Wanasheria tusaidieni, tumeshitakiwa kwa kutengenezewa kesi

Wanasheria tusaidieni, tumeshitakiwa kwa kutengenezewa kesi

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
192
Reaction score
23
Familia yetu Baba, mama, mimi na wadogozangu wawili tumefunguliwa mashitaka katika mahakama ya mwanzo na tayari tumepokea samasi kufika mahakamani hapo tarehe 10 mwezi huu.

HISTORIA YA MGOGORO


1. Baba yetu amekuwa na mgogoro wa Ardhi (kiwanja) na jirani yetu kwa muda mrefu sana.

2. 2008 Baba yetu alimshitaki huyo mzee jirani yetu kuvunja uzio na kuingia kwenye kiwanja chake baba akashinda katika Baraza la Kata.

3. Huyo mzee jirani akakata rufaa wilayani Baraza la Ardhi akashindwa pia. Baba akashinda.

4. Akakata rufaa nyingine Mahakama kuu kitengo cha ardhi, Jaji akagundua makosa katika hukumu ile hakuamua mshindi ni nani akatoa amri kesi hiyo ikasikilizwe upya chini ya mwenyekiti mwingine asiwe yule ambaye alimpa ushindi baba. Sababu ya jaji kuirudisha wilayani ni kwamba mwenyekiti aliandika katika hukumu yake kuwa wazee wa baraza walikubaliana na hukumu ya kata na kutoa maoni yao kuwa mshindi ni baba, lakini kwenye hukumu hapakuwa na maoni yoyote yaliyoandikwa kuthibitisha alivyosema katika hukumu. Hivyo ikaonekana kama kaiamua yeye kama yeye sio jopo la yeye na wazee wa baraza, kwamba hakuwatendea haki pande zote mbili.

5. Ilivyosikilizwa upya, huyo mkata rufaa jirani yetu amemshinda baba.

6. Baba ameomba rufaa mahakama kuu amepewa samasi kumwita huyo mzee jirani kufika mahakamani mwezi wa tano.

7. Wanae wa huyo mzee jirani baada ya ushindi wa mzee wao wakavamia eneo la mgogoro wakavunja uzio na kupanda mahindi na maharage upande mmoja. Na upande wetu tukapanda upande mwingine kwa kuridhika kutofanya vurugu kwa kuwa Rufaa imeombwa tusubiri mahakama iamue tusifanye fujo kwa uvamizi wao.

8. Huyo jirani ameibuka na samasi kutoka mahakama ya mwanzo na hati ya amri ya kizuizi cha baraza la ardhi la wilaya akidai tumedharau amri halali ya Baraza.

9. Baba anashangaa kuona hati hiyo huku akisema hajawahi kuambiwa hata kwa mdomo na Mwenyekiti wa baraza au mtu yeyote barazani kuwa anazuiliwa kufanya kitu eneo la mgogoro ambalo kuna machungwa aliyopanda, mapera na migomba kwa zaidi ya miaka (30) thelathini iliyopita. Anadai ana uhakika M/kiti na huyo jirani wamemtega kwa kuwa alihofia uendeshaji wa kesi wa m/kiti akamripoti TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA kitu kilichozua uhasama wa baba na mwenyekiti huyo aliyediriki kumtishia kwa maneno makali Baba pale barazani kuwa ataona nani zaidi kati ya mwenyekiti wa TUME na yeye. Kwamba wametengeneza kizuizi hicho kisiri siri wamtie hatiani.

10. Tumeshitakiwa Baba, mama, mimi na wadogo zangu wawili (jumla watano) kisa eti tumepanda mahindi na maharage ,huwa tuna chuma machungwa, tunavuna ndizi, tunafyeka nyasi nk kwenye eneo lenye kizuizi cha mahakama. Tunajiuliza maswali

(a) Kizuizi kinazuia upande mmoja mwingine unaruhusiwa kufanya kazi eneo lenye mgogoro?
(b) Kizuizi kinatolewa kwa siri sio wazi na kwa nini anapewa huyo jirani yetu baba hatarifiwi akapewa na yeye?
(c) Kizuizi hicho cha Baraza la wilaya kina nguvu wakati Baba amekata rufaa na imepokelewa Mahakama Kuu?
(d)Tufanyeje siku tukifika mahakama ya mwanzo kama njia ya kujitetea?
(e) Mtu akipatikana na hatia hiyo ya kukiuka amri ya baraza adhabu yake/zake ni zipi?

