Mndwyika.wetu
JF-Expert Member
- Jul 15, 2012
- 652
- 829
Tusubiri waje tuwasikieKikatiba ni wakati gani maandamano ya wanachi yanapokua halali na wakati gani yanakua haramu?
Je maandamano ni hisani kutoka polisi?
Je katiba inasema maandamano halali ni yale tu ya kuunga nkono na kusifia wakuu ?
Maandamano yakiwa ni ya kupinga, kulalamika (picketing) yanakua haramu?
Lipo tatizo moja la sheria za Tanzania, inakupa jambo kwa mkono wa kulia kisha inakupoka kwa mkono wa kushoto.
Maandamano yameruhusiwa kikatiba, hvyo ni Constitutional right, lakini katiba hyo hyo imeweka masharti ya kufuata ili kufanya maandamano, hivyo sio Absolute right. Masharti hayo ni kuomba ulinzi wa polisi(kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa). Sheria ya polisi inaipa jeshi la polisi mamlaka ya kuzuia kutendeka jambo lolote ambalo wanaamini litahatarisha amani na usalama wa nchi. Sasa ukizisoma katiba na sheria ya vyama vya siasa , na ya jesh la polisi 'kwa ujumla wake', utaona polisi hawana mamlaka ya kuzuia mikutano, bali inatoa fursa ya polisi na waandamanaji kukubaliana muda na mazingira ya ufanyikaji maandamano hayo. Sasa wakubwa wanalijua hli ndio maana mapendekezo ya sheria mpya ya vyama vya siasa yanajaribu kuweka masharti makali kidogo.
Of course ni polisiHaya tuambie nani anaetoa kibali cha maandamano?
Absolutely.Tunatakiwa kujua kwamba katiba ni sheria mama inayotoa haki tu ila namna ya hio haki, mipaka ya hio haki na utaratibu wa kuipata hio haki hua inatolewa na sheria zingine za bunge, ndo maana kwenye katiba hakuna sehemu inasema ukiuua kwa kukusudiwa basi unyongwe!
Ni ukweli kua katiba inatoa haki ya maandamano kwa watu, taasisi nk bila bugdha au kuathiri sheria zingine za nchi, ibara ya 30 ya katiba inasema kua ibara zilizomo ndani ya katiba hazi haramishi sheria nyingine za nchi.
Sasa maandamano yana ratibiwa na kuandaliwa chini ya sheria ya jeshi la polisi na kazi saidizi ambayo inataka ili maandamano yawepo basi yafaa kwanza waandaji wa maandamano waombe kibali cha maandamano hayo masaa 48 kabla ya kuandamana... Na endapo hili halitofuatwa basi maandamano hayo hayatakua halali kisheria, lakin endapo polisi wakikataa kutoa kibali icho basi wandamanaji wanaweza kufungua kesi mahakama kuu chini ya hati ya dharura wakiwashtaki mwanasheria mkuu wa serikali na mkuu wa jeshi la polisi waieleze mahakama sababu hasaa ni nini ya kuwanyima watu haki yao ya kikatiba.
Lakini kitu cha juu Kabisa kuliko vyote kwenye mfumo wa sheria ni busara, endapo itaonekana maandamano yale yalikua yana ulazima sanaa na uharaka sanaa kuinusuru jamii basi yatakua halali na ya haki bila hata kibali chochote kwa kile kitakachoitwa "kwa manufaa ya jamii".