Wanasheria Naombeni Msaada Wa Kisheria Ndugu Yangu Ana Tatizo.

Koloboy

Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
61
Reaction score
154
Naombeni Msaada Wa Kisheria Ndugu Wanasheria Juu Ya Matatizo Yaliyojitokeza.
Ni Hivi Kuna Ndugu Yangu Mmoja Alipata Kufunga Ndoa Mwaka 2015 , Na Baada Ya Kufunga Ndoa Wakaendelea Kuishi Na Mkewe Kama Wanandoa.

Na Baada ya mda Yule Mwanamke Akaonekana Kama Ni Mjamzito Kwa Hiyo Mume Hakuwa Na Shaka juu Ya Hiyo Mimba Na Badala Yake Hapo Mume Aliendelea Kuihudumia Ile Mimba Akiamini Kuwa Ni Damu Yake Halali Ambayo Imepatikana Kwa Uwezo Wa Mungu Kuleta Nusra Ndani Ya Ndoa.

Lakini Tatizo Likaanza Kujitokeza Baada Ya Yule Mke Kujifungua Mtoto , Yani Hapa Mwanamke Alianza Kudai Talaka Ili Aachwe Akisema Kuwa Amechoshwa na Maisha Yale.
Mume Huyu Alikuwa Mkalimu Sana Na Baadae Akaamua Kumuacha Yule Mwanamke.
Sasa Baada ya Mwanamke Kuachwa Na Yule Mume Hakutaka Tena Yule Mtoto Hata Akikua aje Kwa Baba Yake Wa Ndoa Ama Baba Yake Aje Kumuona Mtoto Wake.

Mwanamke Alianza Kuweka Vipingamizi Vya Kutotaka Baba Aonane Na Mwanae, Lakini Huduma za Hela Alikuwa Anazipokea Kwa Njia Ya Muamala Wa Simu.
Maisha Yakasonga Mpaka Mtoto Amefikisha Almost Kama Miaka Miwili Mpaka Sasa Hali Ikawa Ndio Hiyo Hiyo Ya Mama Kutotaka Mwanae Aonnane na Babake Wa Ndoa.

Mume Akaona Sio Shida Akaanza Kufuata Sheria Juu Ya Kupata Haki yake Ya Mtoto Na Akaenda Kuongea Na Wazazi Wa Yule Binti Ambao Waliozesha Ile Ndoa Na Wazazi Wakaridhia Amchukue Yule Mtoto Lakini Binti Yao Alikuwa Hataki Hilo Jambo.

Kwa Hiyo Kwa Ufupi Kesi Ikafika Polisi Na Watu Wa Ustawi Wa Jamii Walikuwepo Pia Kwenye Suruhu Hiyo Ila Baadae Yule Binti ( Mwanamke ) Alisema Kuwa Yule Mtoto Si Mtoto Wa Huyu Mwanaume Kwa Sababu Aliolewa Wakati Akiwa na Mimba Ya Kijana Mwingine Na Baadae Ikathibika Kabisa Kuwa Hata CLINIC CARD Pia Alisha Badirisha Jina Kutoka Kwa Baba Wa Ndoa Kwenda Kwa Baba Wa Nje.

Na Polisi Na Watu Watu wa Ustawi Wa Jamii Wakiwepo Wakasema Ili Kesi Ama Baba Wa Harusi Ampate Mtoto Wake Inatakiwa Waende Wakaangalie/ Wakapime DNA.

Kwa Hiyo Naombeni Msaada Wa Kisheria Juu Ya Hali Na Mazingira Ya Mgogoro Huo jinsi Ulivyo Na Ni Yupi Mwenye Mtoto Halali Kati Ya Hao Wazazi Na Yupi Mwenye Makosa Hapo???

Na Ili Baba Wa Ndoa Ampate Mtoto Wake Anatakiwa Afanye Nini Hapa???

Tafadhari Wanasheria Wetu Mtusaidie Juu Ya Hilo Jambo

Anayeweza Kutag Naombeni Amtag PETRO E. MSELEWA
 
Wanawake sisi Sametime tuna matatizo.
Usikute hako Kijana anakokalilia hakana mbele wala nyuma.

