kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Katika suala la kukodisha bandari zetu tujifunze kitu kimoja kikubwa. Kwamba taaluma ya sheria inapotumiwa na mafisadi ni hatari kama ukoma kwenye jamii.
Siku moja tu imepita tumewasikia wanasheria wizara ya ujenzi na uchukuzi wakiwa na waziri wao wakijaribu kutetea uamuzi wa serikali kutaka kuipa falme ya dubai usimamizi na uendeshaji bandari zetu zote kuanzia bahari, maziwa na mito. Na pia kuwapa miundombinu yote inayohusika na utendaji wa bandari hizo kuzisimamia. Uamuzi kama huo bila shaka unatikisa uhuru wa nchi yoyote. Na kwa kuanzia eti watafanya makubaliano na kampuni mali ya mfalme wa dubai kuanza kuendesha bandari ya dar es Salaam.
Nalotaka kuonesha hapa ni jinsi wanasheria wa wizara walivyotetea usiri wa majadiliano yao hadi makubaliano ya kuiteua kampuni ya DPworld huku tayari nchi ikiwa imeshaingia mkataba kukabidhi shughuli zake zote za bandari kwa dubai.
Wanasheria hao wanadai eti washindania wa ksndarasi ndio wanaotaka usiri bila kuelewa kwamba wananchi na jamii inataka uwazi. Nia ya kushindanisha kampuni ni ili kila moja itoe bei yake halisi kufuatana na gharama zake na sio kama kucheza kamari kubahatisha nani anaweza kumpiga bei ya juu kabisa mteja.
Licha katika nadharia ya ubepari dhana ya kwanza kua ndio sahihi lakini ukweli dhana ya pili kucheza kamari ili kumpiga mteja ndio inatumika. Hapo ndio makampuni yanataka usiri na kutumia mbinu chafu za kila aina wakati umma unataka uwazi ili yule mwenye weledi na teknolojia kuweza kutoa ofa ya bei ya chini ndio ashinde kandarasi.
Jambo la kushangaza ni jinsi wanasheria wa wizara walivyoweza kutetea matakwa ya wakandarasi kudai kataka usiri na kuona madai ya umma kutaka uwazi kama sio sahihi. Hapo ndio tunaona shida na hatari nchi kubebeshwa kupewa huduma kwa gharama kubwa ambazo pengine wala sio mahitaji yake ils ni kutokana na vishawishi tu vya biashara za kimataifa kutafuta soko.
Baadhi ya wanasheria wa wizara ambao nadra kuonekana mbele ya umma walionekana kua na siha njema sana hadi kimoyoni mtu kuweza kuhoji vipato vyao kama ni mishahara na marupurupu ya kikazi pekee.