Wanasiasa acheni kujifanya Njiwa ilihali ni Tai

Wanasiasa acheni kujifanya Njiwa ilihali ni Tai

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
495
Reaction score
708
Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuna watu wengi wametia nia ya kugombea nafasi mbalimbali.

Wapo walioanza harakati za kuwashawishi wajumbe kwa kutumia njia mbalimbali hasa fedha ili majina yao yapitishwe. Wapo pia wanaochangia miradi ya jamii katika majimbo wanayotarajia kugombea.

Wengine wametengeneza makundi ya machawa wao wanaoposti kila mtu wao analolifanya ili kupata uungwaji mkono. Kilichonileta hapa si hicho, bali napenda kuwakumbusha watia nia hasa wale wenye ukwasi na wameajiri watanzania wasakatonge kwenye kampuni zao, kabla hawajatapanya pesa zao kwa ajili ya kutafuta uungwaji mkono, wawakumbuke na wafanyakazi wao wanaowaletea hizo fedha wanazochezea.

Kuna watia nia kwenye moja ya majimbo ya mkoa wa Morogoro kwa tiketi ya chama tawala, wapo active sana kwenye uchangiaji wa shughuli za kijamii lakini wafanyakazi wa kampuni zao hawajalipwa mishahara yao tangu mwezi Januari.

Watu wanateseka na familia zao tangu mwaka uanze kwa sababu pesa zao waajiri wao wanahonga machawa na wajumbe wa chama chao cha CCM, wanajifanya kujitolea kusomesha watoto yatima, kuchangia ujenzi wa majengo ya huduma kwa jamii kama shule na madrasa, huku lengo lao likiwa ni kupata uungwaji mkono katika harakati zao za kugombea ubunge. Wasiojua mnayowatendea watanzania masikini nyuma ya pazia wanadhani ninyi ni watu sana, kumbe ni chui mliovaa ngozi ya kondoo. Acheni kujitafutia laana kwa kuwatesa watanzania wahangaikaji pamoja na familia zao kwa manufaa yenu ya kisiasa.

Watanzania hawa wahangaikaji kwa kukosa pakupeleka malalamiko yao wamebaki wakiomba japo malaika wa huruma awaingie mioyoni mwenu muwakumbuke na kuwalipa stahiki zao. Hivi huwa mnawaza wanaishije huko mjini mlikowaweka?.

Sijamtaja mhusika kwa jina hapa na nimetumia uwingi ili tu kumstiri, na ndoto zake za ubunge zisijekupotea. Mhusika unajijua na ukiendelea kuleta ujeuri kwa kuwanyima ujira wafanyakazi wako; nitakutaja wewe na kampuni yako ya urithi ili watu wakujue ulivyo. Ndugu zetu wamegeuka omba omba mtaani na wapiga mizinga kwa sababu yako. Hebu fikiria miezi minne hata mia hujawalipa, unadhani kodi wanatoa wapi?, wanakula wapi? na wanatibiwa vipi wakipata maradhi?

Wahenga walisema "hisani huanzia nyumbani". Hebu kuwa na huruma.
 
Back
Top Bottom