Wanasheria Badilikeni, Toeni majibu ya kisheria

Wanasheria Badilikeni, Toeni majibu ya kisheria

Halafu Hv Mnaotetea Upuuzi Huo Hv Ni Wanasheria? Hapa Hapa, Nyinyi Kwa Nyi Mnatofautiana, Mmoja Amedai Mwalimu Kazi Yake Ni Kufundisha Na Kunukuu Vifungu Vya Sheria Na Mwanasheria Kazi Yake Kutafsri Sheria, Na Wewe Hapa Unasema Mwanasheria Ndiye Anayenukuu Sheria!!

Ebu weka alama hapo palipoandikwa hivo (blue) na mie mkuu...
 
Kwahiyo Hili Jukwaa Wewe Limekuajili Utafsri Sheria? Huruhusiwi Kunukuu Vifungu Kwa Kuwa Halikukuajili Kwa Kazi Hy? Hv Jukwaa La Elimu Likiulizwa Swali Afsa Elimu Haruhusiwi Kujibu Kwa Kuwa Hafundishi Darasani? Hv Ukiwa Mwanasheria Ukanukuu Vifungu Utafukuzwa Kazi? Mambo Ya Ofisini Au Majukumu Ya Ofisini Yaishie Ofisini Na Ya Humu Ndani Hayahusiani Na Majukumu Yenu Ya Ofisi. Sasa Kama Wewe Unajua Mwal Wa Sheria Ndiye Anaepaswa Ajibu Wewe Kwanini Unakimbilia Kujibu? Na Kama Unasema Mwalimu Wa Sheria Ndiye Anaepaswa Anukuu Vifungu Kwahiyo Jukwaa Hili Litakuwa Linawahusu Walimu Wa Sheria,je La Kwenu Ni Lipi?
Hofu yangu ni kuwa hata ukiwekewa vifungu hutaelewa badala yake tutakua tumepotezeana muda. Mbona izo ACT zimejaa kwenye mitandao!!! kama shida ni vifungu, huna haja ya kuja kuuliza hapa. Nenda kasome vifungu kwenye mitandao.:smile-big::smile-big:
 
Iyo ni legal profession. Tunaelekea hata kulazimisha walimu waje apa kusolve hesabu, tunaelekea kuwaamuru madaktari waje jf kutibu wagonjwa, tunakoelekea ni kumwambia fundi simu aje aeleze zana anazotumia apa jf, au ni kuhusu wanasheria tu? Nadhani uliowapa ujumbe watakujibu ila sijui kama umetumia njia sahihi. Pia sitegemei kama watakubali kutoa mkate huu bure, 'There is no free lunch in this world' Kazi ya sheria ni consultancy na na ukumbuke nchi yako imeweka utaratibu lazima pawe na 'Consultancy fee' je iyo utaitumaje kwa mtu aliyefanya analysis bure?

Mkuu pia sheria sio kutaja vifungu tu, iyo ni kujenga mazingira yaliyofanya ushauri wa mtu uyo kufikia apo, na kama si mtihani au kesi then halazimiki mtu kuongea kwa nukuu!

Ikumbukwe kuwa mwanasheria kamili anayefanya kazi iyo bila kipato kingine apo ndo njia ya mkate wake, ni sawa na gsana anavofungua duka asubuhi akitegemea wateja, je gsana akifungua duka aweke vitu ubarazani then wateja waje wabebe bila malipo??na apo apo uyu muuzaji kavilipia, kavinunua, kalala mje akivitafuta then agawe bure! Labda!

Labda nishauri tu kuwa hata apa Jf watu wengi hawapendi mtu aelezee jambo, akiwa genuine ataanza kukejeliwa , nakumbuka mwanajf mmoja aliwahi kuleta mada akilalamika eti jf kila mtu anajifanya mwanasheria...apo ni baada ya kukereka ambapo wengi wa wajuzi walikuwa wamechambua mada yake ilikuwa ni wakati ule ZZK anataka kufukuzwa na chama chake, nikashangaa kwa nini wakati wanasheria wameleta uchambuzi mzuri then watu wanaanza kuwakashifu unategemea watarudi tena?

Sijui ila watakuja uliowatumia salamu wajieleze, ila jua tu moja ya sababu ya Fani ya sheria kutumi maneno magumu na ya kizamani ni kuongeza value pamoja na kuifanya sio kila mtu aielewe. Ukitaka kuielewa lazima uwatafute watalaam wakupe A, B,C... na kwa kuwa mtatumia muda basi Time is Money! Lazima uP.A.Y.E PAY AS YOU EARN EDUCATION!

Nakutakia muda mwema ndugu!
 
mimi mwenyewe nimeona sana hiyo kitu tunahitaji legal consultants wawe wnakuja hapa kutujibia maswali. kuna mmoja aliweka post yake anasema kama una swali lolole kihusu sheria ya ndoa uliza. nimejenga hoja yangu halafu nikaweka na swali kajibu vitu vya ajabu anasema umeshajijibu mimi nijibu nini? huyu ni mwanasheria ambaye tunamaanisha ni consultant ndo anajibu hivyo
Mkuu unanionea bure. Hapa jukwaani hatuwezi kusema yote. Hii ni biashara yetu. Shukuruni kwa tunachowapa
 
Back
Top Bottom