Wanasiasa na ubinafsi wa Katiba mpya

Wanasiasa na ubinafsi wa Katiba mpya

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari wanaBodi..

Tumekuwa tuna wanasiasa wanafki na wabinafsi pia sana.

Watanzania tuna changamoto nyingi za maisha ya kila siku mbali na suala la KATIBA, Yes Katiba ni muhimu lakini Katiba siyo kila kitu, tunaweza kuwa na Katiba mpya lakini isibadilishe maisha ya raia.

Ubinafsi wa Wanasiasa wa Tanzania huwezi kusikia hata siku moja wakipinga bei za Petrol kupanda,bei ya sukari kupanda,bei ya mafuta ya kula kupanda,gharama ya miamala ya simu kupanda wala wakipinga wafanyabiashara kupandishiwa kodi.

Wakati ndiyo mambo ya msingi na mahitaji muhimu ya binadamu kila siku. Labda kwa sababu wao wanalipwa posho za Ubunge na ruzuku za Vyama hivyo mambo kama hayo wao siyo ya muhimu.

Ubinafsi wa Wanasiasa wetu ni kutaka tu kutwaa tu madaraka lakini sidhani kama kweli wana nia ya dhati ya kuwakwamua wananchi wala kuwatetea, wangekuwa na nia hiyo wangeyazungumzia pia mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

My take : Katiba mpya ni kwa maslahi ya wanasiasa wala siyo kutatua changamoto za Watanzania.
 
Tamaa za madaraka na kujitajirisha ndyo shida ya taifa hili kila mtu anataka akae kwenye ile meza ya chakula
 
..kwanini unasubiri wanasiasa wakusaidie kupinga kupanda kwa bei ya mafuta, sukari , nk?

..je, unajua kwamba watawala waliokupandishia bei ya mafuta na sukari wana katiba ya zamani wanayoiunga mkono?

..je, kwa katiba hii ya zamani unadhani watawala wamekupa haki za kupinga kupanda kwa bei za bidhaa ambazo ni muhimu kwako?
 
Habari wanaBodi..

Tumekuwa tuna wanasiasa wanafki na wabinafsi pia sana.

Watanzania tuna changamoto nyingi za maisha ya kila siku mbali na suala la KATIBA, Yes Katiba ni muhimu lakini Katiba siyo kila kitu, tunaweza kuwa na Katiba mpya lakini isibadilishe maisha ya raia.

Ubinafsi wa Wanasiasa wa Tanzania huwezi kusikia hata siku moja wakipinga bei za Petrol kupanda,bei ya sukari kupanda,bei ya mafuta ya kula kupanda,gharama ya miamala ya simu kupanda wala wakipinga wafanyabiashara kupandishiwa kodi.

Wakati ndiyo mambo ya msingi na mahitaji muhimu ya binadamu kila siku. Labda kwa sababu wao wanalipwa posho za Ubunge na ruzuku za Vyama hivyo mambo kama hayo wao siyo ya muhimu.

Ubinafsi wa Wanasiasa wetu ni kutaka tu kutwaa tu madaraka lakini sidhani kama kweli wana nia ya dhati ya kuwakwamua wananchi wala kuwatetea, wangekuwa na nia hiyo wangeyazungumzia pia mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

My take : Katiba mpya ni kwa maslahi ya wanasiasa wala siyo kutatua changamoto za Watanzania.
Katiba ikirekebishwa hayo yote yatakaa sawa
 
Back
Top Bottom