Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Mawakili wa Club za mpira tekelezeni wajibu wenu badala ya kulaumu wachambuzi na wachezaji
Na Wakili Zawadi Lupelo
Leo katika pitapita zangu mitandaoni nimekutana na makala fupi ya Mwanasheria wa Club ya Yanga Wakili Simon Patrick akiwalaumu wachambuzi walioshabikia sakata la Feitoto kuvunja mkataba wake na Yanga kuwa ndiyo waliosababisha kile alichokiita changamoto ya wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao.
Binafsi nikiri kauli hii imenishangaza na kunishtua sana, Naam! Imenishtua zaidi kwa kuwa imetoka kwa wakili msomi na mkuu wa idara ya Sheria wa club kubwa ya Yanga. Pengine nisingeshangaa kama kauli hii ingetolewa na Ally Kamwe au hata Wakili kutoka timu ya kengold au Pamba united. Kauli hii kutoka kwa wakili msomi mwandamizi inafikirisha sana.
Inawezekana vipi mwanasheria mwandamizi kuwalaumu wachambuzi katika swala la mikataba ambalo ni swala kisheria? Inashangaza kwa mwanasheria kuwalaumu wachambuzi wasio hata na elimu ya Sheria katika swala la kisheria. Kama Simon Patrick anaamini wachambuzi ndiyo waliosabisha kile anachoita changamoto ya wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao basi atakuwa anaamini pia kuwa wachambuzi ndiyo wenye mamlaka ya kulikomesha swala hilo?. Na kama tatizo limesababishwa na wachambuzi mbona suluhisho analipeleka kwa TFF?
Ni wazi Wakili Simon Patrick anajaribu kukwepa wajibu wake kama wakili wa club. Kama Kuna changamoto ya wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao basi tatizo halisababishwi na wachambuzi bali linasababishwa na mawakili na wanasheria wa vilabu vya Mpira wa miguu kukosa weledi katika kuandaa na kuisuka mikataba baina ya vilabu na wachezaji. Hivyo badala ya Mwanasheria wa Club kubwa kama Yanga kulitupia swala hili ambalo ni la kisheria zaidi kwa wachambuzi alipaswa kupeleka lawama kwa idara za vilabu vyetu vya Mpira wa miguu.
Kwa mfano tatizo la Feitoto na Yanga halikusababishwa na wachambuzi bali lilisababishwa na jinsi mkataba wa Yanga na Feitoto ulivyokuwa umesukwa kiasi cha kumruhusu Feitoto kuvunja mkataba wake kama atarudisha shilingi Milioni 112 za kitanzania. Swali je ni wachambuzi walioandaa huo mkataba na kuweka hicho kipengele kilichotumiwa na Feitoto kuvunja mkataba wake? Je kama mawakili wa Yanga wasingeweka hicho kipengele Feitoto angepata wapi uthubutu wa kuvunja mkataba?
Sina hakika kama Simon Patrick analinganisha sakata la Feitoto na Prince Dube. Sakata la Feitoto na Prince Dube halifanani wakati Feitoto mkataba wake ulikuwa unamruhusu kuvunja mkataba wake kwa kutoa Milioni 112 Prince Dube mkataba wake ulikuwa unamtaka ili avunje mkataba lazima alipwe Dola za kimarekani 300,000/= ambazo ni zaidi ya Milioni 750 za kitanzania. Hapa utaona utofauti wa mawakili wa Azam na mawakili wa Yanga, wakati mawakili wa Yanga wakiweka pesa ya kuvunja mkataba ndogo wenzetu Azam waliweka buyout clause kubwa zaidi hapa mawakili wa Azam Sports Club walifanya kazi yao ipasavyo wakati mawakili wa Yanga walifeli katika kuusuka mkataba wa Feitoto.
Nitashangaa nikikutana na Wakili alieandaa mkataba wa Awesu Awesu na kuweka buyout clause ya Milioni 50 akiwalaumu wachambuzi kuwa wamefanya Awesu Awesu atoroke club yake baada ya kuwalipa KMC Milioni 50.
Buyout clause ni kipengele cha anasa kinachomwezesha mchezaji kujiamria kununua mkataba wake baada ya kulipa kwa club kiasi cha pesa kilichowekwa katika mkataba. Japokuwa anayetakiwa kununua mkataba wake ni mchezaji lakini practically zoezi Hilo hufadhiliwa na timu inayomtaka mchezaji husika. Duniani kote ipo hivyo ndiyo maana nchi za wenzetu wanaweka buyout clause kubwa na mara nyingi inakuwa zaidi hata ya thamani halisi ya mchezaji.
Ukiweza kuweka buyout clause kubwa ina maana mchezaji hawezi kukurupuka tu na kutaka kununua mkataba wake akizingatia kiasi kikubwa cha pesa anachotakiwa kulipa. Hivyo buyout clause itamlazimisha mchezaji kurudi mezani na timu ku negotiate na kuomba apunguziwe ili alipe pesa kidogo mfano ni kilichotokea kwa Dube na Azam. Mara nyingine club inayomtaka mchezaji itaona ni bora ijitokeze iongee na timu inayommiliki mchezaji na kumnunua kuliko kulipa pesa iliyopo kwenye buyout clause.
Pia siyo sawa kulinganisha sakata la Feitoto na Kibu kwa sababu sakata la Kibu ndiyo kwanza linaanza bado hajaomba kuvunja mkataba Wala hajalipa buyout clause amount kama Feitoto hivyo sakata la Kibu Dennis utatuzi wake pia itategemea zaidi mkataba wake unataka Nini.
Sakata la Feitoto linafanana na Sakata la Dube na KMC isipokuwa tu tofauti ni kwamba Mawakili wa Azam walifanikiwa katika kuusuka vyema mkataba wao na Dube tofauti na mawakili wa Yanga na KMC ambao walifeli na kusababisha club zao kupata hasara.
Badala ya mawakili na viongozi wa vilabu kulaumu wachambuzi walioshabikia sakata la Feitoto wajitafakari wao je wametekeleza wajibu wao ipasavyo? Je mawakili wa Timu zetu wanatimiza wajibu wao wakati wa kuisuka hii mikataba yao na wachezaji?
Maswala ya mikataba ya wachezaji ni maswala ya kisheria hivyo ni aubu sana wanasheria kuwalaumu wachambuzi watu ambao hawana elimu ya kisheria katika mambo ya kisheria kama anavyofanya wakili wa Yanga.
Wakatabahu.
Zawadi B Lupelo Esq