Wanasiasa na Wakurugenzi hamtumii mitandao ya kijamii ndo maana Gen Z wanaishia kuwaona kina Gigi Money na Baba Levo kama Role Models wao

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Juzi umeme ulikuwa umekatika kwangu, ikabidi niende kwa jirani yangu kupoteza muda kidogo nikisubiri umeme urudi.

Jirani yangu (anaelekea utu uzima) ana watoto 3. Mmoja yuko nursery na hao wengine wawili wapo shule ya msingi.

Wakati nimekaa pale nikawa napiga story mbili tatu na wale watoto.

Katika kuongea nao nikawauliza role models wao ni kina nani. Mmoja akaniambia anataka kuwa kama Chino, yule wa kike akamtaja Hamisa Mobeto na huyu mkubwa akasema Hanscana.

Yaani wote role models wao ni wasanii na hawa celebrities.

chino.png

Hakuna mtoto hata mmoja aliyesema anataka kuwa kama Mwalimu Nyerere, Profesa Janabi au hata Tulia Ackson au Isaac Maro au mtu yeyote asiyejulikana lakini anafanya vizuri

Watoto wanamezeshwa content za wasanii tu na wanahisi maisha ni Instagram na kupiga picha. Likes na followers kwao ndo kipimo cha mafanikio.

Tanzania hatuna celebrity doctors, engineers marketing officers, psychologists or politicians au CEOs ambao wanaonesha maisha mazuri wanayoishi.

Baada ya miaka 15, tutakuwa na taifa la hovyo ambalo kila mtu anataka kuwa mkata viuno kama Diamond au chawa kama Mwijaku
 
Kibaya zaidi ni kwamba hao uliowataja (doctors, engineers, marketing officers, polisi etc) licha ya kutokuwa celebrities bado wanapondwa sasa kwenye mitandao kuwa watu wenye maisha magumu sana kwa hiyo hao watoto wakiingia mitandaoni stori wanazokuta za Prof Janabi nyingi ni hasi (negative).

Kwa hiyo ni wazi kwamba wakati ujao hali haitakuwa nzuri sana, kwa sababu kila binadamu hupenda kizuri.
 
Wakuu,

Juzi umeme ulikuwa umekatika kwangu, ikabidi niende kwa jirani yangu kupoteza muda kidogo nikisubiri umeme urudi.

Jirani yangu (anaelekea utu uzima) ana watoto 3. Mmoja yuko nursery na hao wengine wawili wapo shule ya msingi.

Wakati nimekaa pale nikawa napiga story mbili tatu na wale watoto.

Katika kuongea nao nikawauliza role models wao ni kina nani. Mmoja akaniambia anataka kuwa kama Chino, yule wa kike akamtaja Hamisa Mobeto na huyu mkubwa akasema Hanscana.

Yaani wote role models wao ni wasanii na hawa celebrities.

Hakuna mtoto hata mmoja aliyesema anataka kuwa kama Mwalimu Nyerere, Profesa Janabi au hata Tulia Ackson au Isaac Maro au mtu yeyote asiyejulikana lakini anafanya vizuri

Watoto wanamezeshwa content za wasanii tu na wanahisi maisha ni Instagram na kupiga picha. Likes na followers kwao ndo kipimo cha mafanikio.

Tanzania hatuna celebrity doctors, engineers marketing officers, psychologists or politicians au CEOs ambao wanaonesha maisha mazuri wanayoishi.

Baada ya miaka 15, tutakuwa na taifa la hovyo ambalo kila mtu anataka kuwa mkata viuno kama Diamond au chawa kama Mwijaku
Kwani kuwa msanii ni vibaya
 
Back
Top Bottom