Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Nilimsikia huyo wakili wa Mengi kwa mbaaaaaaaali akimtaka RA pia atolee maelezo kuhusu fungu la EPA lililoibwa likatumika kwenye uchaguzi 2005 na eti Mangula analijua hilo. Hapa ndio nikahisi kusisimka maana katriga kwa vidole kiunoni mwa CCM. Kwa hatua hii alofikia sifdhani kama Serikali ya JK itaendelea kufumbia maskio vita hii ya maneno kupitia vyombo vya habari iendelee.

Kweli baadhi ya wana wa CCM wanaoitwa machachari walionekana kumuunga mkono MENGI , lakini huko aendako tusishangae CCM ikimgeuka ghafla mara kuskia kanyamazishwa ukimya wa milele. Tukabaki kusema alikuwa... alikuwa....

Eeeh Mungu Mlinde mja wako Mengi atimize lile lilimjaa Moyoni
.

JK hana ubavu wa kufanya lolote maana ufisadi wa papa fisadi RA unamgusa yeye moja kwa moja. Sasa alidhani kwa kukaa kimya ufisadi wa Rostam utasahaulika na yeye aendelee kupeta Ikulu, bahati mbaya alisahau usemi kwamba mdharau mwiba mguu huota tende!!

Sasa mguu umeota tende katika kipindi kibaya sana kwa Kikwete na CCM maana wao walikuwa katika maandalizi ya kujiandaa na uchaguzi wa 2010 sasa huwezi kudance kama una guu lenye tende na unajua fika kwamba mambo atakayoyamwaga Mengi hayamuharibi Kikwete tu bali yanaiharibia CCM katika kinyang'anyiro cha 2010. Najua haya yanayoendelea kati ya Mengi na Mapapa mafisadi yanawatafuna vichwa sana na kuwakosesha usingizi katika anga za juu za serikali na CCM, sijui kama wana namna ya kulizima hili sakata maana Watanzania wengi tunafuatilia kwa karibu mno, na tayari ndani ya serikali na CCM kuna makundi yanayotofautiana kuhusu sakata hili.

Labda ndani ya CCM kuna watu watashtuka na kumuona Kikwete ni liability kubwa kuelekea 2010 kwa kuwa kiongozi dhaifu na kuendelea kwake kuwakumbatia mapapa mafisadi akina Manji, RA, Jeetu, Somaiya, Subhash Patel na wengineo na hivyo kuamua kumtema vinginevyo Wabunge wengi wa CCM 2010 watapigwa chini na kuongeza idadi ya Wabunge toka upinzani kwa kiwango kikubwa sana.

Mwenyezi Mungu walinde mashujaa wa Watanzania katika vita dhidi ya mafisadi, Dr Slaa na R. Mengi

Alutta Continua!
 
Bubu Ataka Kusema,

Mkuu wangu kama ungejua kinachoendelea wala usingefika huko...Kifupi nakuachia endelea kuitazama sinema hii hadi mwisho.. Ni Action, drama na inatisha... Nina hakika umepotea sehemu nyingi sana kwa sababu hadi sasa hivi unamwona 007 akicheza bila kujua kwamba kuna MI6 nyuma ya mission zote..
 
JK hana ubavu wa kufanya lolote maana ufisadi wa papa fisadi RA unamgusa yeye moja kwa moja. Sasa alidhani kwa kukaa kimya ufisadi wa Rostam utasahaulika na yeye aendelee kupeta Ikulu, bahati mbaya alisahau usemi kwamba mdharau mwiba mguu huota tende!!

Sasa mguu umeota tende katika kipindi kibaya sana kwa Kikwete na CCM maana wao walikuwa katika maandalizi ya kujiandaa na uchaguzi wa 2010 sasa huwezi kudance kama una guu lenye tende na unajua fika kwamba mambo atakayoyamwaga Mengi hayamuharibi Kikwete tu bali yanaiharibia CCM katika kinyang'anyiro cha 2010. Najua haya yanayoendelea kati ya Mengi na Mapapa mafisadi yanawatafuna vichwa sana na kuwakosesha usingizi katika anga za juu za serikali na CCM, sijui kama wana namna ya kulizima hili sakata maana Watanzania wengi tunafuatilia kwa karibu mno, na tayari ndani ya serikali na CCM kuna makundi yanayotofautiana kuhusu sakata hili.

