Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Miaka ya nyuma kidogo Mkoani Tabora kuna Mwanasiasa aliyekuwa akigombea Ubunge aliwahi kufunga TV kubwa Pale soko maarufu kwa jina la Soko kuu.
Aliifunga wakati wa kuelekea kampeni za uchaguzi akalipia na king'amuzi watu wakawa wanatazama mechi bure ikiwemo na kulipia kahawa na kashata watu walipata bure.
Mbinu hiyo huenda imekopiwa na wanasiasa wengine kwani hapa Dar karibu na Stendi ya Magufuli kwenye soko kuna TV imefungwa hapo
Najiuliza nani aliifunga na nani anagharamia gharama za king'amuzi au ndiyo mbinu zilezile za kuelekea uchaguzi kuwadanganya raia waone kuwa wanajaliwa?
Wanasiasa wamekuwa na mbinu nyingi sana, mara wengine wagaregare chini ilimradi tu kuhadaa wananchi waweze kuwachagua.
Hivyo, si ajabu tukaanza kuona vitu vingi vya ofa kama hizi TV na vitu vingine vikigawiwa bure ili tu kuwashawishi wananchi kwa hongo iliyojificha kwa kivuli cha msaada.