Wanasheria JF tunatia aibu

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Hii imekua ni kawaida sasa kukuta mtu wa kawaida tu (layman) asiejua sheria kuuliza swali la kisheria au kutaka msaada wa kisheria then ikapita ata week nzima bila mtu huyu kusaidiwa, ni sawa kusaidiana sio lazima na kwakua huduma hii utolewa kwa malipo ya fedha, ila je nini kusudio la jukwaa hili ambalo wewe mwanasheria ni member? Pili, kwani kutoa ushauri mdogo tu tena mwingine ni wa vitu vidogo kabisa tena vitu vya kuandikiwa ata sentesi mbili tu za maneno ila kusaidiwa inakua tabu sana.

Nafikiri lengo la jukwaa lilikua ni zuli tu na kuwasaidia hawa ambao hawana uelewa kwa kiasi flani wa masuala ya sheria, dunia ni kubwa waungwana utakae msaidia leo ndio atakae kusaidia kesho, alafu pengine ndio anaweza kua mteja wako huyo.

Hili swala la watu kutaka msaada wa kisheria na wasisaidiwe kwa wakati muafaka au majibu mepesi mepesi na kejeli nyingi linakera sana, yaani katatizo kadogo tu mtu hajibiwi ata mwezi au hapati majibu kabisa while humu jf kila mtu ana dai ni mwanasheria na majukwaa mengine ana tamba sanaa ila jukwaa hili kimyaaa! Sasa si tumesomeshwa kwa kodi za hawa watu wakawaida jamani.

Anyway ni mtazamo tu na binafsi nliona kama ata mie nimekua sitendi haki kwa namna moja au nyingine ktk jukwaa hili pi, basi tubadilikeni waungwana, tulifufue jukwaa hili kwa kila namna. Na kwa kuanzia ntajitolea kumjibu kila anaetaka msaada kwa kadri niwezavyo na nipatapo muda walau kwa kiasi tu.

Balozi Mpya Jukwaa la sheria.
 
Miongoni mwa KADA ninayoidharau huku Duniani ni hii ya Sheria Ingawa ni muhimu Lakini watu wenye nayo ndio
HOVYO kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawakili tupo busy sana na kazi za wateja, kama anataka ushauri aende ofisi yeyote ya mawakili atasaidiwa, huku mitandaoni huwezi kutoa ushauri maana kuna facts anakua amezificha hivyo ni ngumu kumshauri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili liko wazi, ila ata elimu ya awali tu au kutoa ata maelekezo ya namna atakapo pata msaada huo, na uenda akawa ata ndo mteja wako huyu.

Muda unaweza kua tatizo pia, ila mbona kila saa tunawaona kule MMU, Siasa na kwengineko au whatsap kule mko masaa 24 online tu tena kwa mambo ya kijinga jinga tu.
 
Mawakili tupo busy sana na kazi za wateja, kama anataka ushauri aende ofisi yeyote ya mawakili atasaidiwa, huku mitandaoni huwezi kutoa ushauri maana kuna facts anakua amezificha hivyo ni ngumu kumshauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna PM n.k...
Ushauri sio kesi mkuu ushauri ni ABC kwa ajili ya kesi....kama unashindwa kushauri kwenye public utawezaje kushauri ofisini?
 
Kuna PM n.k...
Ushauri sio kesi mkuu ushauri ni ABC kwa ajili ya kesi....kama unashindwa kushauri kwenye public utawezaje kushauri ofisini?

Mkuu ni kawaida tu kwa kada hii kulipiwa Ushauri wake, ila hili swala la kushauri ni busara tu, na ni uungwana tu, sasa wengine wamekwama hapa hali inayozua mashaka kidogo kuhusu uelewa wao.
 
Ni wachache tu mkuu
Kiongozi wewe unaweza usiwe mmoja wao lkn asilimia kubwa ni HOVYO
pita kule jukwaa la Sheria kuna watu wanauliza mambo wapate Ushauri kama ilivyo Forums nyingine za Jf unaweza kusubiri kule kama una Kesi itaisha na Ulichouliza hakuna majibu.... mimi ni mmoja wa watu waliotaka kujua Jambo kule tangu mwaka 2015
Hakuna aliepita Kutoa ushauri

Naam mkuu, baadhi ya mambo yalionifanya nikaandika uzi huu ni kwa sababu kama hizi, kkuna uzi wa miaka ya 2016 mpaka leo haikuwai kujibiwa na watu walikua na shida za haraka kweli, tena wengine ni wakuwajibu tu nenda mahali flani na ufanye iv na iv, yeah ni lazma tufanye jambo vinginevyo hili jukwaa halina maana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…