Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
nawaonea huruma waandishi wa ipp media......itv,radio one, guardian nipashe, na mengine katiak hayo.....wako kama dolls...vikaragosi....wanaandika na kumsifia bosi wao tuuuu anachopanga yeyey ndicho hicho....hawana tena uhuru wa kusema...wanaendeshwa kama pia...tena namuonea huruma ndugu yangu...sakina datoo amesoma lakini mhhhh anajidhalilisha pale ipp media.....ukweli mnaendeshwa kama pia ...ni puppets....mnaharibu taaluma yenu....amkeni.....hiii ni taaluma yenye heshma lakini munapoendesha programme zenu kwa shindikizo la mengi...basi mujue mnajidhalilisha... Na wala hamuendelei kitaaluma na kifikra....angalieni wenzenu wa ntv, ktv,citizen, hata kbc za kenya muige mfano wao....kuweni na uhuru wa fikra na mawazo musikubali kuwa watumwa wa hayo....
 
majibu

kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani

je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?
Anakopa akitakiwa kurudisha anakimbilia vyombo vya habari.ndo chanzo ugomvi wake na mawaziri mbalimbali hukumsikia RA.Hivi mengi anafanya biashara gani za kumuwezesha kila kukicha kutoa misaada.Hizo pesa za mafuta au......
 
Haya ndiyo matatizo ya kuwa na uongozi dhaifu ambao unashindwa kushughulikia watu waovu na badala yake wananchi wanaokerwa na hali halisi ya ufisadi ndiyo wanakuwa mstari wa mbele kupambana na hali ambayo hairidhishi. Kikwete yeye hahusiki, angependa sana kuona kasheshe hii inakwisha haraka sana ili aanze kampeni zake za 2010, lakini hili linamgusa kwa karibu mno na amezembea na sasa linazidi kuwa kubwa. Hongera Mengi na Dr Slaa Watanzania wengi tuko bega kwa bega nanyi katika mapambano dhidi ya mapapa mafisadi. Tanzania isiyo na mafisadi INAWEZEKANA kabisa just play your part. We need a new President ni 2010 ambaye hatawekwa mifukoni mwa mafisadi na hivyo kuwa huru katika utendaji wa kazi zake kama Rais wa Tanzania bila kumuogopa yeyote yule. Kikwete hatufai kabisa kama Kiongozi wa nchi yetu.
 
Wewe MACOS acha ujinga. Hapa sio suala la waandishi wa IPP wala nini! Ni suala la ukombozi wa nchi hii inayotawaliwa na Magabacholi. Wewe MACOS sidhani hata kama mama yako mzazi anajua atakula nini mlo unaofuata. Ni kwa sababu hawa mafisadi wamhamisha kila kitu kupeleka makwao. Hao hapa sio kwao ndio maana hawana huruma na sisi. Nahisi wewe ni mwandishi wa fisadi papa Rostam Aziz. Moto aliouwasha Mengi ni mkali na unaashiria mwisho wa mafisadi, hasa Magabacholi na huyo Muajemi Rostam Aziz. Amka ndugu yangu, fikiria mustakabali wa nchi yetu kama wezi hawa wataachwa hivi hivi. Hao waandishi wa IPP ni wapiganaji kama alivyo mwajiri wao Mengi. Wengi wao nawafahamu wana uwezo mkubwa! Na sasa wamechokozwa, hebu sikilizia makombora yatakayorushwa!
 
nawaonea huruma waandishi wa ipp media......itv,radio one, guardian nipashe, na mengine katiak hayo.....wako kama dolls...vikaragosi....wanaandika na kumsifia bosi wao tuuuu anachopanga yeyey ndicho hicho....hawana tena uhuru wa kusema...wanaendeshwa kama pia...tena namuonea huruma ndugu yangu...sakina datoo amesoma lakini mhhhh anajidhalilisha pale ipp media.....ukweli mnaendeshwa kama pia ...ni puppets....mnaharibu taaluma yenu....amkeni.....hiii ni taaluma yenye heshma lakini munapoendesha programme zenu kwa shindikizo la mengi...basi mujue mnajidhalilisha... Na wala hamuendelei kitaaluma na kifikra....angalieni wenzenu wa ntv, ktv,citizen, hata kbc za kenya muige mfano wao....kuweni na uhuru wa fikra na mawazo musikubali kuwa watumwa wa hayo....

