Nafikiri kuna hoja hapa. Tunawapima wanasiasa na viongozi wetu kwa hoja na matendo yao. Hii forum inatoa nafasi ya pekee kujua misimamo ya watu kiitikadi, kifalsafa na kisera. Inaeleweka kwa wananchi wa kawaida kama sisi kuficha majina yetu, lakini kwa kweli sio jambo zuri sana kwa viongozi na wanasiasa wetu.
Wananchi wa kawaida hawawajibiki kujulikana misimamo yao na isitoshe wana haki ya kuogopa na/au kusita kujitambulisha waziwazi kwa sababu za misingi za kikazi, n,k.,Lakini mwanasiasa na kiongozi, ambaye tayari yupo katika public domain, na moja ya kazi yake ni kutoa mchango wa mawazo katika jamii, analazimika na kwa kweli ni lazima tumjue msimamo wake wa kimawazo kwa mambo mbalimbali kama vile ufisadi, n.k.. Sasa wanapojificha wakati tunajua hawana blog na wala hawaandiki makala kwenye magazeti, tutajuaje misimamo yao? Matokeo ya kushindwa au kukataa kujitambulisha kwa njia ya mawazo ndiyo hayo yanasababisha, wakati wa uchaguzi, wanasiasa wetu wategemee kuhonga ili wachaguliwe badala ya kujinadi kwa misimamo ya kihoja. Tubadilike.