Labda ndani ya CCM kuna watu watashtuka na kumuona Kikwete ni liability kubwa kuelekea 2010 kwa kuwa kiongozi dhaifu na kuendelea kwake kuwakumbatia mapapa mafisadi akina Manji, RA, Jeetu, Somaiya, Subhash Patel na wengineo na hivyo kuamua kumtema vinginevyo Wabunge wengi wa CCM 2010 watapigwa chini na kuongeza idadi ya Wabunge toka upinzani kwa kiwango kikubwa sana.

Mwenyezi Mungu walinde mashujaa wa Watanzania katika vita dhidi ya mafisadi, Dr Slaa na R. Mengi

Alutta Continua!

Ukiona mapapa na manyangumi wanagombana wewe kidagaa unashangiria nini?, kaa pembeni na uombe dua asipatikane mshindi maana atakaeshinda atakuwa na njaa sana na atakuja kukula wewe kwa kishindo na hatakuwa na mpinzani hivyo ataamua afanye anavyotaka tu, waache wagombane wamalizane hatimaye bahari itakuwa shwari na sisi vidagaa tutapumua.
 
Inaelekea kwa neno "clearance" una maanisha ushahidi, kama ndivyo O.K. Mimi nilichovutiwa na mawakili wale ni pale waliposema, kuna ushahidi unaonyesha kuwa Rosti Tamu Azizi alikutana na Mkapa na Balali wakajadili akaunti ya Kigoda na inaaminika pesa za Kigoda ndizo zilizomweka madalakani raisi wetu wa sasa. Kama ni hivyo ina maana Mengi anatwanga maji kwenye kinu maana mafisadi washavinjari maeneo nyeti.
 
Kwa hiyo bw Mengi anajikaanga mwenyewe na mafuta yake???
 
Kwa kweli mimi nakubali kabisa kwamba sisi ni waDanganyika.

Ati kwa kuwa Mh. Mengi amelipa hela za Import Support December 2008 na yeye alitakuwa kulipa miaka ya 90... in short amekaa na hela za wananchi for a decade/muongo mmoja hivi... ati sio fisadi nyangumi....

Sasa mbona wale wa EPA waliorudisha hela zetu within deadline ya Mh. Rais wamepelekwa mahakamani?

Hizo hela tulikuwa na makubaliano mengi akae nazo muda wote huo...

Wakati nakubaliana kwamba haikuwa lazima Mengi kupelekwa mahakamani kwa hilo deni la import support, lakini ukweli unabaki sio msafi, hana moral authority ya kuzungumzia mafisadi... aache vita ya ufisadi na JF.
 
best mbona unawatetea sana hawa magabacholi?au tu kwa kuwa ni mengi katoa hizo tuhuma basi hastahili kutoa maoni yake kama mtanzania(mzawa).tatizo la deni l IMPORT SURPOT NA HELA ZA EPA hulijui?(Hasa za rostam) kaka hela za epa ni zile za kagoda ambazo hatujui zilienda wapi(Uchaguzi CCM?????????????) hiyo ndo issue
 
Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.
 
Nyie ndio mnawaponza hawa wazee kwa kukazania jicho kwa jicho.

Mimi nimeangalia conference zote mbili, kwa mawazo yangu RA alijiandaa na kama ni mahakamani ametoa utetezi ambao ni more convincing kuliko Mengi. Watu wa RA walifanya kazi nzuri ya kumwandalia mashambulizi yake.

Mengi awaachie hiyo kazi washauri na wataalamu wake kutayarisha majibu pamoja na documents zote, yeye kazi yake iwe na ku deliver.
Tatizo la mengi hujifanya ana akili hashauriki.watumishi wake hawaruhusiwi kusema chochote isipokuwa ndio bwana.bahati mbaya hata yule mama mkurugenzi wa ITV hawana tofauti na mengi
 
Kwa kweli mimi nakubali kabisa kwamba sisi ni waDanganyika.