Vipi waandishi wa New Habari Corp ya Rostam?
Kama wewe ni msomaji, basi unaona tofauti kati ya Rai ile ya akina Jenerali Ulimwengu na Rai hii ya Rostam.
All in all, tunangojea mambo ya Mahakamani tusikie mambo.
 
Wana-JF naomba nijibiwe: Inakuwaje mtu (mfanyabiashara?) anaishi hapa nchini, anakuwa tajiri mkubwa (bilionea kwa level ya Bongo) lakini hana hata kampuni moja au biashara? Kuna nini hapo jamani?

Kwa nini wengine hawafanyi hivyo? Yeye tu RA ndiye anajulikana kufanya namna hiyo! Hivi TRA, BRELA, na mamlaka zingine husika hazioni kama hili halikai sawsawa?

Kufuatana na press conference yake ya jana, RA hana hata kampuni moja ya kwake -- ambako kuna jina lake Rostam AbdulRasul Aziz -- hana. Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake. Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, New Habari hakuna jina lake! Anafanya nini hapa shughuli inayomfanya kuwa bilionea?

Jana alipoonyeshwa kwamba New habari ilichapisha na kusambaza matoleo mawili ya Rai Alhamisi iliyopita -- yote yenye namba 814 -- aliruka akasema hajui chochote. Magazeti hayo moja lilikuwa linamkandia Mwakyembe, na jingine Reginald mengi -- wote hao mahasimu wake. Anakataa hajui kitu chochote!!!

Watanzania, tusikurupuke kusemasema mabo yasiyo na msingi, hili suala la kuwa na bilionea asiye na biashara yoyote inashtua -- inawezekana labda ni kinara wa unga.
Alisema miaka ya 1800 babu zake waliuza watumwa wakapata fedha nyingi, halafu yeye aliiba EPA na akasema anao kina Sophia Simba, Mkuchika nk serkalini wanomtuma wapi achukue fedha ndio maana alisema alinunua HBC hakwenda hata kuona nini alinunua mpaka kama wiki mbili alipopata habari hakuna anayejua huko kukoje.Huyu ndiye RA aliyewahi kuwa mweka hazina wa CCM kwenda kurekebisha vitabu vya deep green, kagoda, tanggold na meremeta. hili ndio chimbuko la utajiri wake awe na kampuni la nini.
 
Excellently said, rmashauri. I believe mtimti atasoma hii na atajua kwa nini nasimama kidete kusema kuwa NONI ni fisadi. Ziko evidence nyingi sana na si za share 35% za vodacom tu. Kwani Rostam atakubali NONI aende afunguliwe kesi, wakati wa utetezi si atamtaja?? Kwani unafikiri kwa nini Malegesi naye hajapelekwa mahakamani??? Utetezi ake ni tata!!!! Again, mtimti si wote mafisadi watapelekwa mahakamani, watapelekwa tu wale ambao hawana close tie na ssm = Rostam Aziz!!!!

rostam ni fisadi wa kutupwa hilo hakuna mtanzania asiyelijua,lakini nataka nikwambie kitu flani maane,waswahili wanasema kwamba ''ukiwa na ukaribu na ****** basi usishangae na wewe kuitwa ****** hata kama wewe ni basha'',maane unajua jinsi gani kipindi hiki magazeti yapo wazi kuanika vita vya ufisadi?unawajua mwanahalisi wewe?wanangoja nini kumlima noni?NONI ni nani tanzania?ukiniambia kuwa ufisadi wa noni ni kutokana na mazingira ya kazi yake kutokana na amri za wakubwa wake(mkapa na balali)hapo ntakubaliana na wewe lakini ukiniambia kamuuzia hisa rostam hio sio issue kwani ni uamuzi wake nani wa kumuuzia!
 
