Wanasheria naomba mnisaidie hili

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Watu tuliowekeza kwenye biashara ya daladala tunakumbana na shida nyingi sana.
Utasikia dereva anakupigia simu eti gari imekamatwa na imepelekwa kituoni halafu huyo dereva aliyefanya hilo kosa tena wakati mwingine ni la kizembe kabisa yuko huru nje , tena anacheka na kupiga stori na wenzake.
Halafu wewe mwenye gari unaacha shughuli zako na kuanza kuhangaika kuitoa gari.
Swali kwa wanasheria , Je gari ndo yenye makosa ?au ni huyu dereva ambaye yeye ni kiumbe mwenye akili anayejua mema na mabaya?
Na kama ni dereva ndo mwenye makosa kwa nini polisi wanakomaa na gari kituoni , huku dereva akichekelea nje?
 
mkuu vumilia utakuja tu kuelewa mchezo!Ukishakomaa ndio utakuja kugundua kumbe faini ya Laki unapunguza tu sifuri moja na mambo yanaenda!,Dereva atawekwa ndani tu kama amegonga ameuwa mtu au amesimamishwa akusimama na wazee wakamfukuzia wakamkamata
 
Hili swali
Labda nikusaidie ni hivi umechukua mkopo bank ukanunua daladala, ni lazima daladala lako lifanye kazi liingize hela ili upate hela ya kulipa mkopo na kuendesha maisha asubuhi umeenda kibaruani dereva anakupigia simu eti gari imekamatwa kwa sauti ya kilevi, unaomba ruhusa kazini ikiwezekana unajaza likizo ukaitoe gari yako kufika kituoni unaambiwa kuwa dereva amepita taa nyekundu ukimpigia simu kujua alipo anakwambia nimekula deiwaka kwenye gari nyingine....swali la msingi kwa nini kwa makosa kama haya ya kibinadamu wasiwe wanazuiliwa hawa binadamu tofauti na sasa wanazuia magari ambao wamiliki wake hawana hatia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…