Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 82
Ni aibu ya hali ya juu mwanasiasa ambaya anasema anatetea wananchi kuficha jina lake halisi akiwemo humu JF!
Binafsi nampongeza Dr. Slaa na Mh. Zitto kwa mara nyingine kuweka majina yao wazi... na hivyo pia kujua maoni yao katika mambo mbalimbali.
Ni heshima wanasiasa kuweka wazi majina yenu ili kuifanya JF kuwa chombo cha habari cha kuheshimika... na kupunguza wale wenzetu wanaofanya hapa ni mahali pa kupiga soga!
Mwanasiasa imara huwa hana woga wa kutoa maoni yake asikike! hata hivyo pia kwa kuwa wazi ana-promote transparency kwenye jamii yake.
Kwa vyovyote vile mnapoingia hapa kuna mnavyopata na tunawasikia mkitoa hoja kule kwenye lile jumba tukufu... tunaona kabisa maoni mumeyatoa hapa... ni wajibu wenu pia kurudishia jamii kidogo (social responsibility) kwa kutoa mawazo yenu ya ujumla na ya namna gani mnapenda JF iwe!
Mukiweka majina yenu... lengo la JF kuwa ya forum/jukwaa la KiJamii itakuwa imekamilika na kwa hakika tutaonekana sisi ni wazalendo wa hali ya juu kwa taifa letu.
Mwisho wenzetu mnaopenda matusi, kejeli na personality tupunguze tena ili kuvuta watu wengi makini.
MWANAMALUNDI said:Hilo jina la kasheshe ni la kwako??? Kumbuka mwanasiasa ni binadamu kama wewe. Ina maana na wewe ukijiunga na siasa utaweka jina lako la kweli hapa JF???
Tunachoangalia hapa ni hoja na si nani katoa hiyo hoja.
Nikiingia kwenye Siasa YES... by then I will be Public figure... sasa hivi ni Private figure... kwi kwi kwi
Wewe sio Rostam? Tumia lako la kweli basi... 🙂