Ndugu wanasheria tunaomba msaada wenu.
 
Hii kesi sio ile iliotokaga mkoani kigoma...baadae mkaenda mahakama ya wilaya kasulu lakini hakimu akaikataa...?? Kama sio hii samahani...!!
 
Hii kesi sio ile iliotokaga mkoani kigoma...baadae mkaenda mahakama ya wilaya kasulu lakini hakimu akaikataa...?? Kama sio hii samahani...!!

Sio hiyo mkuu! Niisemayo mimi ni nyingine ilivotoka Kasulu haijawahirudi Kasulu iko mbele High Court Tabora hatua ya rufaa kama nilivoeleza hapo juu.
 
Ndugu wana JF
Wiki moja iliyopita niliomba msaada wa kisheria sijapata hata kidogo! Kwa ufupi ni kwamba baba yangu mzazi amekuwa na kesi ya kiwanja na mzee mwenzie kwa muda mrefu. Hivi karibuni hukumu ikatolewa kuwa baba yangu ameshindwa kutokana na rufaa aliyokata mzee mwenzie (jirani) aliyepinga uamuzi wa Baraza la Kata ambao awali ulimpa ushindi baba.

Ajabu ni kwamba wakati mwezi wa tano 2014 baba atakuwa Tabora na mzee mwenzie kwa hatua ya rufaa aliyoomba baba kwa kutoridhika na uamuzi wa baraza la wilaya, huyo jirani yetu ameibuka na HATI ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ikiwa ni amri inayosemekana ilitolewa tangu mwaka jana 2013 kesi ilipokuwa ikiendelea na kutushitaki Mimi, Baba, mama na wadogo zangu wawili.

Tunashitakiwa katika mahakama ya mwanzo eti tumedharau amri halali ya Baraza. Na tulipojaribu kudadisi ni vipi tumeikiua na kuidharau amri hiyo tuliambiwa na jirani huyo kuwa hatupaswi kufyeka nyasi, kuchuma machungwa (baadhi ya miti ya matunda yana 40yrs) katika eneo hilo alipanda baba, wala hatupaswi kuteka maji kwenye bomba baba aliloweka eneo hilo mwaka 1984 kwamba kwa kufanya hivyo tunakiuka amri hiyo.

Tulijaribu kumuuliza baba ikiwa anahabari na kizuizi hicho alijibu kuwa hajawahi kumsikia mwenyekiti wa Baraza kwa maneno au maandishi akitoa amri hiyo. "...sijawahi kuambiwa hata siku moja..... iweje nakala apewe mmoja wetu mimi nisipewe?.....mbona yeye upande mmoja wa eneo hilo hilo la mgogoro amepanda mahindi na maharage?....

MASWALI MNISAIDIE MAJIBU

1. Ni taratibu zipi hufuatwa hatua kwa hatua mpaka both parties kupokea nakala?

2. Je kuna uhalali gani kutushitaki Mimi, Mama, na wadogo zangu wawili?

3. Ni adhabu zipi/ ipi hutolewa ikiwa mtu atakutwa na hatia mahakamani amedharau Amri hiyo?

4. Siku ya kusomewa shitaka kwanza tutakanusha siku ya utetezi tujitetee vipi?

Ndugu wanajf wanasheria wa jukwaa la sheria naomba msaada wenu niwasilishe kwa wenzangu.

Asanteni sana
 
Tafuteni wakil
..bila pesa kidogo za kumlipa wakili binafsi mtadhurumiwa haki yenu na hamtakuwa na la kufanya. Poleni sana...pia kusanyeni mashahidi, wale watu wanaomfahamu baba yenu km mmiliki halali, majirani zake n.k....tatu unaweza kwenda kwenye baraza la dini anakoabudia mzee wenu mpewe barua ya kuunga mkono uhalali wa hiyo mali yenu, itaongeza nguvu kwenye ushahidi wenu. Mwisho kabisa oneni huo nanyi ni mtihani wenu, kama vile wengine walivyo na mitihani mbalimbali kam vile magonjwa hospitali, ajali, vita nk
 
Back
Top Bottom