Wanasheria hili linawahusu

riara

Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
30
Reaction score
45
Nina assets ambazo nimepata nikiwa sijaoa (single) kama ifuatavyo
Nyumba , mashamba , Mifugo pamoja na duka la pembejeo
Ninachoitaji
(a) Namna ya kumiliki assets hizi kisheria ili nitakapooa mwanamke wangu asiwe na haki katika assets hizi mpaka nitakapoamua mwenyewe aidha kumilikisha familia yangu au vinginevyo.
(b) Taratibu za kisheria ninazotakiwa kufuata ili ikiwa ndoa itavunjika mwanamke asipate gawio lolote katika assets hizi alizonikuta nazo pindi tunafunga ndoa.
 
Kama wewe utamiliki papuchi ya mkeo, kwa nini ukatae mkeo kumiliki mali zako?

Omba upate mwanamke mwema atalinda mali zako hizo unazotaka kumnyima umiliki.
 
Kama wewe utamiliki papuchi ya mkeo, kwa nini ukate mkeo kumiliki mali zako?
Omba upate mwanamke mwema atalinda mali zako hizo unazotaka kumnyima umiliki.

Mkuu umetumia hekima kubwa sana kutoa jibu hili, both Mume na mke wakiwa na hofu ya Mungu mambo kama hayo ni madogo sana
 
Tunajisahau sana mkuu.

Mke ni mtu muhimu sana katika maisha ya mwanaume, ana haki zake kama mke kutoka kwa mume wake. Lakini kwa kuwa hatujui mambo kama hayo ndio maana tunajikuta tunaweka fikra zisizo sawa.
 
Ni kweli mke ni mtu muhimu ila hawa wanawake wa kikazi hiki cha sasa wamepoteza uaminifu lazima tuishi nao kwa akili ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari. kinga ni bora kuliko tiba
 
swali zur!
ntarud soon!
 
KWA UTARATIBU WA KAWAIDA KISHERIA HIZO MALI ULIZOPATA UKIWA NA HARAKATI ZAKO BINAFSI BADO ZITABAKI KUWA ZAKO NA KUJUA CHA KUFANYA NAZO. ILA PALE UTAKAPO ANZA MAISHA YA NDOA NA MWENZA WAKO NDIPO YALE MTAKAYOVUNA MKIWA WOTE ITAKUWA HESABU YA NGUVU MOJA HATA KAMA MWANAMKE ATAKUWA MAMA WA NYUMBANI LAZIMA MCHANGO WAKE WA SHUGHULI ZAKE KAMA MAMA NA MKE APEWE THAMANI YAKE KIKAMILIFU. KWAHIYO KUWA MAKINI NDUGU. NA USIWE NA DHAMIRA ZA NAMNA HII UNAKARIBISHA MIKOSI PIA KATIKA MATARAJIO YAKO KAMA MAANDALIZI YA KUKOMOA MTU WA UPANDE MWINGINE. PANGILIA MIPANGO YAKO VYEMA NA FURAHIA MAISHA YAKO KWA BUSARA/HEKIMA.
 
Mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla ya ndoa. Ndoahaiwezi kuwa kigezo cha lazima cha kubadilisha umiliki wa mali yamwanandoa isipokuwa tu kama wenyewe wamekubaliana hivyo napia haimzuii mwanandoa kujipatia na kumiliki mali yake binafsiakiwa katika ndoa. Kifungu cha 58 kinaeleza haki hiyo kwa maana iyo hii kitu igeuze tu kwa upande wako mkuu inafanya kazi kwa wote case closed.
 
Kifungu cha 58 cha kitu gani??
 
Weka kifungu cha marriage acts tujisomee wenyewe.
 
Mamaee
Mkuu naona hutaki kucheka na nyani
 
Kifungu cha 58 cha kitu gani??
Sheria ya Ndoa, Sura Na. 29, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 inatambua kuwepo mazingira yasiyoweza kurekebishika yanayoweza kupelekea ndoa kuvunjika, hivyo sheria huzungumzia talaka. Talaka ni ruhusa ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzie.

Chombo pekee chenye uwezo wa kuvunja ndoa ni MAHAKAMA. Kwa kawaidamahakama hutoa talaka kwa ndoa ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi. Lakini mahakama inaweza kutoa talaka hata kama ndoa haijadumu kwa kipindi hicho cha miaka miwili iwapo mlalamikaji atatoa sababu nzito sana.

Sababu za kuomba au kutolewa Talaka

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kupelekea kutolewa kwa talaka:

• Ugoni • Ukatili• Kulawiti • Kichaa • Uasi (Utoro)• Kuzembea wajibu kwa makusudi• Kifungo • Dhana ya kifo • Tofauti za itikadi au Dini

Kutengana kwa wanandoaUtaratibu wa Kufuata wakati wa kuvunja ndoa

Mwombaji atatakiwa kwenda Baraza la Usuluhishi la ndoa yaliyoteuliwa katika ngazi za wilaya kupitia ofisi za wlaya au katika taasis za dini zilizopewa kibali, Mfano: BAKWATA, Kanisani au Baraza la sheria la Kata.

Mwombaji ataeleza shauri lake kwa Baraza husika na kama Baraza la Usuluhishi litashindwa kusuluhisha basi litatoa hati inayoruhusu shauri hilo lisikilizwe na Mahakama kwa utatuzi. Mwombaji ataandaa madai ya kuvunja ndoa na atayawasilisha Mahakamani kama utaratibu wa kisheria unavyoelekeza.

Ukiambatanisha cheti cha ndoa kama kipo, hati ya Baraza la Usuluhishi na hati yoyote ile ambayo ungependa Mahakama ione

Sheria hii pamoja na mambo mengine inaeleza juu ya haki ya mke kumiliki mali katika ndoa na masuala ya mgawanyo wa mali endapo talaka itatolewa Sheria ya Ndoa Kifungu cha 58 kinaeleza haki hiyo.

Viambatanisho muhimu wakati wa kuwasilisha madai ya Talaka

1. Cheti cha ndoa kuonyesha kwamba kulikuwa na ndoa halali

2. Ainisha sababu za kuwepo kwa mgogoro baina ya wanandoa mfano, ugoni, ukatili na madhara yaliyotokea

3. Barua ya Baraza la usuluhishi kuthibitisha kuwa jitihada za kusuluhisha mgogorozimeshindikana

4. Hati ya madai ya talaka honyesha

• Ndoa ilifungwa lini, aina ya ndoa, muda wa ndoa, mahali mlipoishi

• Watoto wa ndoa, jinsi na umri wao kama wapo

• Mali mliyochuma wakati wa ndoa yenu

• mahakama itatoa uamuzi kama:

  • Ndoa imevunjika na talaka itolewe au kuwepo utengano wa muda kwa wanandoa.
  • Mgawanyo wa mali mliyochuma.
  • Mamlaka ya kukaa na watoto pamoja na matunzo yao
  • Mwenzi wako alipe gharama za kesi
  • Amri nyingine yoyote ambayo mahakama itaona inafaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…