nawaonea huruma waandishi wa ipp media......itv,radio one, guardian nipashe, na mengine katiak hayo.....wako kama dolls...vikaragosi....wanaandika na kumsifia bosi wao tuuuu anachopanga yeyey ndicho hicho....hawana tena uhuru wa kusema...wanaendeshwa kama pia...tena namuonea huruma ndugu yangu...sakina datoo amesoma lakini mhhhh anajidhalilisha pale ipp media.....ukweli mnaendeshwa kama pia ...ni puppets....mnaharibu taaluma yenu....amkeni.....hiii ni taaluma yenye heshma lakini munapoendesha programme zenu kwa shindikizo la mengi...basi mujue mnajidhalilisha... Na wala hamuendelei kitaaluma na kifikra....angalieni wenzenu wa ntv, ktv,citizen, hata kbc za kenya muige mfano wao....kuweni na uhuru wa fikra na mawazo musikubali kuwa watumwa wa hayo....
Nami nawasikitikia wazembe wa kufikiri ambao hadi muda huu wanaendelea kulamba miguu ya Rostam na mafisadi wenzie,kisa njaa zao.Huu ni utumwa mbaya zaidi kuliko huo unaodai kuwepo kwa waandishi wa IPPMEDIA.Utumwa kwa mafisadi ni psychological rape au kwa lugha ya taifa KUBAKWA KISAIKOLOJIA.
 
Jamani watz tuamke sasa! Tunatarajia nini kutoka kwenye hii serikali ya kifisadi. Waziri wa utawala bora anakurupuka na kuwaita mafisadi ni watu safi! Sijui huyu jk anangoja nini kumtimua! Au tumueleweje?
 
Wewe macos jionee huruma wewe mwenyewe na familia yako kwa ujinga wako wa kukubali kuwa mtumwa wa akina rostam. Hao waandishi wa ipp ni watu makini na walio tayari kwa mapambano, ndio maana hawaogopi chochote. Sijui kama huwa unasoma 'thisday' wewe!
 
Mtimti tuliza boli ndugu yangu inawezekana una mapenzi mema na Noni lakini yumkini humfahamu vizuri. Chukulia mfano huu; Peter Noni ni mmilikiwa kampuni ya Planetel ambayo ni super dealer wa Vodacom na ilikuwa inamiliki share 16 % za Vodacom na sasa ameziuza na hauji ni kwa nini. Sasa jiulize Peter Noni alifanya biashara gani ya kupata mabilioni ya kumiliki 16 % ya VodaCom. Huu ni mfano mdogo ninaoujua. Acha kutukana calm down rafiki yangu.

kaka,hata wewe ukiwa unaweza kuthubutu basi utatoka hapo ulipo,si kila aliefanikiwa basi kafanya ufisadi,mi nnaweza kuwa na mipango mizuri sana na pesa kidogo lakini wewe ukawa na pesa nyingi sana lakini mipango huna basi tukaunganisha mipango yangu na pesa zako tukafanya mambo makubwa...hii sio thread ya noni ukitaka nikupe vingi kafungue thread...ila kifupi ni kuwa planetel ndio waliowaleta vodacom tanzania
 
Wana-JF naomba nijibiwe: Inakuwaje mtu (mfanyabiashara?) anaishi hapa nchini, anakuwa tajiri mkubwa (bilionea kwa level ya Bongo) lakini hana hata kampuni moja au biashara? Kuna nini hapo jamani?

Kufuatana na press conference yake ya jana, RA hana hata kampuni moja ya kwake -- ambako kuna jina lake Rostam AbdulRasul Aziz -- hana. Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake. Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, New Habari hakuna jina lake! Anafanya nini hapa shughuli inayomfanya kuwa bilionea?

Watanzania, tusikurupuke kusemasema mabo yasiyo na msingi, hili suala la kuwa na bilionea asiye na biashara yoyote inashtua -- inawezekana labda ni kinara wa unga.

Ndiyo maana wakati mwingine ni heri kukaa kimya. Rostam AbdulRasul Aziz kaingia mwenyewe kichwa kichwa kwenye mtego wa Mengi na hapo wote waliomo na wasiokuwamo kuna hatari ya mtego kuwanasa. Kasema wazi tena kwa kujitapa kuwa watanzania 6,000 kawaajiri na anawalipa viruzi - je ni kwenye shughuli gani kama Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake, Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, Dowans hakuna jna lake na New Habari hakuna jina lake!

