Iyo ni legal profession. Tunaelekea hata kulazimisha walimu waje apa kusolve hesabu, tunaelekea kuwaamuru madaktari waje jf kutibu wagonjwa, tunakoelekea ni kumwambia fundi simu aje aeleze zana anazotumia apa jf, au ni kuhusu wanasheria tu? Nadhani uliowapa ujumbe watakujibu ila sijui kama umetumia njia sahihi. Pia sitegemei kama watakubali kutoa mkate huu bure, 'There is no free lunch in this world' Kazi ya sheria ni consultancy na na ukumbuke nchi yako imeweka utaratibu lazima pawe na 'Consultancy fee' je iyo utaitumaje kwa mtu aliyefanya analysis bure?
Mkuu pia sheria sio kutaja vifungu tu, iyo ni kujenga mazingira yaliyofanya ushauri wa mtu uyo kufikia apo, na kama si mtihani au kesi then halazimiki mtu kuongea kwa nukuu!
Ikumbukwe kuwa mwanasheria kamili anayefanya kazi iyo bila kipato kingine apo ndo njia ya mkate wake, ni sawa na gsana anavofungua duka asubuhi akitegemea wateja, je gsana akifungua duka aweke vitu ubarazani then wateja waje wabebe bila malipo??na apo apo uyu muuzaji kavilipia, kavinunua, kalala mje akivitafuta then agawe bure! Labda!
Labda nishauri tu kuwa hata apa Jf watu wengi hawapendi mtu aelezee jambo, akiwa genuine ataanza kukejeliwa , nakumbuka mwanajf mmoja aliwahi kuleta mada akilalamika eti jf kila mtu anajifanya mwanasheria...apo ni baada ya kukereka ambapo wengi wa wajuzi walikuwa wamechambua mada yake ilikuwa ni wakati ule ZZK anataka kufukuzwa na chama chake, nikashangaa kwa nini wakati wanasheria wameleta uchambuzi mzuri then watu wanaanza kuwakashifu unategemea watarudi tena?
Sijui ila watakuja uliowatumia salamu wajieleze, ila jua tu moja ya sababu ya Fani ya sheria kutumi maneno magumu na ya kizamani ni kuongeza value pamoja na kuifanya sio kila mtu aielewe. Ukitaka kuielewa lazima uwatafute watalaam wakupe A, B,C... na kwa kuwa mtatumia muda basi Time is Money! Lazima uP.A.Y.E PAY AS YOU EARN EDUCATION!
Nakutakia muda mwema ndugu!