Haya ni maswali ya story za vijiweni haya! Ila kukuelimisha ni hivi: Anapotoka kama amemwona yule mtu aliyedhaniwa kuwa aliuawa inatakiwa yeye afungue kesi ili Jamhuri imlipe fidia kwa muda aliopoteza akiwa jela bila kosa! Na kama uvumilivu utamshinda na akiamua kujichukulia sheria mkononi basi atakamatwa tena na atafanyiwa kesi mpya ya mauaji japo kwenye hukumu ya pili anaweza kupunguziwa adhabu kulingana na mazingira aliyotenda kosa! Hiyo itategemea mazingira ya kuua.
Marekani imehatokea mara nyingi watu wakatumikia jela miaka zaidi ya ishirini na baadae ikaja kuonekana kumbe hawakuwa na hatia. Wengi walilipwa fidia kubwa na serikali.