DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa ujuzi wangu na navyowajua Ega hawana uwezo wa kutengeneza mifumo waliyonunua TRA wala TANESCO hata asilimia 10. Ile ni mifumo mikubwa inayotumika Duniani.

Ega ukiangalia tu website za serikali unaweza kujua ni watu wa uwezo gani halafu wapewe kutengeneza mifumo mikubwa kama ya TRA ama TANESCO kweli?

Sio kila kitu lazima kifanywe na wataalamu wetu wakuu. Vitu vingine viko juu ya wataalamu wetu.

Mkuu nadhani utakua mgeni kwenye tasnia ya Tehama, ukisema mfumo mkubwa unmaanisha nini?
 
kuna magenge yameshakata vitaru kwenye sekta za ICT ,yanaona kama ni halali kubinafsisha ICT industry , ukiwakuta mzee wanapanga mikakati kama zimo kumbe majivu tupu
We acha tu!! huko ndiko uchochoro wa makontena yasiyo lipiwa kodi, kisha TRA wanajifanya hawajui kutwa kusumbua watu mtaani. Kuna bandari kavu moja wakifungua loose cargo konteina 7 basi 2 hazilipi kodi
 
na kuna mbunge juzi anasimama kumtetea kijanammoja eti ana akili sana , moyo uliwaka kwa hasira , kijana anayetetewa ana miliki kampuni ambayo kawekwa na wanasiasa, anapiga pesa anawapa mabwana zake wana siasa ni aibu kubwa sana na wanasiasa wanajua mpaka wamefungua tawi Dubai , ni genge la kihalifu lipo serikalini linaendelea na kazi wengine ni viongozi wakubwa sana
Iko hivyo mkuu.

Haya mafisadi ni hatari mno.

Ni wezi wa kimkakati.
 
nchi ni kubwa na ina mambo mengi ,baadhi ya wasaidizi wake ni maharamia
Kuepuka hili ndio maana watu tunataka structure mpya ya Nchi ili impunguzie hizo shida! itamfanya abakiwe na mambo machache atakayo yamudu
ila Cha kusikitisha hataki anateua mutungi atengeneze Katiba
 
Watu wa E-GA mmesikia ya bandar? kituo kinachofuata ni E-GA kubinafsishwa period
japo bandarini kuna mixed feeling ,
 
E-GA ni taasisi inayoratibu serikali mtandao, ni taasisi ambayo inajenga mifumo karibu mingi sana inayotumika na serikali.

Serikali imeokoa pesa nyingi sana kutoka nje ya nchi na imetoa ajira kwa wazawa. Zaidi sana taarifa na usiri ama unyeti wa taarifa za serikali umeongezeka baada ya mifumo ya ndani kuanza kutumia

Nini kinaendelea kwa sasa?
wanasiasa kadhaa ambao sitawataja leo wanaratibu mpango wa kuiua E-GA ili mifumo ya serikali ianze kutengenezwa nje /ku out source kwa jina la kiluguru.

Je hawa wanasiasa wananufaikaje?
wanasiasa hawa wamesha weka hisa zao kwenye kampuni kadhaa ndani na nje ya nchi ambazo wakisha iua EGA , watazipa kandarasi hizo kampuni ambazo nyuma ya pazia ni zao , wanakuja kwa mgongo wa sekta binafsi lakini ukweli sio sekta binafsi , ni matumbo binafsi.

Mpaka sasa wamefanikiwa kuwang'oa E-GA TRA , tayari TRA anakamilisha ununuzi wa mfumo kwa zaidi ya Bilion 12 za kitanzania(TZS).

Mfumo mwingine TANESCO upo njiani.

Hali ni mbaya sana, wanamtafuta Mkurugenzi wa E-GA ikibidi auawe maana anakwamisha madili

************************* UPDATES********************
Taarifa Mpya tulizozipata zinaeleza juu ya uhusika ya Viongozi waandamizi toka taasisi mbalimbali za serikali na wanasiasa kadhaa kusuka mpango huu wa kuifuta E-GA . Script iko kama hapa chini.

1.E-GA iwe moved from ofisi ya rais utumishi kwenda Wizara ya TEHAMA chini ya Waziri Nape Nnauye.
2. Ikishafika wizara ya TEHAMA , haraka haraka mswaada wa kuninafsisha mashirika na taasisi kadhaa za umma utapitishwa , na moja ya taasisi za kubinafsishwa itakua ni E-GA.

3. Wakisha kubaliana bungeni, E-GA itachukuliwa rasmi na kikundi flani ambacho kitakua kimetegesha Kampuni flani kuimeza E-GA.

4. Watumishi waliopo E-GA baadhi watasambazwa kwenye taasisi mbali mbali wengine watabaki kwenye hio kampuni binafsi , kama ilivyo kwa AIRTEL ambapo serikali ina share kadhaa.


Rai yangu: Waziri Nape Nnauye huu ni mtego unategewa , ng'amuka mapema , unaangushiwa jumba bovu .
NOTE: Majina ya wahusika yapo tayari , hayatakua shared hapa kulinda policy za platform hii.
Kumbe figisu zilianza kitambo
 
Kumbe figisu zilianza kitambo
watu wamejipanga ,wameanza kuimega E-GA kuna kazi zake zinagawanwa ,sasa hivi NEST iko PPRA badara iwe E-GA
miezi si mingi kuna service inaitwa ERMS kuna taasisi itapewa jukumu la kuunda mfumo huo, maana yake wanataka E-GA abaki kama mlinzi wa banki, pesa zote sio zake
 
watu wamejipanga ,wameanza kuimega E-GA kuna kazi zake zinagawanwa ,sasa hivi NEST iko PPRA badara iwe E-GA
miezi si mingi kuna service inaitwa ERMS kuna taasisi itapewa jukumu la kuunda mfumo huo, maana yake wanataka E-GA abaki kama mlinzi wa banki, pesa zote sio zake
NEST imejengwa na nani PPRA wanasema October ndiyo unaanza kutumika
 
Rais Samia ikikupendeza leta wataalamu toka taasisi tambulika huko duniani, waje watengeneze mfumo imara wa e Govt, hakuna lingine wezi watapata tabu sana,
Wasimamizi wa mifumo hii wawe waajiriwa toka ngambo!.
Kampuni tiifu zenye principle imara.
 
Rais Samia ikikupendeza leta wataalamu toka taasisi tambulika huko duniani, waje watengeneze mfumo imara wa e Govt, hakuna lingine wezi watapata tabu sana,
Wasimamizi wa mifumo hii wawe waajiriwa toka ngambo!.
Kampuni tiifu zenye principle imara.
Hujielewi kabisaa
Ishu ya Mifumo ya Gvt uipe kampuni binafsi kweli?? Usalama wa taarifa zako zitakuwa salama kweli??!
 
Rais Samia ikikupendeza leta wataalamu toka taasisi tambulika huko duniani, waje watengeneze mfumo imara wa e Govt, hakuna lingine wezi watapata tabu sana,
Wasimamizi wa mifumo hii wawe waajiriwa toka ngambo!.
Kampuni tiifu zenye principle imara.

Hana ubavu huo wala nia tu.
 
IMG_5284.jpg
 
Back
Top Bottom