Wanasheria Badilikeni, Toeni majibu ya kisheria

Wanasheria Badilikeni, Toeni majibu ya kisheria

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2014
Posts
3,509
Reaction score
3,741
Ukifuatilia Post Za Watu Wengi Waliouliza Maswali Utakuta Hazina Majibu Kabisa Na Hata Zile Zenye Majibu Hazikujibiwa Kitaaluma Ya Kisheria,yaani Zimejibiwa Kama Na Mtu Tu Asiyesomea Sheria Kabisa!Mfano Unakuta Post Imejibiwa Lakini Mjibu Swali Ambae Tunategemea Ni Mwanasheria Hajibu Kwa Kutaja Na Kunukuu Vifungu Vya Sheria Vinavyohusiana Na Swali, Anajibu Kama Siyo Mwanasheria.

Sasa Hapo Utatofautishaje Jibu Hili Ni La Mwanasheria Na Hili Siyo La Mwanasheria Ikiwa Majibu Yote Hayana Nukuu Ya Vifungu Vya Sheria? Sasa Hapo Sisi Ambao Si Wanasheria Tutajuaje Hicho Kifungu Kinapatikana Wapi Ili Nasisi Tuvitumie Kujilinda Navyo?

Wanasheria Badilikeni Na Mjibu Maswali, fikiria Post Inakaa Wiki Nzima Haina Majibu? Tuseme Hakuna Wanasheria Kwenye Hili Jukwaa? Basi Bora Lisiwepo Kabisa.

Nawasilisha.
 
ukiona wanafanya blablaa ujue wanataka wasikulishe bure, wanataka ukwawaingeji uwape hela ndio wakupe kitu chenyewe. sheria ni biashara. wafuate kwenye ofisi zao uone kama watakupa majibu yasiyo na authority.
 
Ukifuatilia Post Za Watu Wengi Waliouliza Maswali Utakuta Hazina Majibu Kabisa Na Hata Zile Zenye Majibu Hazikujibiwa Kitaaluma Ya Kisheria,yaani Zimejibiwa Kama Na Mtu Tu Asiyesomea Sheria Kabisa!Mfano Unakuta Post Imejibiwa Lakini Mjibu Swali Ambae Tunategemea Ni Mwanasheria Hajibu Kwa Kutaja Na Kunukuu Vifungu Vya Sheria Vinavyohusiana Na Swali, Anajibu Kama Siyo Mwanasheria,sasa Hapo Utatofautishaje Jibu Hili Ni La Mwanasheria Na Hili Siyo La Mwanasheria Ikiwa Majibu Yote Hayana Nukuu Ya Vifungu Vya Sheria? Sasa Hapo Sisi Ambao Sy Wanasheria Tutajuaje Hicho Kifungu Kinapatikana Wapi Ili Nasisi Tuvitumie Kujilinda Navyo? Wanasheria Badilikeni Na Mjibu Maswali,fikiria Post Inakaa Wiki Nzima Haina Majibu?Tuseme Hakuna Wanasheria Kwenye Hili Jukwaa?Basi Bora Lisiwepo Kabisa, Nawasilisha.

Tabia ya wanasheria sawa na mafundi saa, gari, simu etc. Anarekebisha fault kwa kukuficha usione eti kesho hutarudi. Wanasheria kweli hawachangii jukwaa la sheria. Naunga mkono badilikeni jamani, acha uchoyo, kazi zipo mtapata! Shyster lawyers!
 
mimi mwenyewe nimeona sana hiyo kitu tunahitaji legal consultants wawe wnakuja hapa kutujibia maswali. kuna mmoja aliweka post yake anasema kama una swali lolole kihusu sheria ya ndoa uliza. nimejenga hoja yangu halafu nikaweka na swali kajibu vitu vya ajabu anasema umeshajijibu mimi nijibu nini? huyu ni mwanasheria ambaye tunamaanisha ni consultant ndo anajibu hivyo
 
pole sana kijana ila kumbuka sheria nayo ni biashara nayo imelipiwa ada.je unataka upewe kila kitu bure?. lakini umetoa dukuduku zuri na litakuwa limewafikia walengwa
 
Ndugu hujui hata kutoa ushauri wa kisheria inabidi ulipie. Sasa akikupa details zote in and out atakula wapi. Pia mtu asie mwanasheria anahitaji kujua tu vitu basic unaweza tajiwa vifungu bado ukaenda kusoma halafu usielewe.

Kwahiyo kama amekuelekeza jua hivyo ndio muhimu kwa wewe kujua akiingia deep anaweza kukuvuruga msielewane kabisa.
 
mfano,wewe unajibiwa na mwanasheria kuwa unahaki ya kuishi pasipo kifungu chochote kinachohusika, halafu anatokea mtu mwingine anaikiuka hy haki mfano polisi, mtu huyo akataka kukuchalenge hebu nitajie kifungu hicho unachodai nimekikiuka dhidi yako utamtajia nini?au utasema mi sijui ila nilimsikia wakili anasema tu kuwa ninahaki ya kuishi!! hvy ndivyo unavyotaka uwe sharo kiasi hicho?
 