Hapa ndipo panya anapojinasa kwenye tundu maanake anaongezea kwa kusifia alivyo mfanya biashara mwenye rekodi nzuri TRA ya kulipa kodi !! Ni biashara gani hiyo - halafu wengine mnashangaa kwa nini serikali iko kimya na kwa nini mkulu JMK kaumbuliwa na Mengi. Kampuni za Mengi zinajulikana mpaka Rostam anaziorodhesha, lakini zake hata BRELA hawana habari. Mengi hakuwashambulia Wahindi, ameshambulia kichaka cha wezi wanaojificha chini ya CCM na kutanguliza Wahindi. Ameshambulia utaratibu wa kuanzisha kampuni hewa uliobarikiwa na tuliowapa dhamana ya nchi.

Bahati nzuri leo Rostam katusaidia kwa kutufungua macho, asante Mengi !! Tumeweza kujua kuwa kuna biashara zisizo na wenyewe lakini zinaingiza mabilioni, zinakopa benki, zinaingia mikataba na serikali, zinafadhili chaguzi na zinaiba mchana kweupe - nani ashtakiwe ? Zimeweza kufanikiwa kwa kuwa hakuna mwenye ubavu wa kuzigusa - si wana ubia na dola na wanakula pamoja ? Rostamu kauliza ni vipi atajipeleka mwenyewe mahakamani kujishtaki na toka lini serikali ikajishtaki na kwa nani ? Adui mkubwa wa wezi hawa ni yule atakayethubutu kuwanyooshea kidole, Mengi kathubutu.
Mengi kalikoroga, Rostam kalinywa !!​
 
Wewe MACOS acha ujinga. Hapa sio suala la waandishi wa IPP wala nini! Ni suala la ukombozi wa nchi hii inayotawaliwa na Magabacholi. Wewe MACOS sidhani hata kama mama yako mzazi anajua atakula nini mlo unaofuata. Ni kwa sababu hawa mafisadi wamhamisha kila kitu kupeleka makwao. Hao hapa sio kwao ndio maana hawana huruma na sisi. Nahisi wewe ni mwandishi wa fisadi papa Rostam Aziz. Moto aliouwasha Mengi ni mkali na unaashiria mwisho wa mafisadi, hasa Magabacholi na huyo Muajemi Rostam Aziz. Amka ndugu yangu, fikiria mustakabali wa nchi yetu kama wezi hawa wataachwa hivi hivi. Hao waandishi wa IPP ni wapiganaji kama alivyo mwajiri wao Mengi. Wengi wao nawafahamu wana uwezo mkubwa! Na sasa wamechokozwa, hebu sikilizia makombora yatakayorushwa!
 
Ndiyo maana wakati mwingine ni heri kukaa kimya. Rostam AbdulRasul Aziz kaingia mwenyewe kichwa kichwa kwenye mtego wa Mengi na hapo wote waliomo na wasiokuwamo kuna hatari ya mtego kuwanasa. Kasema wazi tena kwa kujitapa kuwa watanzania 6,000 kawaajiri na anawalipa viruzi - je ni kwenye shughuli gani kama Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake, Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, Dowans hakuna jna lake na New Habari hakuna jina lake!

Hapa ndipo panya anapojinasa kwenye tundu maanake anaongezea kwa kusifia alivyo mfanya biashara mwenye rekodi nzuri TRA ya kulipa kodi !! Ni biashara gani hiyo - halafu wengine mnashangaa kwa nini serikali iko kimya na kwa nini mkulu JMK kaumbuliwa na Mengi. Kampuni za Mengi zinajulikana mpaka Rostam anaziorodhesha, lakini zake hata BRELA hawana habari. Mengi hakuwashambulia Wahindi, ameshambulia kichaka cha wezi wanaojificha chini ya CCM na kutanguliza Wahindi. Ameshambulia utaratibu wa kuanzisha kampuni hewa uliobarikiwa na tuliowapa dhamana ya nchi.

Bahati nzuri leo Rostam katusaidia kwa kutufungua macho, asante Mengi !! Tumeweza kujua kuwa kuna biashara zisizo na wenyewe lakini zinaingiza mabilioni, zinakopa benki, zinaingia mikataba na serikali, zinafadhili chaguzi na zinaiba mchana kweupe - nanai ashtakiwe ? Zimeweza kufanikiwa kwa kuwa hakuna mwenye ubavu wa kuzigusa - si wana ushiriki wa dola na wanakula pamoja ? Rostamu kauliza ni vipi atajipeleka mwenyewe mahakamani kujishtaki na toka lini serikali ikajishtaki na kwa nani ? Adui mkubwa wa kichaka hiki ni yule atakayethubutu kuwanyooshea kidole, Mengi kathubutu.

