Wanasiasa msitumie imani zetu kisiasa

Wanasiasa msitumie imani zetu kisiasa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Waumini ni wakati wa kujiuliza maswali machache badala ya kushabikia chochote kinachosemwa na wanasiasa. Tunavyosema Mungu katusaidia Tanzania pekee si kweli na tusimuhusishe Mungu na agenda zetu za kisiasa.

1. Je, Mungu ana weza kusaidia watu akaishia Namanga pale na kusema siwasaidii Kenya?

2. Je, Mungu ana mipaka? Hii mipaka ya nchi imewekwa na wakoloni Mungu hana mipaka. Mfano kama una ndugu yako anasoma India na kukatokea milipuko huko, je maombi yako hayata mfikia kwasababu yuko nje?

Hao wanaosema Mungu anatusaidia sisi tu na sala zetu zinaishia mipakani huo ni uchawi si Mungu. Mungu hana mipaka na atasaidia watu sehemu yeyote na wakati wowote. Kuna watu wanaanza kuamini kila kitu kinachosemwa na wanasiasa kama vile wenyewe ndiyo Mungu.

Yaani eti mwanasiasa akisema Corona iishe nayo inaisha, wanasiasa wakienda kanisani wenyewe ndiyo wana ongea kama vile Mungu anajali vyeo. Hii sio Tanzania pekee lakini lindeni familia zenu na msiamini wanasiasa na kila kitu wanachoisema.

Wengi wa wanasiasa ni kutumia saikolojia kuwaongoza mpaka hapo mtakapo gundua ukweli.
 
WARUMI 13:1
Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
 
Back
Top Bottom