Hiyo ndio siasa, hasa katika baadhi ya mataifa yasiyo thamini utawala wa kisheria.
Ni ukweli usiopingika kwamba mahakama zetu zipo imara na zimesheheni wasomi wenye weledi. Na kazi zake kuu kwa miaka mingi toka Uhuru ni kutafasiri jinai zote dhidi ya Jamhuri.
Sasa sijui hapa labda neno 'UFISADI' ndio jipya. Lakini kisheria yote hii ni jinai, na mahakama haijawahi shindwa toka kuanza kuhudumu kazi zake.
Wazo la msingi hapa ni kuishauri serikali kuziboresha mahakama zetu na kuwajengea masilahi bora watendaji wake.
Kauli ya Raisi kuokoa fedha za umma ianzie hapa.