labda Hawana Majibu Ya Maswali Ya Wananchi Dhidi Ya Tuhuma Dhidi Ya Serikali Na Chama Chao. Umewasahau Wanasiasa Wengine Humu Waliojitambulisha Freeman Mbowe, John Mnyika, Kitila Mkumbo Bila Kumsahau Asha Abdala, Wote Kutoka Chadema.
Yani Hata Balozi Wa Nyumba Kumi Tu Naye Anaogopa Kujitambulisha Humu, Sasa Itakuwaje Kwa Chiligati Na Makamba Nk!
Asha
...hoja yake ili base kwa prominancy ya wanasiasa na hasa wale walio famous...
Wengine ni wafanyakazi wa serikali na waajiriwa wa mashirika ambao kwa wao tunapata datas na kuzipenyeza kwa wanasiasa. Sasa sisi hatuna haja sana ya kujulikana.
Siku na mimi nikitoka katika ajira na kujiunga na Si-hasa, nitaweka jina langu hapa jf ...
Nafikiri kuna hoja hapa. Tunawapima wanasiasa na viongozi wetu kwa hoja na matendo yao. Hii forum inatoa nafasi ya pekee kujua misimamo ya watu kiitikadi, kifalsafa na kisera. Inaeleweka kwa wananchi wa kawaida kama sisi kuficha majina yetu, lakini kwa kweli sio jambo zuri sana kwa viongozi na wanasiasa wetu.
Wananchi wa kawaida hawawajibiki kujulikana misimamo yao na isitoshe wana haki ya kuogopa na/au kusita kujitambulisha waziwazi kwa sababu za misingi za kikazi, n,k.,Lakini mwanasiasa na kiongozi, ambaye tayari yupo katika public domain, na moja ya kazi yake ni kutoa mchango wa mawazo katika jamii, analazimika na kwa kweli ni lazima tumjue msimamo wake wa kimawazo kwa mambo mbalimbali kama vile ufisadi, n.k.. Sasa wanapojificha wakati tunajua hawana blog na wala hawaandiki makala kwenye magazeti, tutajuaje misimamo yao? Matokeo ya kushindwa au kukataa kujitambulisha kwa njia ya mawazo ndiyo hayo yanasababisha, wakati wa uchaguzi, wanasiasa wetu wategemee kuhonga ili wachaguliwe badala ya kujinadi kwa misimamo ya kihoja. Tubadilike.
Na mimi la kwangu ni la kwangu hivyo tupo wenye majina yetu humu.
Ndugu Kasheshe naomba unijibu jawabu la kweli, jee na wewe umeficha jina lako au kweli unaitwa Kasheshe ?
Ina umuhimu gani kwa hao wanasiasa kutumia jina kamili kama wanagoma kujibu hoja? Nilishangaa Mh. Dr.Slaa alipomsikiliza Asha na kuacha kujibu maswali yangu ilikuwa ni halali yake. Bado nasubiri majibu yake na nitamkumbushia akija tena mtandaoni.
Waoga tupu hawa nani ana uwezo huo wakati wanafikiri iko siku nao watapata nafasi ya kufisadi? Hawa wote si unasikia wameamua kula jiwe kama vile hawapo wala hawaoni nchi ya wajukuu wao inavyomezwa?Niliwahi kumsikia Kiula anakoromea serikali hii lakini naye si fisadi? kwani anaweza kujivua hiyo? Tena aliwahi kutolewa kafara! Wengine katika orodha yako hakuna wa kujaribu hata kukooaVipi ambao ni wanasiasa lakini sio 'famous,' Nalaila Kiula, Richard Mja, Hawa Ghasia, Kitila Mkumbo, Juma Mkate?
Labda hawana majibu ya maswali ya wananchi dhidi ya tuhuma dhidi ya serikali na chama chao. Umewasahau wanasiasa wengine humu waliojitambulisha Freeman Mbowe, John Mnyika, Kitila Mkumbo bila kumsahau Asha Abdala, wote kutoka CHADEMA.
Yani hata balozi wa nyumba kumi tu naye anaogopa kujitambulisha humu, sasa itakuwaje kwa Chiligati na Makamba nk!
Asha
Ni aibu ya hali ya juu mwanasiasa ambaya anasema anatetea wananchi kuficha jina lake halisi akiwemo humu JF!
Binafsi nampongeza Dr. Slaa na Mh. Zitto kwa mara nyingine kuweka majina yao wazi... na hivyo pia kujua maoni yao katika mambo mbalimbali.
Ni heshima wanasiasa kuweka wazi majina yenu ili kuifanya JF kuwa chombo cha habari cha kuheshimika... na kupunguza wale wenzetu wanaofanya hapa ni mahali pa kupiga soga!
Mwanasiasa imara huwa hana woga wa kutoa maoni yake asikike! hata hivyo pia kwa kuwa wazi ana-promote transparency kwenye jamii yake.
Kwa vyovyote vile mnapoingia hapa kuna mnavyopata na tunawasikia mkitoa hoja kule kwenye lile jumba tukufu... tunaona kabisa maoni mumeyatoa hapa... ni wajibu wenu pia kurudishia jamii kidogo (social responsibility) kwa kutoa mawazo yenu ya ujumla na ya namna gani mnapenda JF iwe!
Mukiweka majina yenu... lengo la JF kuwa ya forum/jukwaa la KiJamii itakuwa imekamilika na kwa hakika tutaonekana sisi ni wazalendo wa hali ya juu kwa taifa letu.
Mwisho wenzetu mnaopenda matusi, kejeli na personality tupunguze tena ili kuvuta watu wengi makini.
Nikiingia kwenye Siasa YES... by then I will be Public figure... sasa hivi ni Private figure... kwi kwi kwi
Wajitambulishe Kwenye Forum Ya Chama Kingine.....!