kama mkataba unao manake unakuonesha nani mwajiri wako,kimsingi huyo ndo unaweza kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. Hapa umesema mko kama hamsini hivi,hatujajua mnataka shitaka lenu kuwa la kawaida(ordinary civil suit) au la uwakilishi (representative civil suit) ni lazima kujua kuwa kwa mjibu wa sheria hapa kuna taratibu tofauti za kufuata kufungua mashitaka hayo.
sijajua uko maeneo yapi lakini kama unaweza mtafute mwanasheria karibu yako au kituo chochote kinachotoa msaada wa kisheria,kwa ushauri zaidi,mana atakuwa na nafasi ya kupitia mkataba wako na kuona haki zako ziko namna gani.
Ingawa kwa maelezo yako inaonekana mnahaki ya kulipwa sitahili zenu. Usiogope tatizo watanzania wengi ni waoga sana linapokuja swala la kumshitaki mwajiri wako. Unapopigania haki yako hupaswi kuwa mwoga wala kukata tamaa,haki ya mtu haiwezi kupotea mwanadamu atakachofanya ni kuichelewesha tu,kila la heri na mungu akutangulie.