Mengi kalikoroga, Rostam kalinywa !!​

Mkuu nimeona walau niongeze fonti bandiko hili ili lisomeke kwa karibu, Asante sana Mkuu, umeiweka sawia, tupo pamoja. Tundu kaisha ingia, hao watu 6000 kawaajiri wapi? labda watu wa pwani husema maluhani!
 
kaka,hata wewe ukiwa unaweza kuthubutu basi utatoka hapo ulipo,si kila aliefanikiwa basi kafanya ufisadi,mi nnaweza kuwa na mipango mizuri sana na pesa kidogo lakini wewe ukawa na pesa nyingi sana lakini mipango huna basi tukaunganisha mipango yangu na pesa zako tukafanya mambo makubwa...hii sio thread ya noni ukitaka nikupe vingi kafungue thread...ila kifupi ni kuwa planetel ndio waliowaleta vodacom tanzania

Ni kweli rafiki yangu mtimti nafahamu kuwa Planetel ndio waliowaleta VodaCom TZ baada ya lile kampuni walilokuwa wanafanya nalo biashara la Iridium Africa kufilisika maana gharama zao zilikuwa kubwa sana hata Tanzania nakumbuka walikuwa na wateja kama 10 tu. Anyway, basi acha tushie hapa tusiongee sana issue ya Noni maana thread siyo maalum kwake. Nashukuru sana.
 
Mengi endelea Baba tuko nyuma yako na safari hii wahindi mafisadi Papa hawaponi hata wakihujumu maghala ya JWTZ hatuogopi mabomu kwani bora tufe nchi yetu itoke mikononi mwa wahindi wezi(mafisadi papa)
 
Mengi endelea Baba tuko nyuma yako ...

Oohh my my, Utakuwa nyuma yake huku umefumba macho ili akitumbukia shimoni utumbukie nae?

Utakuwa nyuma yake huku hujafumba macho yako ili akitumbukia shimoni urudi ulipotoka?

Nilidhani utamuunga mkono na kumuongoza njia ikibidi; na akianguka umnyanyue.
 
nawaonea huruma waandishi wa ipp media......itv,radio one, guardian nipashe, na mengine katiak hayo.....wako kama dolls...vikaragosi....wanaandika na kumsifia bosi wao tuuuu anachopanga yeyey ndicho hicho....hawana tena uhuru wa kusema...wanaendeshwa kama pia...tena namuonea huruma ndugu yangu...sakina datoo amesoma lakini mhhhh anajidhalilisha pale ipp media.....ukweli mnaendeshwa kama pia ...ni puppets....mnaharibu taaluma yenu....amkeni.....hiii ni taaluma yenye heshma lakini munapoendesha programme zenu kwa shindikizo la mengi...basi mujue mnajidhalilisha... Na wala hamuendelei kitaaluma na kifikra....angalieni wenzenu wa ntv, ktv,citizen, hata kbc za kenya muige mfano wao....kuweni na uhuru wa fikra na mawazo musikubali kuwa watumwa wa hayo....

Wee Balile sijui Manyerere,

Kumbuka kuwa siku Mabwana zenu wakifa, siku ya kifo cha MAFISADI basi na nyie colaborate wao mtakwenda na maji. Heri wa Mengi ambao wanasifu tu na kupata Matapeli kwa data. Ila hao wa RA na kupakazia watu mtakiona cha mtema kuni.

Hivyo anza kujionea HURUMA mwenyewe maana siku ikifika, nyie mtaptiakana kiurahisi maana RA atachukua KIPIPA chake na kwenda zake Kenya kama siyo IRAN. Mwingine nasikia kanunua kabisa YACHT ili aweze kulala mbele mara mambo yakiharibika. Naombea njiani Wasomali wamkamate na kujichukulia Yacht na Mapesa yake. Cha mlevi huliwa na mgema...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom