Wanasheria masuala ya kazi msaada tafadhali

Wanasheria masuala ya kazi msaada tafadhali

frank mkweli

Member
Joined
Aug 9, 2013
Posts
92
Reaction score
12
Habari wakuu vipi wazima?

Mimi mzima nina swali naomba nikuulize.

Hivi kuna Sheria ya kumshitaki mwajiri kama alikuwa haweki hela za NSSF na loan board ukamshitaki, na lingine kama bima yangu haifanyi kazi.

Natakiwa nifanye nini na pia zile hela za helsb ambazo zimekatwa kwangu hazijaenda naweza zi claim cash?
 
Maelezo yako hayapo clear.
 
Ziandikie barua hizo taasisi yaan NSSF na HESLB kuwajulisha kuwa umekatwa pesa na mwajiri kuwasiliaha kwao ambatanisha na salary slip nakala ya barua mpe mwajiri. Tunza nakala yako.
 
Hivi kuna Sheria ya kumshitaki mwajiri kama alikuwa haweki hela za NSSF na loan board ukamshitaki, na lingine kama bima yangu haifanyi kazi.
1. kuhusu NSSF wewe huna mamlaka ya kumstaki Mwajiri isipokuwa itabidi utoe taarifa katika ofisi za NSSF alafu wenyewe watafanya ufuatiliaji na ikibidi kufungua kesi dhidi ya Mwajiri wako,kwani wao ndio wana mamlaka kisheria.
2.HESLB-una uhakika kuwa mwajiri alikuwa hawakilishi mkato yako katika bodi ya mikopo?
hapa pia utaratibu unabaki wa wewe kutoa taarifa bodi ya mikopo na wao watafanya ufuatiliaji pamoja na kufungua kesi dhidi ya Mwajiri wako (endapo itabidi kufanyika hivyo),ila mara nyingi kinachofanyika Bodi ya mikopo wanaandika barua kwa Mwajiri kuonyesha mIchango ambayo haikulipwa kwa mujibu wa sheria pamoja na penalty(adhabu)ya kiasi chote cha pesa ambacho kilipaswa kuwasilishwa katika bodi ya mikopo.

3.Kuhusu bima ya Afya-Naomba kujua unatumia BIMA gani?na utaribu wa malipo wa huduma husika unafanyika vipi?

Natakiwa nifanye nini na pia zile hela za helsb ambazo zimekatwa kwangu hazijaenda naweza zi claim cash?
HESLB:huwezi kupewa kiasi chochote incash kwani sheria hairuhsu hivyo,hivyo uanweza kusoma muongozo hapo juu pia wasiliana na ofisi za HESLB kwa ufafanuzi zaidi.
Japo kupata hela za NSSF incash inawezakana(negotiation)na mwajiri endapo kama ulikuwa ukikatwa hela kwa ajili ya NSSF.
 
Back
Top Bottom