Wanasheria wa Vilabu vya Soka Tanzania fanyeni wajibu wenu, msilaumu wachambuzi

Serikali haikuingilia maamuzi ya TFF, Rais kwa hekima zake alishauri Yanga mmalizane na Feitoto, ilikuwa ni ushauri tu Yanga ingeweza kupuuza na kuendelea na kesi kule CAS.

Yanga kwa kutambua kuwa wakipuuza huenda ombi lao la uwanja lisingekubaliwa wakatumia nao busara na kumalizana na Feitoto.

Nikija kwenye hoja ya mauzo ya Feisal siyo kweli kwamba Feitoto mauzo yake yalifika hiyo mil 500+ na hiyo hesabu ya kupigia kuongezewa uwanja Haina uhalisia, kwani uwanja haujatoka Azam ni serikali imewapa kwani Feisal Salum anaenda kucheza timu ya Serikali ili muingize uwanja kama sehemu ya consideration au price ya Feitoto? Kwani kusingekuwa na mgogoro wa Feitoto Yanga isingeomba uwanja kwa serikali? Na je wasingepewa?
 
TFF si ilisema Fei ni mchezaji halali wa Yanga,mara tatu yale ni maamuzi ya chombo kinacho tambulika na FIFA chini ya Rais Karia ndio maana kiongozi yoyote wa serikali haruhusiwi kuingilia maamuzi ya chombo kinacho tambulika na FIFA.......

Haya mbona walishindwa kwenda CAS hao wakina Fei na Yanga walishinda mara tatu TFF,kitu gani kilicho wazuia wanasheria wa Fei kwenda CAS.....? Au unazani Wanasheria wa Fei walikiwa wajinga kama wewe,......... walikuwa wanajua wanachoenda kukutana nacho CAS.

Halafu tokea lini mpira ukaendeshwa na hekima na busara za rais? Huu mpira wenu na ndio maana leo kila mchezaji anajiamulia.Mpira unasimamiwa na kanuni zinazo ongoza mpira ambazo zipo chini ya FIFA ambazo zinatafsiriwa na Mwanasheria, sio mchambuzi.

Sawa uwanja haujatoka Azam,ila si umepatika kupitia swala la Fei........

Tushukuru FIFA hawa kulisikia hili kwani tungeishia humu humu kucheza NBC league,Mapinduzi na CRB Confederation na wachezaji wasingecheza mashindano yoyote yale.
 
Nitakuwa mwehu kama wewe nisipolaumu the so called wachwambuzi. Hao binadamu ni vichomi na Hakuna wanajua zaidi ya kufanya ushabiki kuwa uchambuzi.
 
Ishu ya Feitoto ni aibu hata kuiongelea kisheria maana maamuzi yametolewa kisiasa.

How comes useme kua wanasheria wa Yanga walizembea ilhali maamuzi ya mwisho hayajathibitisha hilo??
Utajuaje maamuzi ya wanasheria wa Yanga ni hovyo wakati bado walikua wanapambania kuuelewesha umma kupitia sheria kua huo mkataba unaosema ni wa hovyo wao waliona si wa hovyo.

TFF waliona wapo sahihi, wewe unasema TFF hawakua sahihi, mpaka hapa ni wanasheria wa yanga 1 Fei 0. Fei akachangiwa pesa aende mbele zaidi lakina hapo kati ndo raisi akamria hilo, hapo bado wanasheria wa Yanga walikua sahihi.
 
Tatizo ukiwa shabiki wa yanga huwezi kuwa na akili hata ukiwa na PhD.

Hilo ni kwa wote viongozi,mashabiki na wachambuzi wenye mapenzi na timu.
 
Nani kapoteana?Shida zenu ninyi mashabiki wa yanga hamna akili.Hakuna shabiki wa Simba anayebabaika na Kibu.
Na akiomba kuindoka ataruhusiwa na siyo afanye ujinga halafu Simba isuse!
Kama una akili utaelewa ila ndio hivyo tena
 
Tatizo unaongea na vichwa mbuzi wanajua kula nyasi tu,hawatakuelewa.Wakili wao msomi ndio kwanza anaandika ujinga,unadhani mashabiki watakuwaje?
 
Kwa utafiti wako suala la Feitoto lilihitimishwa kisheria na wanasheria!?
Hoja ya Simon Patrick ni kwamba kuna nguvu iko nje inatumika visivyo kuwaoa wachezaji kiburi cha kuzigeuka timu zao. Na hiyo nguvu ina nguvu mno ndio maana Rais alipoingilia kati suala la Feitoto hata hao wachambuzi hakuna aliyesema wazi kuwa uamuzi ule ulivunja sheria na taratibu za soka.
Ngoja hali iendelee kuwa hivi baadae huko wachezaji wenyewe watajitojeza kuomba haya mambo yawekwe sawa.

Matajiri wametulia tu kwa sasa wanaangalia game inavyochezwa na hawa vijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…