Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
Mimi ni mfanyabiasha wa nyumba za kupanga mkoani arusha. Hoja yangu ni kuwa mpangaji mmoja anataka nimpe mkataba ambao haujawekwa saini ya mwenye nyumba na mpangaji. Mpangaji huyu anadai huo mkataba atapeleka kwa bosi wake ili apewe kodi ya kulipia pango kabla kodi yake haijaisha. Nilipomuambia kwanini asipeleke mkataba ambao tumeshasaini akasema inahitajika mkataba ambao haujajazwa chochote je kisheri hii ikoje? Je nikimpa mkataba ambao haujasainiwa si anaweza kunichezea mchezo mchafu? Nawasilisha.