Ati kwa kuwa Mh. Mengi amelipa hela za Import Support December 2008 na yeye alitakuwa kulipa miaka ya 90... in short amekaa na hela za wananchi for a decade/muongo mmoja hivi... ati sio fisadi nyangumi....

Sasa mbona wale wa EPA waliorudisha hela zetu within deadline ya Mh. Rais wamepelekwa mahakamani?

Hizo hela tulikuwa na makubaliano mengi akae nazo muda wote huo...

Wakati nakubaliana kwamba haikuwa lazima Mengi kupelekwa mahakamani kwa hilo deni la import support, lakini ukweli unabaki sio msafi, hana moral authority ya kuzungumzia mafisadi... aache vita ya ufisadi na JF.

Mkuu Kasheshe,

Unajua watu kama wewe wenye kuelewa haya mambo lakini mnaamua kutumia haki yenu ya kuwa wavivu wa kufikiri mnatuchelewesha wengine bila sababu yoyote kwenye mapambano haya ya ufisadi.

Zaidi ya hilo, unachelewesha pia wale ambao ni kweli hawana uelewa ulionao wewe.

Mkuu kweli unafanananisha EPA na MIKOPO ya Import Support?
 
Wacha walumbane wajieleze yote halafu vyombo vya dola visiwe na visingizio eti uchunguzi mgumu kama wananchi tunataka wote hao wafikishwe mahakamani.
 
Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Sioni kwa nini umeyachukulia haya serious, kwa kufiria tu utaona kuwa RA ameyataja haya kujazia jazia tu list yake isiyokuwa na credibility.

- Malipo kwa wafanyakazi; amevunja sheria? Kuna vyama vya wafanyakazi vinaweza kuchunguza hilo any day na kutoa statement ya kuishutumu ipp au kuipeleka ipp mahakamani. Hao wafanyakazi wamekuwepo hapo for years leo ndio RA anaona alizungumzie hili?

- Kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi; hao aliogombana nao sio viongozi ni vibaraka wa RA. Hili RA limetumiwa kupoteza lengo, naona amefanikiwa kukupata nalo.

- Kutaka Matatizo yawe ya Kitaifa; Mkuu kweli unaona EPA, Dowans, Richmond, Kagoda sio matatizo ya kitaifa haya?? Zaidi ya hayo kuna CRIME kubwa kuliko zote, kufadhili rushwa kwenye siasa yetu...matatizo hayawezi kuwa ya Kitaifa zaidi ya hapo.

Tafadhali, kwenye hii vita moja ya mbinu za hawa mafisadi ni kupoteza lengo. Tusiwape mwanya huo hata chembe.
 
Mengi hits back, tells Rostam to come clean

main.jpg
IPP Executive Chairman, Reginald Mengi THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

IPP Limited Executive Chairman Reginald Mengi yesterday challenged the Igunga Member of Parliament, Rostam Aziz, to come clean and publicly disclose the number of legitimate businesses that he currently owns.

At a news conference in Dar es Salaam yesterday, lawyers representing Mengi challenged Rostam to respond to widespread allegations that he has interests in at least three companies implicated in massive corruption scandals in the country - Dowans Holdings Limited, Richmond Development Company, and Kagoda Agriculture Trading Company Limited.

’’Let Mr Aziz tell the public in what capacity he was following up on payments for the companies from various banks in the country,’’ IPP Ltd Company Secretary and corporate counsel Agapitus Nguma queried before the packed-to-capacity news conference.

He said apart from disclosing what type of business(es) he is involved in within the country, the Igunga legislator should also make clear in which companies he is legally recognized as a bona fide director by the Business Registration and Licensing Agency (BRELA).

Armed with a loaded briefcase of documentary evidence, Nguma and private advocate Michael Ngalo also sought to dismiss various allegations made by Rostam against the IPP Ltd chief over the weekend.

They described Rostam’s media statement on Sunday as being baseless with no grain of truth, and went on to produce documents to counter each of Rostam’s allegations against Mengi.

Said Ngalo: ’’Honourable Rostam Aziz’s statement was full of personal attacks, which also targeted companies to which Mengi is shareholder. In his statement, Rostam failed to respond to the numerous allegations of graft being levelled against himself.’’

