Unamaanisha ndoa za mkeka? Nilishamsikia waziri wa nchi ofisi ya Rais katiba na utawala bora Zanzibar akilalamikia hili jamo mwaka jana kuwa nyingine zikufungwa mpaka katika kituo cha polisi. Ofisi ya Kadhi Mkuu, nayo ililalamikiwa kwa hili. Ndoa zilizofungwa kimila zinatambulika na sheria ya ndoa. Ili zitambulike kisheria inabidi zifungwe kuwa kufuata desturi na taratibu za mila husika. Kwa kaida sheria za kiislamu zinatambulika kama moja ya sheria za mila na desturi zetu.
Ndoa hali ya kiislamu ni lazima ifuate mashari yafuatayo.
1. Anayeoa na anayeolewa lazima wakubali kuoana kwa hiyari yao wenyewe.
2. Lazima walii (wazazi au walezi) wa msichana waidhinishe hiyo ndoa.
3. Lazima kuwe na mashahidi wawili waadilifu katika hiyo ndoa.
4. Lazima isomwe khutba ya kuozesha.
Kama kijana na msichana walishaishi pamoja na kuzini inabidi kuwe na sharti jinginne la kuwatenganisha kwa muda ili kuwa na uhakika kama msichna ana mimba. Katika kipindi hicho inabidi wote warudi kwa ala kwa kuomba msamaha, kutubu na kutia azma ya kutorudia, kuacha maasiya na kufanya mema mengi. Yote haya yakitimizwa ndoa inaweza kufungwa na kutambuliwa kisheria baada ya kusajiliwa na sheria ya ndoa.
Kwa vile ndoa ni muunganino wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke, sidhani kama ndoa za mkeka zinatambulika kisheria kwa sababu ni za kulazimishana. Makubaliano ya hiari ni element muhimu sana kwenye ndoa za aina zote, ziwe za kawaida au za kimila.