasa huyu Nyerere Mtu kutokea Bara akawaje tena RAIS?!
Uzalendo...
Hili ni jibu la swali kama lako nililoulizwa na hapo chini ni jibu langu.

Nimehariri kidogo ili jibu likae vizuri:

"Katika mkutano uliofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda kumtaka ushauri kuhusu kumwingiza Nyerere kwenye uongozi wa juu wa TAA Hamza alishauri kuwa Nyerere achaguliwe kuwa rais na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Huu ni mwaka wa 1953 kati ya mwezi January na March.

Historia hii nimeieleza mara nyingi hapa JF naamini wengi wanaijua.

Nafasi ile ilitakiwa ishikwe na Mkristo ili upatikane umoja wa wananchi wote.

Harakati za siasa zilitawaliwa na Waislam na hofu ilikuwa ikiwa TANU itaundwa na kiongozi ni Muislam sura iliyokuwa imejengeka itadhihirisha kuwa harakati zile ni za Waislam.

Waingereza watatia fitna kuwashawishi Wakristo na wao wawe na chama cha siasa kulinda maslahi yao katika Tanganyika huru.

TANU walijifunza lililowafika Mohamed Ali Jinnah na Nehru kudai uhuru wa India vyama vyao vikuu viwili vikiwa vimejishikiza kwenye dini zao - Uislam na Uhindu.

Leo usiku wanapewa uhuru.

Asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinalipuka.

TANU ilitaka kujiepusha na balaa hili.

Nia ikiwa kuingia katika kudai uhuru chini ya chama kimoja.

Viongozi wa TAA hawakutaka Tanganyika iingie katika kudai uhuru imegawanyika katika misingi ya dini.

Baada ya uchaguzi wa Arnautoglo baina ya Abdul Sykes na Nyerere 1953 na TANU kuundwa 1954 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Baraza la Wazee wa TANU chini ya uongozi wa Sheikh Suleiman Takadir wakafanya juhudi kubwa kujenga umoja wa wananchi chini ya Julius Nyerere.

Kuna historia ya kusisimua jinsi Bantu Group nayo kwa upande wake ilivyohamasisha wananchi kuwa wamoja kwa kufuta, "Salaam Aleikum Warahmatullah Wabarakatuh," kuwa mamkizi ya wanachama wa TANU.

Bantu Group akina Juma Selemani na Rashid Sisso wakaja na Salaam mpya, "Ahlan Tabu."

Hii Ahlan Tabu mimi niliiwahi na kuisikia kwa masikio yangu nikiwa na kama miaka mitano hivi.

Kibwagizo cha "Uhuru na Umoja" kilipokuja ndiyo Ahlan Tabu ikafa.

Yapo mengi na yote nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Sasa baada ya shutuma zile za Sheikh Suleiman Takadir dhidi ya Nyerere Waislam wote walimghadhibikia Sheikh Takadir wakamuona anasaliti msimamo uliowekwa na waasisi wenyewe wa TANU.

Hii ilikuwa 1958 na ilikuwa wazi kabisa kuwa uhuru unakaribia.

Hili ndilo tatizo kubwa lililokuwapo.

Bahati mbaya historia hii ya TANU ilifutwa na hii ndiyo sababu leo naulizwa nini lilikuwa tatizo kubwa kiasi Sheikh Suleiman Takadir apigwe pande hata na nduguze Waislam?

Umoja ule uliokuwapo 1958 kupinga chokochoko za ubaguzi ndiyo uliokuwapo hadi uhuru unapatikana 1961 na Nyerere hakuwa na mpinzani wa kumshinda.''

Picha hiyo hapo chini inasema maneno 1000.


 
Sehemu kubwa ya hayo unayoyaandika umehadithiwa.

Vipi walitia CHUMVI hao waliokupa hizo taarifa.

Bila shaka enzi hizo wakati wa harakati za uhuru ulikuwa mtoto Wala hukushuhudia yaliyofanyika.

So watu lazima wawe na mashaka.

Kila mwamba ngoma huvutia kwake
 
Mangungo...
Sehemu kubwa ya historia niliyoandika ni kutokana na Nyaraka za Sykes na mahojiano kutokana na niliyosoma.

Taarifa nyingine ni kutoka kwa waliokuwapo wakati wa kupigania uhuru.

Hakuna popote nilipohisi kuwa wapashaji wangu hawasemi kweli.

Ikiwa wewe nafsi yako ina shaka kuwa historia hii ni uongo huna sababu ya kujihangaisha.

Usiamini hata kama hawa niliowataja kwenye kitabu walikuwapo.
 
 

Attachments

Unawaponda akina Shivji! Kwani wewe kitabu chako kimechukua muda gani kujulikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…