Wanasiasa gani walipotea kisiasa baada ya kuingia migogoro na Serikali au chama tawala?

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Katika historia ya siasa za Tanzania, si kila anguko la mwanasiasa husababishwa na kushindwa uchaguzi. Mara nyingi, migogoro ya ndani ya chama, tofauti za kiitikadi au ukosoaji wa mamlaka huwa mwanzo wa kupungua kwa ushawishi wa kisiasa. Wapo waliowahi kuwa na nguvu kubwa jukwaani, lakini mazingira ya kisiasa yalibadilika ghafla na kujikuta wakisalia pembeni ya ulingo.

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
Nimejikumbusha hili baada ya kumuona nguli wa siasa za upinzani nchini, mchumi mbobevu Profesa Ibrahim Lipumba, akipitia mjadala mzito wa kisiasa kama waliowahi kupitia wengine kabla yake. Tarehe 13 Februari 2026, Msajili wa Vyama vya Siasa alikitaka Chama cha Wananchi (CUF) kufanya upya uchaguzi wa viongozi wa juu akieleza kuwa ofisi yake imepokea malalamiko kuhusu ukiukwaji wa taratibu katika uchaguzi uliompa ushindi Lipumba uliofanyika Desemba 2024.

Soma Mwisho wa enzi ya Lipumba ndani ya CUF

Duru za Siasa zinasema Profesa Lipumba alijisahau kama kakalia kuti kavu na kujikuta akianza kutoa matamko ya kuikosoa Serikali kuhusu uchaguzi mkuu wa 20225, tukirejea katika kauli yake ya Novemba 5, 2025 na Januari 27, 2026.

Pia soma Mirambo arithi mikoba ya Profesa Lipumba CUF

BIBI TITI MOHAMMED
Titi Mohammed huyu alihukumiwa kwa kesi ya Uhaini. Katika mahojiano aliyofanya na gazeti la RAI mwaka 1994., alisema kuanguka kwake kisiasa kulitokana na kumpinga Mwalimu Nyerere kwenye halmashauri kuu ya TANU, wakati Nyerere anatafuta kuungwa mkono na waislam ndani ya TANU baada ya kuivunja EAMWS. Soma Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

OSCAR KAMBONA
Oscar Kambona alikuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika TANU miaka ya mwanzo wa uhuru, akishika nafasi muhimu serikalini na chamani, na kuonekana kama mrithi wa Mwalimu Nyerere. Hata hivyo, mwaka 1967 baada ya Azimio la Arusha, alitofautiana vikali na uongozi juu ya mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi wa nchi. Hofu ya kukamatwa na mvutano wa kisiasa vilimsukuma kuondoka nchini na kwenda uhamishoni Uingereza. Akiwa uhamishoni alipoteza mtandao wake wa kisiasa na ushawishi wa ndani ya nchi. Aliporudi Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990, mfumo wa vyama vingi ulikuwa umeanza, lakini hakuweza tena kurejesha nafasi na nguvu yake ya awali katika siasa za kitaifa.

Soma The Rise and Fall of Oscar Salathiel Kambona

TUNTEMEKE SANGA
Tumtemeke Sanga anatajwa miongoni mwa wanasiasa wa awali wasomi waliokumbwa na misukosuko ya kisiasa katika kipindi cha chama kimoja. Alijitokeza kama kiongozi aliyekuwa na ushawishi katika siasa za wakati huo, lakini tofauti za msimamo na uongozi zilimuweka katika mgongano wa kisiasa. Baada ya kuingia kwenye mvutano huo na Mwalimu Nyerere, aliondolewa katika nafasi za uongozi, kufungwa kifungo cha ndani na kupoteza ushawizi

Pia soma - Tuntemeke Mesaka Nnnung'wa Sanga na Hoja ya Muungano mwaka 1993

CHRISTOPHER KASSANGA TUMBO
Kassanga Tumbo alikuwa miongoni mwa viongozi waliowahi kushika nafasi serikalini katika miaka ya mwanzo baada ya uhuru. Baada ya kutofautiana kisiasa na uongozi wa wakati huo, aliondolewa katika nafasi za madaraka na kupoteza ushawishi wake wa kitaifa.

Soma
Kuna wengine ambao hawakuathirika sana na mkono wa Serikali au chama tawala hasa kutokana na ukweli kuwa wakati wao ulikuwa umeisha, Wanasiasa kama Hayati Lowassa na Mzee Sumaye ambao walipata kuwa Mawaziri Wakuu walikumbana na mkwamo wa kisiasa baada ya kuhamia CHADEMA uchaguzi mkuu wa 2015 na baadaye walilazimika kurudi CCM baada ya kupata usumbufu katika miradi yao.

Soma
Ongeza wengine
 
Lipumba alipotea kwenye siasa baada ya kukubali kutumika na ccm dhidi ya upinzani uchaguzi wa 2015. Huku kwingine hadi anaondolewa juzi alikuwa ameishapotea.
 
Kipindi kile aliwasaliti UKAWA kisa vipande vya fedha, hakujua CCM ni mashetani
 
COVID 19 na chaumwa!
 
Lipumba alipotea kwenye siasa baada ya kukubali kutumika na ccm dhidi ya upinzani uchaguzi wa 2015. Huku kwingine hadi anaondolewa juzi alikuwa ameishapotea.
a.k.a muzee ya buguruni!
 
Imran Kombe nasikia naye alipotezwa baada ya kusema CCM kimepoteza mvuto. Aliuawa akidhaniwa kuwa mwizi wa gari. Cha kushangaza alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, swali tunalolijua kuwa wale askari walikuwa hawamjui aliyewahi kuwa boss wa TISS?
 
Mchana anakuwemo kwenye mikutano ya kiusalama usiku yote yalioongelewa anamfikishia home boy wake Mrema.

Mkapa akapewa taarifa, watu wa mfumo wakashughulika nae. Akaja Apson baadae ambaye pia alikuwa mtuwa Lowassa, nadhani JK alimshughulikia kimya kimya.
 
Back
Top Bottom