Ujana haubagui.[emoji53][emoji53]
 
Mwanamke siku zote ndo wanaojua baba halisi wa mtoto!!!! Kwahiyo hapo hakuna haja ya DNA, mke keshasema mtoto sio wake. Ampe talaka tu. Poleni sana. Sometime wanawake ni wapumbavu sana.[emoji51][emoji51][emoji51]
 
pole,ila lichukulie hili jambo kisheria zaidi,tumia pesa please pima parternity test,matokeo yake will put this issue to bed.
 
Kwa tamaduni za ki kurya hata kama bibi arusi alikuja na mimba bado mtoto ni mali ya yule aliyeoa, lakini bado asikate tamaa mwambie yule ni mwanae hata kama DNA itagoma maana mtoto hana shida yoyote maana yeye hakupenda ayumbishwe hivyo ni tamaa za wazazi wake na ili huyo ndugu yako aweze kubalikiwa mwambie aendelee kumtumza mtoto.
 
Kwa issue hii DNA ndo msemakweli.

Sent from my Compaq desktop-1997 Using Jamiiforums desktop app
 
Mkuu mama wa mtoto ndio hujua baba wa mtoto!! Ukishajua tu hapo itakusaidia huko kwingine.
 
Aachane na mtoto aombe miamala yake yote ya simu ilipwe na hao wazinifu wawili,pia adai matunzo yoote ya kumtunza hayawani
 
Wanawake sisi Sametime tuna matatizo.
Usikute hako Kijana anakokalilia hakana mbele wala nyuma.

Ujana haubagui.[emoji53][emoji53]
Yani We Acha tu!!!

Mpaka anakubari Kuolewa Aiseee Wakati Ana Msela nje Huko Daaah
 
Mwanamke siku zote ndo wanaojua baba halisi wa mtoto!!!! Kwahiyo hapo hakuna haja ya DNA, mke keshasema mtoto sio wake. Ampe talaka tu. Poleni sana. Sometime wanawake ni wapumbavu sana.[emoji51][emoji51][emoji51]
Tunalijua Hilo Mkuu Lakini Sasa Anapataje Haki Zake Za Msingi Kama Vile Gharama Ambayo aliitumia Kumlea Mtoto???
 
pole,ila lichukulie hili jambo kisheria zaidi,tumia pesa please pima parternity test,matokeo yake will put this issue to bed.
Hiyo Sheria ndio Inasubiliwa Kuona Ni Wapi Pa Kuanzia na Kumalizia pia..
 
Aachane na mtoto aombe miamala yake yote ya simu ilipwe na hao wazinifu wawili,pia adai matunzo yoote ya kumtunza hayawani
Haki Ya Kupata Miamala Ya simu Anaipataje Hapo Ndipo Msaada wa kisheria Unapohitajika
 
Haki Ya Kupata Miamala Ya simu Anaipataje Hapo Ndipo Msaada wa kisheria Unapohitajika
si miamala inaanzia kwenye simu yake kwenda kwa huyo mwanamke?yye aombe voda miamala yake sio ya mkewe,huwezi kunyimwa miamala yako,ukimaliza unadai chako kwa kutunza kima wa mtu
 
Hakuna kwenda kupima DNA kama hajatokea mwanaume wa kudai kuwa yule mtoto ni wake. ...na isitoshe alimuoa mwanamke wkt hana mtoto wala mimba.
Akamfungulie kesi ya kubadili jina la mtoto bila idhini yake na kumnyima kumwona mtoto wkt anatoa matunzo toka mtoto kazaliwa then kama DNA basi aombe aitwe huyo mwanamme anayesemwa ni baba wa mtoto ili wakafanye wote DNA. .....ikiwa mtoto ataonekana sio wake basi awafungulie kesi ya madai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake bhana ni ngumu sana kuwaelewa....
 
Hiyo Sheria ndio Inasubiliwa Kuona Ni Wapi Pa Kuanzia na Kumalizia pia..
no wasikucheleweshe omba mahakama itoe amri ya kupata bold sample ya mtoto na mama yako then unganisha na ya kwako,naamini laboratories nyingi zinatoa hii huduma,kama no tuma Nairobi,Kenya wanazo hizi lab ila lazima upate ushauri wa kitaalamu jinsi ya kuhifadhi hizi blood samples zisije haribika wakati wa usafirishaji.Good luck
 
Nashukuru Kwa Ushauri Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…