Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Sio kwa nia mbaya lakini ni kuwa na jicho critical kidogo, nauliza tu "wanasheria wetu wa kizazi hiki wana viwango?" kwa nini kama nchi kila kesi kule nje kwa wakoloni tunashindwa na kulipa mabilioni ya walipa kodi kiroho safi tu? Tuna maprofesa wa sheria wanapoongea hadi wanatoa macho yanataka kuanguka, wanashindwaje kuwakilisha nchi ya baba na mama zao kuokoa haya mapesa? Tuna wanasheria wanajiita wazalendo kupindukia, wametusaidia nini? Wanasheria wetu wanaona kilio kikubwa cha jamii kuhusu uonevu na kuporwa kwa haki ya kuishi, ya uongozi, ya huduma mbalimbali, nk, hawaoni hiki kilio, wanataka nani abebe jukumu la kutetea haki za jamii zao? Wanalalamika tu kama raia wengine hii ni sawa? Wanaona mfumo wa haki ulivyojaa rushwa na wakati mwingine wemetumika kudhulumu haki kwa kushikiana rushwa na majaji na mahakimu ikiwa ni pamoja na kupanga hukumu ili tu wapate maslahi ya kifedha (allergedly).
Imefikia hata wao wenyewe hawaaminiani, the case ya Mh. Adv. Lissu kumlipa Amsterdam amtetee hamna watanzania mahiri wa kutetea wateja kwa kesi za kimataifa?, hamna wanasheria wenye kuweza kushindana kimataifa? Wananchi tuende wapi? Tuendelee kuwaamini? Au uwezo wao hauvuki mipaka? Tumeona madaktari, manesi, wanasayansi wakifanya kazi katika nchi zilizoendelea na kuwa na umahiri unaolingana au unazidi hata wakoloni ndani ya nchi zao, why not wanasheria?
Naomba kuelewa wanabodi kama mtanzania mwenzenu na najua wazee wetu wametusomesha kwa shida kubwa na kufanya investments zao za time na mali lakini tunawalipa nini? Rushwa au umahiri?