Dealing with the allegations made by the Igunga MP blow-by-blow, Ngalo produced documents to show that Independent Television Limited, Body-Care Limited, Bonite Bottlers Limited, and Anche Mwendu Limited had all repaid their Commodity Import Support (CIS) debts by last year.

’’Neither Reginald Mengi nor any of the companies which he owns have an outstanding CIS debt. All CIS debts have been repaid,’’ Ngalo declared.

According to the documentary evidence availed by the legal counsel, Bonite Bottlers was allocated a 160m/- CIS loan in 1991/92, but utilized only 159.7m/- and repaid over 396.5m/- between October 16, 1992 and April 15, 1994. Several cheques were paid in between the two.

As for ITV and Body-Care, documentary evidence shows that the two companies had an outstanding CIS debt of 852,554,975/- by February last year, which was settled through cheque number 166599202400 issued by IPP Limited from its Standard Chartered Bank account.

A letter to the Ministry of Finance, dated February 6 last year and signed by Nguma on behalf of Mengi, reads in its final paragraph: ’’Please confirm in writing that there is no liability outstanding in respect of CIS for Body-Care Limited and ITV - Independent Television Limited.’’

And a reply letter dated February 14 last year and signed by finance ministry senior official Ms M.N. Ngingite, with reference number TYC/E/450/11/05, states: ’’We would like to take this opportunity to acknowledge with thanks receipt of bank pay-in slip amounting to 852,554,972/45 with NMB Bank House branch, dated February 6, 2008.’’

’’We hereby confirm to you that you have been cleared of all your outstanding balances emanating from utilization of Commodity Import Support facility by your two companies,’’ the ministry’s letter continued.

Responding to Rostam’s allegations that Anche Mwendu defaulted on a 5bn/- debt obtained from National Bank of Commerce Limited, Ngalo said the bank only provided a letter of guarantee facility to enable the company to import a flask manufacturing plant from an Indian firm, JG Vaccum Flasks Limited.

’’The Indian company supplied Anche Mwendu with a different plant - not that used for manufacturing flasks as required. NBC demanded repayment of the debt, but no cash was ever paid, so we went to court where a judge dismissed the case,’’ Ngalo said.

He said High Court judge Thomas Mihayo’s 1993 verdict dismissing NBC’s loan demand to Anche Mwendu for failing to prove that the money was actually paid out, had never been overturned and thus remains valid.

Ngalo was also dismissive of allegations that, as one of the major shareholders of National Investment Company (NICO), Mengi unduly influenced the board of directors to invest in a non-viable company, Interchem Pharma Limited, which is owned by his brother.

The advocate said Mengi, who was chairman of NICO’s investment committee, was never involved in this decision taken by the board of directors, and that when he later became aware of it, he resigned from his position.

A letter dated August 7, 2007, signed by Mengi himself and addressed to NICO Board chairman Felix Mosha, states point-blank his reasons for resigning as being the fact that NICO had decided to invest in Interchem Pharma Limited.

’’This investment was not recommended by the investment committee, because the proposal thereof was not submitted to the committee as it was required. In other words, it was approved by the board without the recommendation of the investment committee, of which I am the chairman,’’ Mengi wrote in the letter, also produced at yesterday’s news conference.
 
Na Boniface Meena
MALUMBANO kati ya wafanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi na Rostam Aziz, yaliendelea jana kufuatia wanasheria wa Mengi, Michael Ngalo na Agapitus Nguma kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Rostam juzi huku wakiacha kujibu hoja nyingine na kuongeza maswali kadhaa waliyodai yanahitaji majibu.

Katika mkutano na waandishi wa habari mwanasheria wa Mengi, Michael Ngalo wa Ngalo & Company Advocates alijibu baadhi ya tuhuma hizo kwa niaba ya Mengi na kudai kuwa wako mbioni kumfungulia kesi Rostam Aziz kutokana na tuhuma hizo wanazodai kuwa ni za uongo.

Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.

Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.

Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.

Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.

Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.

Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.

Hata hivyo Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma alimtaka Rostam kujibu maswali manne, la kwanza, likiwa la kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi, na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.

