Wanasheria ufafanuzi hapa Tafadhali.

Wanasheria ufafanuzi hapa Tafadhali.

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,646
Naomba kupewa ufafanuzi ndugu zangu mliobobea katika masuala haya ya Sheria,hivi askari anapokuwa katumwa katika operesheni fulani kwa ajili ya kudhibiti amani lakini ikatokea akajifyatua na kufanya kazi hiyo kwa kufuata miongozo yake hadi kufikia kutenda kosa la jinai mfano kuua,kutia kilema(kujeruhi) n.k je sheria inasemaje??je anaweza kushtakiwa?Je ni nani hasa mwenye jukumu la kufungulia kesi?
Tafadhali naomba msaada wenu wataalam kwa kina zaidi.
 
Kama makosa kama hayo ulotaja hio ni jinai...jamhuri inahusika hapo

Rejea Kesi ya Daudi Mwangosi (Aliyekuwa Mwandishi wa Channel ten Iringa) na hata kesi ya Abdallah Zombe japo kwa upande wa kesi hii waliachiwa huru ..kesi zinazoendana na suala ulouliza
 
Naomba kupewa ufafanuzi ndugu zangu mliobobea katika masuala haya ya Sheria,hivi askari anapokuwa katumwa katika operesheni fulani kwa ajili ya kudhibiti amani lakini ikatokea akajifyatua na kufanya kazi hiyo kwa kufuata miongozo yake hadi kufikia kutenda kosa la jinai mfano kuua,kutia kilema(kujeruhi) n.k je sheria inasemaje??je anaweza kushtakiwa?Je ni nani hasa mwenye jukumu la kufungulia kesi?
Tafadhali naomba msaada wenu wataalam kwa kina zaidi.
Kimsingi na kisheria hapo kuna kesi mbili, ya jinai na madai.

Kesi ya madai anaweza shitaki yeye muathirika kama amejeruhiwa, ila kama amefariki basi ndugu ama wawakilishi wake wa kisheria wanaweza shitaki serikali kwa niaba ya marehemu na jinai ni maslahi ya jamuhuri serikali inawashitaki wale waliotenda kosa.

Mfano mzuri wa hili ni kesi maarufu ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa wakati huo, IMRAN KOMBE ambapo kulikuwa na jinai na madai.
 
Kuna Mahakama ya kijeshi pia!
Hii ni kwa wanajeshi,Sasa inategemea na askari gani unamuongelea!
 
Back
Top Bottom