Wanasheria hili linawahusu

Wanasheria hili linawahusu

Sheria ya Ndoa, Sura Na. 29, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 inatambua kuwepo mazingira yasiyoweza kurekebishika yanayoweza kupelekea ndoa kuvunjika, hivyo sheria huzungumzia talaka. Talaka ni ruhusa ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzie.

Chombo pekee chenye uwezo wa kuvunja ndoa ni MAHAKAMA. Kwa kawaidamahakama hutoa talaka kwa ndoa ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi. Lakini mahakama inaweza kutoa talaka hata kama ndoa haijadumu kwa kipindi hicho cha miaka miwili iwapo mlalamikaji atatoa sababu nzito sana.

Sababu za kuomba au kutolewa Talaka

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kupelekea kutolewa kwa talaka:

• Ugoni • Ukatili• Kulawiti • Kichaa • Uasi (Utoro)• Kuzembea wajibu kwa makusudi• Kifungo • Dhana ya kifo • Tofauti za itikadi au Dini

Kutengana kwa wanandoaUtaratibu wa Kufuata wakati wa kuvunja ndoa

Mwombaji atatakiwa kwenda Baraza la Usuluhishi la ndoa yaliyoteuliwa katika ngazi za wilaya kupitia ofisi za wlaya au katika taasis za dini zilizopewa kibali, Mfano: BAKWATA, Kanisani au Baraza la sheria la Kata.

Mwombaji ataeleza shauri lake kwa Baraza husika na kama Baraza la Usuluhishi litashindwa kusuluhisha basi litatoa hati inayoruhusu shauri hilo lisikilizwe na Mahakama kwa utatuzi. Mwombaji ataandaa madai ya kuvunja ndoa na atayawasilisha Mahakamani kama utaratibu wa kisheria unavyoelekeza.

Ukiambatanisha cheti cha ndoa kama kipo, hati ya Baraza la Usuluhishi na hati yoyote ile ambayo ungependa Mahakama ione

Sheria hii pamoja na mambo mengine inaeleza juu ya haki ya mke kumiliki mali katika ndoa na masuala ya mgawanyo wa mali endapo talaka itatolewa Sheria ya Ndoa Kifungu cha 58 kinaeleza haki hiyo.



Viambatanisho muhimu wakati wa kuwasilisha madai ya Talaka


1. Cheti cha ndoa kuonyesha kwamba kulikuwa na ndoa halali

2. Ainisha sababu za kuwepo kwa mgogoro baina ya wanandoa mfano, ugoni, ukatili na madhara yaliyotokea

3. Barua ya Baraza la usuluhishi kuthibitisha kuwa jitihada za kusuluhisha mgogorozimeshindikana

4. Hati ya madai ya talaka honyesha

• Ndoa ilifungwa lini, aina ya ndoa, muda wa ndoa, mahali mlipoishi

• Watoto wa ndoa, jinsi na umri wao kama wapo

• Mali mliyochuma wakati wa ndoa yenu

• mahakama itatoa uamuzi kama:


  • Ndoa imevunjika na talaka itolewe au kuwepo utengano wa muda kwa wanandoa.
  • Mgawanyo wa mali mliyochuma.
  • Mamlaka ya kukaa na watoto pamoja na matunzo yao
  • Mwenzi wako alipe gharama za kesi
  • Amri nyingine yoyote ambayo mahakama itaona inafaa
 
Back
Top Bottom