Hatua hiyo ya Mengi kujibu baadhi ya tuhuma, na kutoa maswali hayo imekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara Rostam Aziz kumlipua Mengi na kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi" baada ya Mengi kumwita yeye na wenzake wanne kuwa ni mafisadi papa.

Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.

Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa Igunga.

Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo hapo mwanzo wakati anawataja mafisadi papa hao na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe.
 
Na Leon Bahati
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema malumbano ya wafanyabiashara yanayoendelea kushika kasi nchini kuhusiana na ufisadi, hayana tija kwa taifa badala yake yanalitoa katika harakati zake ya kukabiliana na changamoto za maendeleo.

Profesa Lipumba alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusiana na kauli ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz aliyemtuhumu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ni ‘nyangumi wa ufisadi'.

Alisema malumbano hayo yanawafanya Watanzania wengi kuacha kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo na kubaki kwenye fitina zinazosambazwa na wafanyabiashara hao.

Aliitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukomesha tabia ya wafanyabiashara kukamiana kupitia vyombo vya habari, kwa lengo la kuwashirikisha wananchi kwenye chuki zao ambazo zinaotesha mbegu za rangi na ukabila, hivyo kutishia amani ya nchi.

"Tanzania ni nchi maskini ingawa tuna rasilimali nyingi. Tumekuwa na tatizo kubwa la kushindwa kujipanga vizuri katika kuzitumia. Kwa jinsi suala hili la ufisadi linavyokwenda, linazidi kutuvuruga," alisema Lipumba na kufafanua: "Mijadala (malumbano) hii inazidi kututoa kwenye mstari."

Hata hivyo, alisema katika maelezo ya Rostam, ambaye pia ni Mbunge wa Igunga, kuna hoja nzito alizozitoa na ambazo zimewafumbua macho Watanzania, hivyo Rais Kikwete hana budi kuzishughulikia kikamilifu.

Alitaja miongoni mambo hayo kuwa ni tuhuma kuwa Mengi alikopa mabilioni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kabla haijabinafsishwa na hakurejesha na vile vile alichukua mabilioni mengine kwenye mfuko unaochangiwa na wahisani; Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (CIS) ambazo pia hakuzirudisha serikalini kama ilivyo utaratibu wa mfuko huo.

Aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuutangazia umma wote waliokopa NBC na CIS na kuwaamuru walipe na kwamba, wachukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa mafisadi wengine waliochota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Profesa Lipumba, alisema kama nyaraka zinazohusu fedha za CIS zitakosekana Hazina, serikali iwasiliane na nchi wahisani wa mfuko huo, kwa sababu wana kumbukumbu za kampuni zote zilizokopa.

Alimtaka Rais Kikwete kuonyesha dhahiri nia yake ya kupambana na ufisadi kwa kutowaonea huruma wafanyabiashara wote wawili ambao kila mmoja anaonekana yuko karibu naye (rais).

Profesa Lipumba alisema anamtambua Rostam kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mengi ni mwanachama wa CCM ambaye amekuwa akijinadi kuwa anamsaidia Rais Kikwete kwenye vita dhidi ya mafisadi; hivyo akasisitiza wote wako karibu na Rais Kikwete.

Alisema fedha za Mfuko wa CIS hutolewa na wahisani ili kuwasaidia wafanyabiashara kuagiza bidhaa nje na hutakiwa kurejeshwa serikalini kwa shughuli nyingine za maendeleo, hivyo kama hazikurudishwa, huo utakuwa ni wizi wa mali ya Watanzania.

Kuhusu EPA, Profesa Lipumba aliendelea kusisitiza kuwa ripoti ya awali ya ukaguzi ilionyesha kampuni ya Kagoda ilighushi nyaraka ili kuzichota hizo fedha, hivyo haoni sababu ya serikali kutowapeleka mahakamani wahusika au wamiliki wake ambao mpaka sasa wanafichwa.
 
Kwa nini Mengi alishindwa kuongea na waandishi wa habari?
Angesimama yeye mwenyewe kuliko kuwatumia hawa wapambe wake naona walichemka tu nilikuwa siwaelewi kabisa nikaamua kuzima TV.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom