Wanasheria tupeni uchambuzi kesi ya Sabaya

Wanasheria tupeni uchambuzi kesi ya Sabaya

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Wakuu,

Watanzania wengi kwa sasa hawaelewi kitu gani kinaendelea kuhusiana kesi ya aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai.

Hivi wanasheria wasomi ndani ya nchi hii hamuoni missing gap hapa kwa wananchi wa kawaida?

Sisi Watanzania tunahitaji uchambuzi na ufananuzi zaidi kuhusiana na scenario ya kesi hii
 
Kesi iko wazi mno na haina complications za kisheria. Mtuhumiwa no 1 kaanza kujitetea kwa kutaja high profile figures kea majina na vyeo vyao, kimsingi ni kama kawataja kama washirika wake!

Kama mahakama isipopuuza huu utetezi watajwa wataitwa mbele ya mahakama kuthibitisha ama kukanusha kwamba alitumwa na kayafa nao walikuwa na taarifa kamili, tena wafanye hivyo kwa ushahidi kamili hasa kama watakanusha
 
Uko sahihi mkuu
 
Kwanini kesi ya sabaya inasomwa kila siku? Au kwasabu ni ya UJAMBAZI wa KUTUMIA SILAHA?
 
Miaka 30 hapo wananchi wawapi hao wasiojua hukumu ya kuiba kwa kutumia siraha.
 
Kesi ya msingi inayomkabili ni unyang'anyi wa kutumia silaha.

Sasa utetezi kua alitumwa na mamlaka hautoshi kisheria kuhalalisha kosa alilotenda, endapo upande wa mashtaka ukiweza kuthibitisha uhalifu wa mtuhumiwa.
 
Kwa namna kesi ya jambazi sabaya inakoelekea,inafanya kesi ya gaidi mbowe kutosikika kabisa.

Lakini nyumbu waendelee kushangilia jambazi akijitetea maana ndio furaha waliyobaki nayo,huku bibie akendelea kuipiga mbungi ya kujaza nusu uwanja.
 
Kesi ya msingi inayomkabili ni unyang'anyi wa kutumia silaha.
Sasa utetezi kua alitumwa na mamlaka hautoshi kisheria kuhalalisha kosa alilotenda, endapo upande wa mashtaka ukiweza kuthibitisha uhalifu wa mtuhumiwa.
Inabidi aithibitishie mahakama kuwa alilazimishwa na mamlaka kufanya vitendo vya uhalifu katika hiyo operesheni., Na kwamba kwa wakati huo hakuwa na akili timamu ya kutambua Jema na baya!!
 
Nina mpango wa kufungua kesi dhidi ya PAUL MAKONDA
 
Inaonyesha kuwa kwenye fani ya sheria kuna mawakili wasomi na makanjanja?

Njia gani inatumika kuwabaini hawa 🤔
 
Kwa akili yako jinsi inavyokutuma, kuna ‘mwanasheria’ asiye ‘msomi’? , nauliza tu...
 
Back
Top Bottom