pole sana kijana ila kumbuka sheria nayo ni biashara nayo imelipiwa ada.je unataka upewe kila kitu bure?. lakini umetoa dukuduku zuri na litakuwa limewafikia walengwa

nakataa,kuna kitu ambacho siyo biashara?mbona upande wa afya kule madaktari mbona wanajibu kwa ufasaha zaidi? nenda jukwaa la elimu walimu wanajibu maswali vizuri zaidi na wanakupa mpaka rejea ya vitabu kwani wao hawafanyi biashara ya tuition?
 
pole sana kijana ila kumbuka sheria nayo ni biashara nayo imelipiwa ada.je unataka upewe kila kitu bure?. lakini umetoa dukuduku zuri na litakuwa limewafikia walengwa

ni kipi ambacho siyo biashara? udaktari,ualimu zote ni biashara na zote watu wametumia gharama kusoma lakini wanakupa majibu kwa undani kabisa,mfano daktari ataeleza chanzo cha tatizo,asali zake,namna ya kujitibu,na kujikinga na mwisho anakushauri tatizo likiendelea nenda zahanati,kituo cha afya au hospital iliyokaribu nawe.waalimu nao wanajibu maswali kwa ufasaha na wanakupa mpaka rejea ya vitabu ilihali wanatuition wanafundisha,sasa vp hawa mawakili?
 
Mwanasheria na muda...

nani asiyetumia muda?daktari hatumii muda kutoa majibu yahusuyo afya zetu?mwalimu hatumii muda kujibu maswali tuwaulizayo kwenye majukwaa yao? hoja yako ya muda pia naikataa, hvy mbadilike,toeni vifungu vya kisheria nasiyo kuleta porojo zenu hapa,ili uweze kumtofautisha mwanasheria na asiyemwanasheria ni majibu yanayoambatana na nukuu za kifungu husika nasiyo kuishia kusema tu et unahaki ya kuishi bila kukitaja kinapatikana wapi na kukinukuu
 
Unadhani muda wako kwangu uta mean chochote?
 
mfano,wewe unajibiwa na mwanasheria kuwa unahaki ya kuishi pasipo kifungu chochote kinachohusika, halafu anatokea mtu mwingine anaikiuka hy haki mfano polisi, mtu huyo akataka kukuchalenge hebu nitajie kifungu hicho unachodai nimekikiuka dhidi yako utamtajia nini?au utasema mi sijui ila nilimsikia wakili anasema tu kuwa ninahaki ya kuishi!! hvy ndivyo unavyotaka uwe sharo kiasi hicho?

Unajua tofauti ya mwalimu wa sheria na mwanasheria ambaye si mwalimu wa sheria?
 
Ebu mtoa mada kuwa na busara kwa kufikiri kidogo, wewe umewahi kwenda hospitali kwa kuumwa malaria ama kumpeleka ndugu yako huko, unachokijua ni kupata injection na dawa, ulale na neti. Umewahi kuuliza jinsi ya kutibu malaria? jinsi ya kujipa injection mwenyewe? jinsi ya kuweka vipimo vya dawa? kwanini? Jibu unalo wewe mwenyewe...
Pengine umewahi kupeleka kitu kwa fundi, kitu utakachouliza ni kwanini imekuwa mbovu na si inatengenezwa vipi... understood?
Unadhani wanasheria wanaogopa kuja hapa kukujibu, ila kwanini unadhani wamepita na kuondoka?
Ebu jifunze kutunza muda kwa kuleta mada za kujifunza na si mipasho na majibishano ambayo hayatatufikisha popote.

NB: Jaribu kuheshimu kazi za watu na kuwa na shukrani kwa kidogo unachopewa bure....
 
mleta maada ukipewa jibu au ushauri kwamba una haki fulani kwenye jambo fulani hilo jibu linakutosha kabisa kwa sababu tayari unakuwa umeshapata ufahamu kwamba unayo hiyo haki. ukitaka kuifafanua zaidi au kuitetea kwa kina ni lazma umtafute mwanasheria ili aweze kuifanya hiyo kazi kitaaluma , hii ni kwa sababu hata akikutajia vifungu havita kusaidia kwani mahakamani hutaji vifungu tu bali kuna namna ya kuwasilisha hoja, kuitetea na kutafsiri hivyo vifungu .
 
ni hv, kwanza mara nyingi wote haki zetu na uhuru wetu huwa tunazijua hata kama zitakiukwa, hvy haihitaji mwanasheria et aje akwambie kuna haki fulani et imevunjwa dhidi yako, ambacho sisi huwa hatukijui ni kuwa hii haki iliyovunjwa ni kutoka kifungu kipi cha sheria na kinasemaje? haihitaji mtu mwingine et aje akwambie et kuna haki yako imekiukwa!! hvy hatuulizi ili nijue haki yangu kama imekiukwa isipokuwa huwa tunajua kuwa hapa haki yangu imekiukwa,lakini je imekiukwaje na kifungu kipi cha sheria kimezungumzia hl? hapo ndo mwanasheria anapaswa ajibu kwa vifungu hvy.
 
Huna shukrani mleta mada.

hata ukiwa unapewa utumbo unataka ushukuru tu hata kama ni umeambiwa upuuzi? utofauti wa majibu ya mwanasheria na mtu tu ambae si mwanasheria ni katika kujibu maswali,mwanasheria nategemea atanukuu kifungu kisha anakueleza namna haki yako ilivyokiukwa lakini huyu asiye mwanasheria atajibu pasipo kutumia vifungu
 
Back
Top Bottom