KERO Wanasema tujiandae na El Niño lakini Matosa Uzaramuni – Goba tunateseka na Kalavati bovu

KERO Wanasema tujiandae na El Niño lakini Matosa Uzaramuni – Goba tunateseka na Kalavati bovu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-09-04 at 12.56.28.jpeg
WhatsApp Image 2026-09-04 at 12.56.30.jpeg
Uongozi wa Wilaya ya Ubungo umekuwa ukitoa tahadhari kwa wananchi kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Niño, lakini wakazi wa baadhi ya maeneo tunahoji hatua zinazochukuliwa kukabiliana na maeneo ambayo tayari yamekuwa na changamoto tangu mvua za El Niño za mwaka 2023.

Miongoni mwa maeneo hayo ni kalavati lililopo Barabara ya Kawawa Road, Goba–Matosa–Uzaramuni, ambalo halijawahi kutengenezwa wala kufanyiwa ukarabati licha ya kuharibika kwa muda mrefu. Hali hiyo imeacha mashimo na miundombinu ikiwa katika hali inayotia hofu, hasa wakati mvua zinaponyesha.

Kinachowashangaza zaidi ni kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi, viongozi mbalimbali walifika eneo hilo na kujionea hali halisi ya kalavati pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi. Wananchi wanasema viongozi hao walishinda uchaguzi, lakini tangu wakati huo hawajasikia hatua yoyote kuhusu ukarabati wa kalavati hilo.

TARURA inafahamu kuhusu tatizo hilo na imekuwa ikieleza kuwa inasubiri bajeti ya Serikali ili kufanya ukarabati. Hata hivyo tunajiuliza kwa nini tatizo hilo limeendelea kwa zaidi ya miaka minne bila kupata suluhisho, licha ya kuwa barabara hiyo iko chini ya TARURA.

Ikiwa kalavati hilo limekuwa na tatizo tangu mwaka 2023, na mpaka sasa halijarekebishwa, wananchi tutapita wapi wakati wa mvua zijazo?

Wakazi wa Matosa - Goba, Mwaka wa 3 tunabembeleza kujengewa kalavati, TARURA wanakuja kupiga picha wanaondoka


 
Back
Top Bottom